Yanayoendelea sasa hivi nchini ni hatari kwa uhai wa chama kilichopo madarakani na baadhi ya viongozi waliopo Serikalini

Huwezi kutumia Siasa katika kutoa majibu yanayohitaji ujuzi wa Kitaalamu. Sasa hivi kanywea kama piritoni uwezo huo hana tena. Tusubiri wakati wanajadiri ripoti hiyo halafu tuone mchango wake hapo Bungeni ndio mtajua huyu ni nani hasa.
Aibu kubwa sana
 
Ebooh! Kwani Yeye ndiye alikuwa anaagiza hazina wafanye malipo?

Hahusiki na haya ndio maana aliagiza CAG kwamba asing'ate ulimi.
 
Usiwe kama mtu usielewa huyo alikuwa amebanwa hata kusema hawezi mwendazake aliifanya nchi kama kampuni yake
Kwahyo Samia ambaye alikua makamu, ni msafi kabisa. Ila tu Rais?

Yeye kama makamu wa Rais anakuaje msafi kwa yote hayo? Hivi ni chuki tu kwa Magu au kuna cha zaidi?
 
Ushawahi ona wapi Waafrika wanajiuzulu sababu ya kashfa...?
 
Muhimu viroba na kutekana kusiwepo tu
 
Lawama zinaenda kwa nahodha wa chombo kwani ndio huwa na kauli ya mwisho! Halafu kuna kitu kinanishangaza iweje lawama mzikatae wakati sifa alikuwa anapewa peke yake? Ukikubali kushangiliwa ujue pia kuna kuzomewa! Hii kule mkekani tunaita both team score
 
kwenye familia marehemu akifa unafikiri jambo gani hutokea?
 
Kwa kujua kuwa wanakanusha katiba wajiwekea kinga ya kutoshtakiwa. Kumbuka kama kuna suala nyeti bungeni linalohusu kupiga kura, mfano kura ya kutokuwa na imani na spika, haiwezekani hata siku moja uongozi wa bunge ikakubali ipigwe kura ya siri, itapigwa kura ya wazi. Sasa ni mbunge gani wa CCM ana ubavu wa kusema ndiyo naunga mkono hoja ya kumuondoa spika! Bunge nalo ni maigizo tu. Wanapitisha bajeti isiyokuwa na ununuzi wa ndege wala SGR, Lakini ndege zinaaminika, kinachofuata ni kurap pongezi tuuu! Bila Transparency na Rule of Law hayo mambo ya ufisadi yatadumu milele na milele. Ndiyo maana tunasema kuliko kujenga daraja la surrender Bora angejenga mfumo wa utawala ikiwemo katiba mpya yenye kuzingatia maoni ya wananchi ikiongozwa na rasimu ya tume ya Warioba! Hata Mama Samia ikilikwepa hili, hawezi kufika mbali. Serikali, Bunge, Mahakama na vyombo vya habari viwe independent!
 
Kwahyo Samia ambaye alikua makamu, ni msafi kabisa. Ila tu Rais?

Yeye kama makamu wa Rais anakuaje msafi kwa yote hayo? Hivi ni chuki tu kwa Magu au kuna cha zaidi?
Hakuna Mwenye Shida. Tatizo lipo kwa Wakaguzi. Sheria za ukaguzi wa Mahesabu ya Serikali kwanza ziliandaliwa na Wahasibu kwa kushirikiana na Wagavi. Lengo lao likiwa ni kuhakikisha Wananufaika kulingana na taaluma zao. Sasa baada ya Mfumo kubadilika kuanza kutumia F akaunti wao walikuwa hawana pa kupigia kutokana na utaratibu kubadilika fedha za miradi kusimamiwa moja kwa moja na Wananchi ndiyo maana miradi iko poa.
Mifumo ya kuisimamiwa na wananchi wanafanya manunuzi kwa bei ya Soko siyo ile ya kujiongezea mfano bati la 20000 linanunuliwa 50000 au 60000 na kuingiza hasara Serikali.
Kutokana na Hali hiyo kuna watu hapo walichanganywa na Mfumo huo ambao ni
1. Wazabuni
2. Wakandarasi
3. Wahasibu
4. Wakuu wa Idara
5. Wakurugenzi
6. Wakaguzi
N.k. Kutokana na Hali hiyo wanatumia kila mbinu kuu disaapoint Mfumo wa usimamizi wa Wananchi moja kwa moja.
Na Uzuri wananchi tumeisha jua janja yao. Wakituzingua na cc ni wajumbe tuna Jambo letu. Ukituzingua na cc tutakukanyaga ili tu tusonge mbele.
 
Kama na wewe ni great thinker, basi Taifa hili bado lina safari ndefu. Muda huu uliotumia kuandika pumba hizi ni Heri ungelimsaidia mkeo kuchambua mchele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…