Yanayoendelea sasa hivi nchini ni hatari kwa uhai wa chama kilichopo madarakani na baadhi ya viongozi waliopo Serikalini

Yanayoendelea sasa hivi nchini ni hatari kwa uhai wa chama kilichopo madarakani na baadhi ya viongozi waliopo Serikalini

Kwa ufisadi mkubwa ulioibuliwa na CAG uliofanyika awamu ya tano, makamu wa Rais wa kipindi hicho anakuwaje msafi ilihali ndiye aliyekuwa mtendaji wa karibu zaidi na Rais?

Tukiacha siasa, ni dhahiri kabisa haya yote yametendeka kutokana na uzembe wa mwendazake na wasaidizi wake akiwemo Rais wa sasa.

Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.
Mtu alishasema yeye jiwe, tangu lini jiwe likashaurika? muache Mama atuongoze ni zam yake, hutaki hama nchi.
 
We, we, we! Mtu ana bastola kiunoni na ametangaza hapangiwi. Hata kumshauri kungeweza kuleta madhara makubwa!

Naona kuna upepo mwanana. Ukweli haufichwi hata kama ni mchungu. It is a new beginning. Hongera Rais Samia Suluhu Hasan kwa kutoa RUKSA kusema ukweli.

TAKUKURU waangalie asikimbie mtu. Kila aliyeiba na azitapike hizo fedha.
 
Kwa ufisadi mkubwa ulioibuliwa na CAG uliofanyika awamu ya tano, makamu wa Rais wa kipindi hicho anakuwaje msafi ilihali ndiye aliyekuwa mtendaji wa karibu zaidi na Rais?

Tukiacha siasa, ni dhahiri kabisa haya yote yametendeka kutokana na uzembe wa mwendazake na wasaidizi wake akiwemo Rais wa sasa.

Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.
Kwa Katiba ipi? Vyama vipi vya siasa? Taasisi zipi imara? Na wananchi wepi wanaojitambua kiasi Cha kushinikiza waliopo madarakani ambao ni zao lile la ufedhuli na ufisadi wa kutisha??

Usiwe kama wale mashabiki wakibongo wa soka la Ulaya wanaotamani Yanga icheze kama Sevilla...!!
 
Kwa ufisadi mkubwa ulioibuliwa na CAG uliofanyika awamu ya tano, makamu wa Rais wa kipindi hicho anakuwaje msafi ilihali ndiye aliyekuwa mtendaji wa karibu zaidi na Rais?

Tukiacha siasa, ni dhahiri kabisa haya yote yametendeka kutokana na uzembe wa mwendazake na wasaidizi wake akiwemo Rais wa sasa.

Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.
Hausiki hata CHEMBE msitafute Kwa kukimbilia!
 
Huu mchezo nadhani unasimiwa na watu ambao kwasasa masilahi yao hayapo ndani ya ccm sasa wanaamua kukoroga mambo.

Ukitazama the late magufuri amefanya mambo mengi sana ndani ya muda mfupi sana wa miaka mitano, NO ONE HAS SUCH RECORD....

Hakuna uongozi utakuja hapa duniani bila kupewa tuhuma za ubadhirifu wa pesa na mamlaka.

Ila kiongozi wa kweli huacha ishara ya tofauti ambayo huwa ni matokeo ya moja kwa moja ya jitihada zake...

Magufuri ameacha hiyo ishara kwa vitu ambavyo ameshafanya kwa usimamizi wake....

Wanafiki hawatakosekana katika kumchafua.... Ila subiri.... Muda ndio huonyesha nani alikuwa mkorofi.... Ipo siku wale mnaosema ni mbaya mtaona mazuri yake......

Kwasasa subira ni kitu muhimu....

Ila kiukweli kila ninaposafiri kuwa najionea mabadiliko ambayo kila ukiuliza siambiwi ni Mzee wetu kikwete au Mkapa walifanya bali naambiwa ni Mzee wetu Hayati Magufuri.

Kila nikipita pale ubungo kuelekea mwenge au nikirejea kutoka mwenge huo najisikia sana fahari....

Naweza kupita hata kama sikuwa na haja ya kuzunguka upande ule kuelekea town ila huwa naona ufahari wa hali ya juu kupita pale mahala....

Mzee mazuri yake amefanya hata kama mtamsema kwa roho mbaya....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakulaumiwa ni wale wote waliohusika na ufisadi huu na sio hayati Magufuli tu ndo atupiwe lawama zote
...hayati anahusika makamu wake anahusika Waziri mkuu na mawaziri ambao wizara zao zimeguswa wanahusika pia ilipaswa hawa wote wajiuzuru nyazifa zao maana wamesababishia Nchi hasara kubwa wakati mda wote walikuwa wanatamba majukwaani kwamba wamezibiti ufisadi na kujisifu kwa serikali yao kununua ndege na kujenga SGR...chakushangaza lawama anatupiwa hayati wakati hawa ndio walikuwa washauli wake na waziri mkuu ndie msimamizi wa shughuri za serikali
 
Anapumulia mashine kwa sasa maana wenye nafasi zao bado kitambo kidogo wanarudishiwa , soon anarudi kwenye uanaharakati wake na ndio kutakua na unafiki uliodhihirika just kipindi kifupi tu baada ya mkuu wa malaika kututoka
 
Kuna sheria ya kikatiba ya kuwalinda hawa kwa hizi hoja zako? Au kuwasaidia Bunge likisema linapiga kura ya kutokuwa ba imani.
Jiwe alipoamua kuikanyaga katiba ndipo hayo yote yalipo pata kasi. Njia iliyoonekana inawafaa kwake ni kutunga sheria ya kuwapa kinga wanaokumbatia uharifu - kinga kwa rais, spika na Jaji mkuu. Mimi nasema ANASTAHILI LAWAMA NA LAWAMA HIZI ZIMFUATE HUKO ALIKO BILA KUPINDA PINDA. Sasa unaminya uhuru wa wananchi kuongea, kutoa maoni, unafungia magazeti ya uchunguzi unaacha TANZANITE NA UHURU unategemea matokeo gani? Wajuzi wa kuibua hoja bungeni unawadhulumu haki yao ya kuchaguliwa, wananchi unawanyima haki yao ya kuchagua kiongozi wanayemtaka unakusudia kufanya nini? We acha kutetea upuuzi! SPADE NI SPADE NA SPOON NI SPOON.
 
"NAAAM....!

Miradi yake mingine inaleta foleni kubwa kabisa kuwahi kutokea, haina maana ni hasara? Mbona ni rahisi tu, kwa nini tuendelee na Ma-foleni na Ma-hasara? Nashauri Vunjeni Madaraja na Flyovers zote, Ng'oeni reli zote hasahasa ya SGR, uzeni Ndege zote na vivuko vyote nchini, Uza Meli zote Mpya zilizozinduliwa kule ziwa Nyasa, simamisheni Ujenzi wa Bwawa la umeme tununue majenerata kwa wahindi tupate kodi, Gaweni Migodi yote kwa wawekezaji uchumi ukue, Binafsisheni Milima, Maziwa na Mbuga kwa watu binafsi tupate faida Bomoa Bandari zote zilizoboreshwa ikiwemo Mtwara, Tanga na Dar, Jengeni moja ya Wachina Bagamoyo kwa mkataba wa miaka 100. Rudisheni Ada mashuleni walimu walipwe vizuri tukuze uchumi, Wapeni Matajiri misamaha ya kodi waongeze mzunguko wa pesa, Ruhusuni Makinikia na gesi kwenda nje wawekezaji waongezeke zaidi tupate pesa, Vunjeni Masoko mapya ya Madini mikoani yakauziwe nje huko, Charaza Bakora Machinga mjini waache kusumbua watu, Mwaga wali wa Mama Ntilie wasituchafulie jiji, Vunja vyama vya wakulima na utaratibu wa stakabadhi ghalani umepitwa na wakati, Ruhusuni Uhuru wa Mashoga nao wana haki kama wengine, ruhusuni Chanjo ya Corona wasije wakatutenga, Msitumie nguvu kukabiliana na majangiri wa tembo tutafukuza watalii, Uhuru wa mateja kwa wingi mtaani nao ni ndugu zetu, Madawa ya kulevya sio yote yanalevya mengine yanalewesha tu kama bia n.k. Pia Msisahau kuifunga ile Mahakama ya Mafisadi sab ufisadi hauta isha hata hivyo, Kwa uchache tu Hakika hapo sasa pengine Tanzania itakuwa kama ULAYA, Tanzania ya Asali na Maziwa!.
 
Ila mama tusimlaumu , kwa sababu jamaa alikuwa ni dikteta, pengine mama alikuwa anamshauri sana, ila mwendazake kupotezea ushauri
 
Hivi wewe ni monde arabe?
 
Alishatamka yeye mwenyewe kwa kinywa chake kwamba Mara kadhaa alishataka kujiuzuru lkn baadae wakawekana sawa. Kamanda kwa ile style ya Magu wewe ungeweza pinga chochote? Waliopinga si uliona walivyokuwa wanashughulikiwa? Prof Assad alisema Kuna haja ya kujenga taasisi imara na si mtu imara. Mama hana hatia kabisa, Wala waziri mkuu hana hatia kabsaa, baba alitawala kwa mkono wa chuma! Hakuna wa kumpinga. Ndugu zako walikufa kwa korona, ulitoka hadharani kusema korona ipo?
Samia wakati madudu yanafanyika alikuwa wapi?
 
Back
Top Bottom