Aliyemtengua CAG aliyepita alikuwa mama Samia?Kwa ufisadi mkubwa ulioibuliwa na CAG uliofanyika awamu ya tano, makamu wa Rais wa kipindi hicho anakuwaje msafi ilihali ndiye aliyekuwa mtendaji wa karibu zaidi na Rais?
Tukiacha siasa, ni dhahiri kabisa haya yote yametendeka kutokana na uzembe wa mwendazake na wasaidizi wake akiwemo Rais wa sasa.
Msemakweli ni mpenzi wa Mungu.
Mnataka kumuonea mama wa watu bure kwa kuwa ndiye aliyekuwa makamo wake na tulishawahi kusikia huko nyuma mama alitaka kujiuzulu, basi tu ndiyo mipango ya Mungu ya kuwa yeye ndiye atakaye kuwa raisi.
Mzee Magu alikuwa anachagua ushauri.