Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Vijana wa kiafrika katika kusaka Hela. Huwa ni sawa tuko jehanamu. Kazi tunazozifanya hazilingani na kipato kunachokipata. Ni maumivu makubwa sana Tena Sana.
 
Hebu tuacheni unafiki

Kwani mmelazimishwa kufanya hizo kazi?

Utalipwa kutokana na thamani yako , ukiona mshahara hautoshi jiongezee thamani .

Tafuta fani ya ufundi , jifunze endeshea maisha..

Sio lazima mrundikane wote kiwandani.
Nyie ndo wale wale chawa wa ccm.. mnaojitoa ufahamu wa akili mkiwa chawa. Unafikiri watu wote wanaweza kujiajiri? Hujui nafasi ya serikali katika hili..
 

Kwa maana hiyo Elimu ndio kipimo cha Utu?

Elimu unayopewa na binaadam Kama wewe inapita vipi kiwango cha Utu ulichoumbwa nacho?
 
Once you are born in Africa life is automatically leading you 1-0.

And if you are not educated that's 2-0.

At this point you have no option than hustling like a donkey.

Educated in what sense?

Knowledge will take you even further n Life, places no amount of education you receive could ever afford them.

Knowledge illuminates all beings equally while Greed & Misconceptions portrays man made Education as reality.

Knowledge flows naturally, only to beings with open currents and free from brainwashing systems called education.

Knowledge has no limit nor boundaries.
 
Hebu tuacheni unafiki

Kwani mmelazimishwa kufanya hizo kazi?

Utalipwa kutokana na thamani yako , ukiona mshahara hautoshi jiongezee thamani .

Tafuta fani ya ufundi , jifunze endeshea maisha..

Sio lazima mrundikane wote kiwandani.

Kwahiyo wale wasioweza kuzitambua thamani zao waachwe waangamie?

Kuna dhambi gani kila binaadam akapata thamani Sawa na nafasi Sawa katika kujipambania katika uhai wake?

Kwamba akilipwa kila saa elf 5 badala ya Mia 5 huyo bilionea akashuka kuwa milionea na dunia ikatulia, shida itakua nini?

Binaadam tunatengeneza madaraja kati yetu tena kwa kupenda wenyewe lakini yakitukuta maafa tunaanza kutafuta mchawi.
 

Lakini bila huyo “unskilled person” huyo tajiri si chochote.

Kimsingi huyo unskilled person ndio engine ya kiwanda lakini anafanywa kama ndio dekio la kiwanda.

Ni ukweli uliopo lakini haina maana kwamba ndio Ukweli sahihi na unaopaswa kuwapo.
 
Mimi naona huu ni mpango wa serikali wa makusudi kabisa. Kuwafanya wananchi wake kuwa watumwa kwa kutumikishwa bila kujaali kwamba watanufaika au laa. Sio viwandani tu bali pia sehemu zote mishahara ni midogo sana angalia hata kazi za ulinzi watu wanalipwa kidogo sana.

Wakati mwingine hata hizi sera za siasa kwa pande zote mbili yaaani wapinzani na wanaotawala hakuna hata mmoja ambaye kipindi cha kampeni atagusia kuhusu ajira na malipo kwa wananchi wanaoingia kwenye ajira. Kwamba watashighulikia badala yake husema tu tutaongeza ajira bila kusema namna ya kuboresha maslahi kwanza.

Nchi yetu ipo kwenye wakati mgumu sana kuhusu maendeleo ya watu wake ndiyo maana ni rushwa na ujanja mwingi maeneo mengi ya kazi. Haiwezekani eti mtu analipwa kwa siku 5000 au laki Moja na nusu kwa mwezi.
 
Sasa mkuu unaposema hivyo, sio sahihi, kwani sasa hivi hata huyo aliyesoma sana, naye kipato anacholipwa ukiangalia kimahesabu ni sawa tu na huyo casual labour!! Juzi waziri wa kilimo anasifia kuwa sasa wahitimu wa SUA, watakuwa wanaajiriwa moja kwa moja kwenye makampuni ya pamba kwa mshahara wa tsh. 500,000 kwa mwezi sawa na karibia 17,000 kwa siku!! Hii si hatari?!!
 
Kweli. Rushwa na ufisadi ni kama vina baraka kutoka serikalini.
Mtu ana familia laki na nusu inamtosha kufanyia nini?
Hata kula mtu mmoja kwa mwezi haitoshi.
 
Kibongo bongo 500k ni mshahara mkubwa,
Walimu ndio wanakunja hio,
Polisi wanakunja hio,
 
Na huko wanalipa Tsh 400 kwa saa?
 
Kama ndoo ya plastiki ya cello inauzwa 2500 kariakoo kiwandani inauzwa shs ngapi? Unadhani gharama ya kuzalisha ndoo moja ni shs ngapi? Halafu wewe wakulipe shs ngapi? Muda mwingine mtumie vichwa vyenye nywele kufikiri, hiyo kazi ya elfu tatu kuna watu wamejenga na kusomesha watoto kwa hiyihiyo kazi na kuna watu wanahonga pesa kuipata hiyo kazi, uwe na adabu nyoko
 
Kujenga na kusomesha??😉😉
 
Wanazalisha ndoo moja kwa siku?
 
Mtumwa anaposifia utumwa.
Kama mfanyakazi wa kiwandani anajenga huyo ni aidha mwizi au hana akili yaani hali kama anavyopaswa kula mwanadamu na badala yake anaweka akiba sehemu ambayo hakupaswa kuwekwa akiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…