haya mambo wazungu walipitia mwaka 1600 to 1800 mwishoni huko ndio kulikuwa na unyonyaji wa design hizi huko ulaya maana hakukuwa na sera wala sheria za kuwalinda wafanyakazi.
ila cha ajabu sasa leo mwaka 2024 nchi yetu inasera, miongozo na sheria za kuwalinda wafanyakazi hawa lakini wamiliki wa hivyo viwanda bado wameachwa wafanye wanavyotaka mafano kima cha chini kwa sasa kwa siku kwenye viwanda kwa mijibu wa serikali ni tsh. 5,770 kwa siku. kwa wiki 34,618 na kwa mwezi 150,000= bado unajiuliza inakuwaje mhindi mmoja mjinga tu amelowea hapa nchini anawatumikisha ndugu zetu kwa ujira wa 3,500/= kwa siku na bado anakenuliwa meno na viongozi wetu.
je hawa viongozi wetu waliojaa kama utiriri kuanzia serikali za mitaa, kata, tarafa, wilaya, mkoa wanatusaliti au ni wamelogwa au ni nini!
pia hii sheria inatakiwa itamke wazi kabisa haya malipo ni kwa masaa mangapi maana ukisema kwa siku mwingine anawafanyisha watu kazi saa moja asubh hadi saa moja jioni nayo ni siku sheria zetu wenyewe zinatukandamiza haya ni maajabu kabisa.
hivi hakuna wanasheria wanaweza kujitolea kusimamia hivi vitu ili wananchi wanyonge wapate haki yao.