Yanayofanyika viwandani Tanzania ni utumwa. Kazi ngumu, maslahi duni. Serikali haina mpango na wananchi wake, inachoangalia ni kodi tu

Ndugu yangu,hivi msomi ni yupi?
Kuna sehemu niliajiriwa,ilikuwa ukiangalia vibarua wengi ni form four na six ambao hawana
wa kuwaendeleza wanasaka chapaa ili wajisomeshe na wengine hawakupata maksi nzuri
ili kuendelea,Sasa ukiangalia mshahara huo kama huna mtu anayekuhifadhi huwezi fanya lolote
utaendelea kuteseka hadi nguvu ziishe.
Cha kufanya,kama kwenu kuna shamba ni heri urudi ukalime,au basi jitahidi uwe machinga
 
Sad truth, maisha hayaangalii process,
Ni kweli wanatafuta hela ya kujisomesha, ila hapo wapo kama unskilled labor, na issue ya wao kutokwenda shule sio kesi ya mwenye kiwanda ni kesi yao wenyewe, hapo watalipwa pesa ya siku,

Kwenye maisha hulipwi ili kutimiza ndoto zako, unalipwa kwa kiasi cha value unayo add, mwajiri hakulipi ili uende shule, analipa kwa kile unampa kwenye biashara yake,

Huu ni ukweli mbaya, hausound vema ila ndivyo ilivyo
 
Umewahi kufanya kazi kwenye ofis mbalimbali?
 
Ulikuwa unashusha mizigo kwenye makontena?.
 
Kuna siku niliongelea humu swala la civil society (workers civil groups) umuhimu wake. Ila nikagundua Wafanyakazi wengi hawajui hili swala. Na sio kutokujua tu. Hata wale ambao wamejiunga huwa wanatumia vyama hivi kipindi cha shida tu tena kwa uchache. Acha watu waumie. Waendelee kugoma na vyama vya siasa wakati kuna vyama unaweza peleka tatizo elekezi kwao.
 
Hii ni Manamba
 
Halafu mchawi mwingine ni mtanzania mwenzako(supervisor). Muhindi anakupiga kwa kukulipa 5000 per day, halafu msimamizi wako nae anakupiga kwakukulipa 4000 au 4500 per day.Maisha ya viwandani ni magum sana hapa tz
 
Uko sahihi mkuu. Kuna wapakistan na wahindi pale Deira, Dubai wanaishi maisha ya hovyo sana na kupigishwa kazi balaa. Kuna mmoja ni fundi cherehani aliniambia nikiweza kumlipa mshahara kama laki 9 na kumtafutia work permit yupo tayari kuja na kupiga kazi kwenye ufundi cherehani kama nitafungua hiyo biashara. Kazi yake ni balaa na nusu. Ni kipaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…