Wapendwa Kwanza niwakumbushe hawa Waheshimiwa hawajawa Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba.
Kama sikosei watakuwa hivyo baada ya kula kiapo na hilo Bunge maalum kuanza kazi.
Hivi sasa nadhani ni wateuliwa wamo kwenye semina.
Kuna jina lilimpa shida sana Mwenyekiti wa muda kulitamka la mjumbe aliyejitambulisha kuwa ni mwalimu kwa taaluma.
Sasa ni Kila saa, utamsikia Mwenyekiti akimtaja "Mheshimiwa ALL WATCH", ni Kila saa !!
Huyu Mwalimu inaelekea amejipanga vizuri, hata wakati mwingine akisimama tu anaunga mkono ...Katibu wa Bunge maalum atakuwa na madaraka makubwa... kama mjumbe aliyetangulia alivyosema naunga mkono.
Haya mi sielewi labda huko mbele kuna fursa zitawajia za kuwa Wenyeviti wa Kamati kwa sasa wanakula mazoezi !!!