Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Sendeka ndo kuwa chanzo baada ya kumushambulia mbaruk personaly badala ya kamati. Mle wakuu ni cuf na ccm kwa mitizamo ya muungano. Ole sendeka hatumbua kuwa imvi ni busara sio kila kitu anataka aseme tena sio kwa staa. Anacheza na wazanzibar atachezea kichapo na utu uzima wake
 
Kwa kweli bunge hili ni kilabu cha komoni,mbege,mapuya na ulanzi.
 
Kwa hili kwa kweli tumechemsha lakini Mwenyekiti wa muda ameshindwa kusimamia shuguli za Bunge, maana nadhani anaposhindwa kufuata kanuni lazima haya yatokee. Kukiwa na haki amani lazima itatawala.
 
Kuahirishwa kwa bunge leo kabla ya muda ni matokeo ya wanasiasa ambao ni wabunge kujali masilahi ya vyama vyao badala ya masilahi ya taifa, ilipaswa wajumbe hawa wakitoka kupitisha katiba wasigombee vyeo vya kisiasa kwa maana ya wabunge, madiwani na wawakilishi, kumbukeni pesa inayolipwa ni kodi za walala hoi wa nchi hii. Wananchi tusikubali nitakua wa kwanza kuandamana kwa matumizi mabaya ya pesa yetu. Baada ya mjadala wa rasimu itungwe sheria kuzuia walioshiriki kupitisha rasimu ya katiba wasigombee nafasi za kisiasa
 
Jana bunge liliahirishwa kwakuwa wabunge walidai wamechelewa kupewa nakala ya sheria namba 32 hadi 43. Leo bunge limeahirishwa kwa sababu secretariet imetoa majedwali mawili ambapo jedwali moja halionyeshi majina ya akina Mwalimu na Sendeka.

Kwa vyovyote vile wazembe wanajulikana na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa dhidi yao.

Kama mwendo huu utaendelea kila siku bunge litakuwa linaahirishwa huku posho zetu waamka taabani zikiendelea kuliwa.

Ushauri wa bure kwa kamati ya kanuni, waandae sheria ya mpito kwamba hapo bungeni yeyote atakaeonekana kuanzisha vurugu asilipwe posho. Na kwa njaa walizonazo hao watu utaona kama watafanya tena fujo.

Kuna tabia nyingine imezuka ya watu kupiga tu kelele za kuzomea hata kama jambo linaweza kuzungumzika na majadiliano yakaendelea. Hili mimi naona linasababishwa na baadhi ya wabunge wanaotaka bunge kiahirishwe ili wakafanye starehe zao. Dawa ya hawa watu ni kuwawekea monitor atakaeandika majina ya wapiga kelele ili yanapotokea mazingira ya hivyo, majina yanasomwa then kama kawaida wanakatwa posho.

Haya yasipofanyika, hakuna rasimu wala katiba mpya hapo mjengoni. Tutarudi mwaka 77 kuendelea na zilipendwa. Kikwete alisema 'mkileta utoto hatutapata katiba mpya. Na kwa vile nchi haiwezi kuendeshwa bila katiba tutarudi kwenye katiba ya zamani'
 
Safi abubakar mbane werema mpaka akose pumzi walizoea kupindisha kanuni na kuvunja katiba
 

Ni kweli Olesendeka, huwa hanaga hoja zaidi ya kutetea ccm hata kama ni jambo la kijinga... Mmoja wa wabunge wanaopayuka bila kuwa na pont. SIJUI HUWA NAMUONAJE.
 

we mnduku una kushawa nini ole sendeka ni chadema?? Mbona unaiandama chadema hata kwa mambo ambayo haihusiki?? Unagenye wewe una tafuta bwana wa kuk rafi.
 
na hii kanuni ya 57 Mwakyembe angeonyesha ni national security ipi ambayo inaweza kuwa violated, kwa waandishi wa habari kuingia kwenye kamati na kutoa balanced news? ili tuweze kujiridhisha.
 
Duuh. binadamu n mbwa! unatofauti gani na hao unaowaita mbwa?
Kwa tabia hii hata wewe ungekuwa mjengoni ungekuwa kituko

Ningekuwa bungeni huyo mmasai wenu mpenda sifa siku nyingi tu angeshachezea vitasa na semina ingeendelea tu jinga kabisa Ole Sendeka.
 
Pale wamefata Posho tu hakuna la zaidi...
 
Mjumbe akataa kuombwa radhi, asema yeye anajuwa kanuni zaidi ya miaka 30 na afikirii mtu atoke Simanjiro miaka kumi iliyopita halafu ajifanye eti anajua kuliko watu wengine. Kikao kimeghailishwa mpaka saa kumi jioni huku sintofahamu ikiendelea....

Kuna haja ya kuachana na swala la katiba mpya kama hali itaendelea kuwa hivi.
 
rekebisha hapo kwenye red, sio hili tu bali Watanzania sote ndivyo tulivyo. Mlidharau sana cdm walivyotoka nje lakini taratibu tunaweza kuanza kuwaelewa sasa, tulidhani Mh. Joseph Mbilinyi ni mhuni kwa kudhalilidhwa na wanausalama wa Bunge lakini sasa tunaweza kuwaona wahuni ni kina nani. Mchakato ulianza japo sio vizuri lakini mara viongozi wakuu wanaanza mipashoa ya misimamo badala ya maoni hapo ulitegemea nini!?
Watanzania tuna matatizo na hasa kwenye kupanga na kuamua na ndio maana wenzetu kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki - EAC wametuchoka, sidhani kama wanajisikia vizuri kututenga lakini hawana jinsi. Hatuvumiliki!
 
Nikionacho ni fedhea tupu kama si aibu,.ila ngoja tuone japo ninamashaka sana na hili bunge la katiba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…