Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Yanayojiri Bunge la Katiba Dodoma leo 06/03/2014

Dua?Serikali na organs zake ni secular

Mambo ya dua yametoka wapi?
 
huu jamaaa. yupo vizuri sana. na naona prof mahalu anamtumia sana kutoa fafanuzi mbalimbali kwenye majadiliano ya kupitisha kanuni.
 
Baadhi ya wachangiaji wametaka kabla ya bunge hilo kuanza na kumaliza basi iwe kwa dua ili wale wenye mashetani akina Olesendeka mashetani hayo yaweze kuondoka vichwani mwao., waislam wakiristo wataomba kwa dini zao. TBc Live


...hilo bunge litakosaje mapepo/mashetani wakati humo ndani kuna hadi mwakilishi wa wachawi!?...
 
Ole Sendeka atandikwe mangumi hata nje ya bunge ili awe na adabu.
Halfu huwa nashangaa sana anavyotikisa ------..na kihere here kujipitisha mbele za watu.Niliwahi muona simanjiro, Clock tower Arush na mlimani City dar...huyu jamaa ana kiherehere sana..km mtoto au chakula fulani
 
Leo mtoto hatumwi dukani.Leo, asiye na mwana aeleke jiwe.Leo,ukigeuka nyuma unakuwa jiwe la chumvi.Leo,macho mbele kama tochi. Leo,masikio na macho ni marafiki muhimu. Leo, kila kitu kina watu;wale wastaarabu na fyatu.Usisubiri kusimuliwa.Jionee au sikiliza mwenyewe leo.

Kwa nyaraka zilizopo,shughuli hiyo itakuwa jioni.Leo,Bunge la Katiba linafikia vifungu vya 37,38 na 39 vya Rasimu ya Kanuni za Bunge hilo ili kuvipitisha.Vifungu tajwa,pamoja na mambo mengine, vinazungumzia namna ya upigaji kura wa kupitisha Rasimu ya Katiba utakavyokuwa ndani ya Bunge hilo.Wapo wa KURA YA SIRI na KURA YA WAZI/DHAHIRI. Leo watajulikana vyema.

Lazima leo Bunge liamue kupitisha au kuviondosha vipengele hivyo vya Kanuni. Ni leo.Si kesho. Lakini, kupitisha SIRI au DHAHIRI kutafanywa kwa SIRI au DHAHIRI? Mwenyekiti wa muda ataongozwa na Kanuni au Taratibu zipi leo kuamua kuendesha kura za SIRI au DHAHIRI wakati itakapojitokeza haja ya kufanya hivyo? Leo kitaeleweka tu.Zege halilali!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (sasa Dodoma)

--------------


kweli anayejua anajua tu
 
Kodi za walalahoi zinateketea, mtu anajikunja kwenye foleni kuwapa posho wapiga kelele na kusahau tulichowatuma
 
Nakiri kutowasikiliza wachangiaji wote; lakini kwa niliowasikiliza; nahitimisha bila shaka: wawakilishi kutoka Znz wanajenga hoja kuliko wale wa bara na wako fair zaidi kwenye itikadi.
Mifano ipo mingi; lakini chukulia Pro kama Simbachawene, wazir, anajenga hoja kua waandishi wakiruhusiwa watatoa habari nusu-nusu (kana kwamba waandishi hao hawajawahi ripoti vikao vingine vya bunge-kama hivi vinavyoendelea); huku aki-pause ili awe echoed na na vile vigelkegele vya 'Viti maalumu'. Kiufupi wabara wengi wanaongea kwa emotion wakichagizwa na platform. Wakati huohuo pro mwenzake kutoka Znz; waziri wa sheria; kinagaubaga anamwambia mwenyekit, mzanzibar mwenza na spika wake kua aache kuvunja kanuni!
Lakini ikionesha wabara wameathiriwa zaidi na itikadi; Sendeka anamlipukia kua katumwa na chama! Kana kwamba hakuna hoja ya msingi!
Spika Kificho amewakilisha vema ma_pro kutoka Zenj. Baadhi wanasema anapwaya; lakini ni kwasababu tu baadhi yetu tumezoea siasa za maspika wa JMT za 'ku-deal' na ma-opposers. Tatizo ni nidham ya wajumbe.
No wonder mzee amekua spika kwa miaka 18 katika bunge lenye 50_50 competition. Huhitaji kujifunza ku-deal na wajumbe. Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwa wazenj!
Kwa hoja zenu, mtapata maslahi yenu; Karibuni Tanganyika
 
Uko sahihi kwa alichokifanya Ole Sendeka hakikupaswa kufanyika, na ametia aibu wabara wote. nadhani angesema vile wa CDM wangesema ni watu wa fujo. Hivi wakiahirisha kikao wanalipwa posho nusu? maana wanaahirisha ahirisha tu.
 
Uko sahihi kwa alichokifanya Ole Sendeka hakikupaswa kufanyika, na ametia aibu wabara wote. nadhani angesema vile wa CDM wangesema ni watu wa fujo. Hivi wakiahirisha kikao wanalipwa posho nusu? maana wanaahirisha ahirisha tu.

Mkuu sie tunategemea zaidi makofi kupitisha vifungu, hata kama vinapingana na katiba.
Mwanasheria mkuu wa Znz alisema mkata wa Muungano ni wa wananchi; hivyo mwananchi yeyote anaweza uona. Hiyo ni baada ya wabara kama kawaida yao kusema "mkataba ni nyeti"! Jamaa wako sana mbele ki demokrasia.
Angekua cDm ndio ingetumika nguvu kubwa, pasipo hoja kukuza itikadi bungeni
 
Pale aliposema kuusu kanuni ya mjumbe atakapofariki gharama anabeba nani..?
Kumbe kuna kanuni inasema kabisa kua bunge ndo litabeba gharama zote
Tundu lisu akamuumbua akasema mh mwenyekiti tumebewa vitabu ivi ili tuvisome na akamsomea sheria inasema vipi kuusu ilo swala
 
Nakubaliana nawe kwamba katika muda mfupi niliangalia Bunge jana AG wa Zanzibar,Jussa,Waziri wa Sheria wa Zanzibar,Lissu na Prof. Mahalu walinifurahisha.

Ni jukumu la Wabunge wetu wa Tanganyika ns.hasa hawa wasomi kujifunza toka kwa wenzao wa Zanzinbar. Watambue wamepewa fursa muhimu kuandika Katiba yetu lakini fursa binafsi kukumbukwa ktk historia ya taifa letu. Kama wataendelea kupiga kelele na kutetea vitu ambavyo ndani ya roho zao wanajua ni uwongo historia itawahukumu kama makuadi!
 
Unamshangaa wa nn wakat wajua ni mzigo ulioshushwa kwny baraza arumeru magharibi wameupewa wakaufukie?
 
Back
Top Bottom