Mtikila ni mtu anayeweza kujieleza vizuri sana lakini anapokwenda nje anakuwa hatari. Binafsi nampenda kwa kusimamia Tanganyika kwa miaka yote bila kugeuka.
Lakini ndani ya CCM kuna wazembe wa kutisha kuliko hata Mtikila. Hawana mchango wowote!
thatha, hii thread unaiharibu...hivi hujaona ajabu mnaochangia ni ninyi hao hao? Sifa kuu ya Mwenyekiti wa kikao muhimu kama hiki ni kutoshabikia upande wowote mapema kama alivyofanya Sitta. Kwa kauli yake hiyo kaonesha hicho kiti kinamzidi kimo na angekuwa na hata chembe cha busara angefuta hiyo kauli na kuwaomba wajumbe msamaha. Lakini ndiyo hivyo tena huo ndio msimamo, kama tunavyoambiwa, wa chama tawala na hivyo tusitegemee mjadala unaotanguliza maslahi ya Watanzania bali ya wana CCM. Of course Sitta ana nafasi nzuri tu ya kuchaguliwa na hiyo ni kwa sababu wajumbe wengi wako mle ndani kuwakilisha matumbo yao na ya waliowateua. Sitta ni moja kati yao watu hao na kwa hakika huu ni muendelezo tu wa kundi la kisanii ndani ya chombo chetu hiki ambacho kwa bahati mbaya maamuzi yake yataacha madhara makubwa kwa taifa letu huko mbeleni, yangu macho.
Unatoa msimamo katika wakati muafaka na eneo husika (at a right time and space) pale unaomba kuwa judge wa watu wenye hisia na mawazo tofauti, katika hatua za mwanzo tu unaonyesha uko upande wa X na wale wa upande Y si wako!
sijaona tatizo lolote mkuu'kasema hatapenda kuona muungano ukivunjika'Muungano waweza kuwa wa serikali 2 ama serikali 3,means serikali ya Tanganyika,ya Zanzibar na ya Muungano