Baada ya habari za kutoka nje kwa UKAWA huko DODOMA kuanza kuenea kama moto wa Nyasi kavu huko Zanzibar ,wananchi wameanza kuandaa mapokezi ya ari na nguvu ikiwa UKAWA hawatorudi tena bungeni ,aidha habari zilizozagaa ni kuwa wabunge hao watasubiriwa kwa hamu na kupokewa kwa maandamano ambayo wanasema hayajawahi kutokea Zanzibar ,hizo ndio habari za matayarisho punde tu ikijulikana wanarejea visiwani humo wakiwa wameonyesha ari na nia zao za kuitetea Zanzibar bila ya kumuonea haya mtu au kumuogopa mtu.Maneno na maandishi ni Zanzibar kwanza Tanzania baadae.
Je WaTanganyika watabaki wameshika tama na kusubiria wanayoyataka vigogo wa CCM ? Zanzibar kwanza.