Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Yanayojiri Bungeni Dodoma: Jumatano, Trh 16 Aprili 2014 - Majadiliano ya bunge zima sura ya 1 & 6

Maskini! mpaka nawaonea huruma wajumbe wanaotetea serkali mbili. Niwepesi mno kwa hoja! Wananyanyaswa na wenzao wa serkali tatu kwa hoja nzito na rejeo (references) zilizoshiba!
Bi Asha Bakari Mtama, yeye akaishia kumjadili Ismail Jussa, na vitisho vya mapinduzi...maskini! Watu wanajadili serkali tatu, yeye anawaambia CUF hamuipati serkali SMZ tumepindua! Kumbe hofu ya CCM wa Zanzibar ni zikija serkali tatu wanaona CUF watachukuwa serkali?! Geni hili kwangu mie!
Ushauri: Maalim Seif waahidi hao CCM wa Zanzibar kwamba, kama wakikubali muungano wamkataba au japo serkali 3, wewe na CUF yako hamugombei tena Zanzibar....Hahaha! Angalau nasie tunonoooke...huu muungano untunamia vibaya
naona mitandaoni suala la katiba mnafanya vizuri nyie wala viroba ila nina uhakika yatawapata ya kalenga na chalinze.
 
naona mitandaoni suala la katiba mnafanya vizuri nyie wala viroba ila nina uhakika yatawapata ya kalenga na chalinze.

Inawezekana via vyako vya uzazi vinaendana na jina lako kabisa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nigewaamini wajumbe wa ccm zanzibar kama wangekuja na hoja ya serikali 1 ningeamini kama kweli wanapenda muungano wa kweli na wenye usalama wa aina zote.Na hata ile khofu waliyo nayo ya kurudi kwa ukoloni wa sultani ingepotea.
 
Ccm hawana hoja zaidi kuokoteza vihoja mbalimbali, eti wanamuenzi mwl. Nyerere. Nawaonea zaidi huruma maccm ya zanzibar jinsi yalivyotekwa na watanganyika wanaoitawala zanzibar! Tanganyika haiko tayari kuvua koti lake la muungano!
 
Wazanzibar (CCM) wamezoea kula urojo kwao sasa wamefika Dodoma wamakutana na misosi ya nguvu imewabadili akili!!
 
Wanabodi, leo nikaona ngoja nicheki maoni mbalimbali mitandaoni kwa upamde wa Zanzibar! Bila hiyana nikaingia: Mzalendo.net( Mzalendo net Zanzibar) kuna mijadala mingi tu kuhusu yanayoendelea kule Mjengoni-Dodoma. Mada mbili zenye vichwa vya habari zilinivutia
1. Muundo wa Serilali2 ni Butu
2. Maswala kwa Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba juu ya Serikali2
3. Zilizoungana ni Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na kuitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wala siyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Hivyo wadau, siyo mbaya mukapitia mara moja moja kuona mijadala yao! Ijapokuwa nilivyoangalia, muundo wake haufanani na JF.
 
naona mitandaoni suala la katiba mnafanya vizuri nyie wala viroba ila nina uhakika yatawapata ya kalenga na chalinze.

Wajua unachokiongea sicho unachofikiria.Hivi kwa namna hali ya hewa Zanzibar ilivyo kunahitaji kumtuma Malaika akakague?Hivi Watanzania bara waishio Zanzibar baada ya hili Bunge linaloonyesha Ze Comedy likiisha mustakabali wataifa umefikiwa.

Ni muumini wa Serikali mbili na niko tayari kuipigia kura hata ya wazi lakini ni baada ya kuwekewa sawa masharti ya UHAI wa mdanganyika aishie Zanzibar.

Masharti hayo ni MARITHIANO ya pande zote mbili na hasa Zanzibar tukubaliane namna ya kuendesha Muungano huu,vinginevyo tunajidanganya,haitachukua miaka mingine 50 bila kuvunjia,na utavunjika vibaya kuliko sasa.
 
Mpaka sasa, hoja ya serikali1 ndio bora zaidi inayofuata ni Serikali2 hii ya Serikari3 ni kelele tu, hakuna hata mmoja aliyetoa point inayoshawishi hadi hivi sasa sana sana wengi wanashabikia kwa vile ni sera ya vyama vyao.
 
Mi kwa mtazmo wangu, muungwana hupinga hoja kwa hoja na si hoja kwa kashifa au tusi. Tuwaacheni waendelee kutafuta katiba mpya na baada watatuletea rasimu ya pili ya katiba.
 
Kama Serikali moja haiwezekani, basi huo muungano ufe tu. Hizi gilini macho ndiyo zinakuza hizi chokochoko zinazoendelea.
 
Muungano unaweza kuvunjika hata tukiwa na serekali 2
 
Ni msimano wa chama chao wa serikali mbili ndio uliowafunga!! wanatia huruma maana hoja zao ni nyepesi mno. As we move on Tume ya Mh. Warioba inazidi kupata points.
 
Mpaka sasa, hoja ya serikali1 ndio bora zaidi inayofuata ni Serikali2 hii ya Serikari3 ni kelele tu, hakuna hata mmoja aliyetoa point inayoshawishi hadi hivi sasa sana sana wengi wanashabikia kwa vile ni sera ya vyama vyao.
serikali 2 ni kuendeleza ukoloni wa tanganyika dhidi ya zanzibar! Ni heri kugawana mbao kuliko kuendelea kutawala kisiwa cha zanzibar!
 
Back
Top Bottom