miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,811
- 49,053
yani wewe akili yako bwana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwenyekiti amelazimika kusitisha shughuli za bunge leo jioni baada ya wabunge kukataa kusikiliza hotuba ya mwenyekiti wa tume ya Katiba. hii inaonesha pia Warioba ameamua kugoma kusoma kwani wazo la Sita lilikua isomwe tu.
Inadaiwa kuwa wabunge hawa wanataka protocol izingatiwe na Rais alifungue bunge kwanza na si vinginevyo hofu bila shaka ikiwa ni umuhimu wa hotuba ya Warioba utatiwa kampuni ikianza.
Yetu macho. tunaendelea kuona sura ya ule muhafaka unaotarajiwa na una sura inapambwa na matukio kama haya!
Bunge limehairishwa kwa muda.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati m/kiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Warioba akianza kusoma hotuba yake,wabunge kadhaa walianza kugonga meza na kuzomea bila kikomo.hali hiyo imemfanya m/kiti wa bunge mh. Sitta kusitisha shughuli za bunge hadi itakapotangazwa tena.
Ni kweli bunge limeahirishwa mpaka watakapotangaziwa baada ya jaji Warioba kukaribishwa kuwasilisha rasimu ya katiba lakini wabunge walikuwa wanagonga meza zao kuashiria kutoafiki kuwasilishwa huko, pia nimewasikia wengine wakisema kanuni zifuatwe.
Mkuu, na kwa nini Rais ahutubie kabla wabunge hawajakabidhiwa rasmi Rasimu ya Kanuni? Hapo umenikumbusha hadithi ya nini kimeanza kati ya kuku na yaiKwanini Warioba ahutubie kabla ya Bunge kuzinduliwa na Rais? Alafu kazi yote ile ya tume alafu wanapewa masaa mawili tu?
Kwa jinsi Mtiririko wa Matukio ulivyo,Najuta kwa nini nilizaliwa nikajikuta napenda kufatilia masuala ya Siasa,Bora ningekua Mfatiliaji hata wa Mieleka Nikaepukana na Pressure hizi,Maana napoona Watu wachache wanajaribu kupindisha Maoni ya Walio Wengi kwa Maslahi yao Binafsi, Moyo Wangu unajaa Mithili ya Kuripuka,Eee Mungu nisaidie.
Mkuu, na kwa nini Rais ahutubie kabla wabunge hawajakabidhiwa rasmi Rasimu ya Kanuni? Hapo umenikumbusha hadithi ya nini kimeanza kati ya kuku na yai
Mkuu, na kwa nini Rais ahutubie kabla wabunge hawajakabidhiwa rasmi Rasimu ya Kanuni? Hapo umenikumbusha hadithi ya nini kimeanza kati ya kuku na yai
wajumbe poleni na majukumu
pamoja na kelele za wadau mbalimbali waliolalamika kuhusiana na mchakato wa katiba mpya kutokupitia hatua muhimu, sheria ya mabadiliko ya katiba ilipelekea baraza maalumu la katibu kuundwa kwa ajili ya kujadili vipengele mbalimbali vilivyoainishwa katika rasimu ya pili ya katiba ya jmt.
Hadi kufikia leo hii, tumeona rafu mbalimbali zinazochezwa na baadhi ya wadau. Uzi huu utahusisha rafu za aina zote; ziwe za kikanuni, kisheria au kimazoea na namna ambavyo ilitakiwa ifanyike kwa malengo ya kuwajuza wawakilishi hao juu ya namna wanavyopaswa kuenenda katika shughuli za bunge kwa malengo ya kupata katiba iliyo bora
kwa mfano: Kufuatia mwenyekiti wa kudumu wa bmk kutoa mwongozo wa kazi kwa juma hili., kuna rafu tayari imechezwa juu ya taratibu
aina ya rafu: rais kutoa hotuba yake katika bmk baada ya mwenyekiti wa tume ya marekebisho ya katiba kuwasilisha rasimu ya pili bungeni.
usahihi: mwenyekiti wa tume ya marekebisho ya katiba alitakiwa kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba ya jmt baada ya raisi wa jmt kutoa hotuba yake
nina uhakika kabisa kwamba matokeo juu ya muelekeo wa hatua za awali za kuanza kazi hii kwa kuzingatia scenerio hizi mbili za nani aanze kabla ya mwenzake yatakuwa na tofauti kubwa sana kwa kuwa kila atakayekuwa anamalizia atakuwa na nguvu ya kushawishi wajumbe juu ya ya masuala yatakayokuwa yameongelewa na ama mwenyekiti wa tume ya mbadiliko ya katiba au rais wa jmt.
Haikazwi pia kurejea rafu zilizochezwa so far kama ushaziona au kusikia au toka katia source yoyote.
Nb: Rafu ninazozungumzia ni kutoka makundi yote ya wajumbe wa bunge maalumu la katiba
karibuni
Yani leo jioni unaweza kuwa mwanzo wa mpasuko wa taifa endapo wajumbe wasipokua makini
Kwa nini mkuu