Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

Acha propaganda na uongo wa mchana kweupe. Eti upinzani walishindwa uchaguzi wa 2015 kwasababu hawana media?! Nawashangaa sana hao wanaokulaga matango pori yako.
Pascal amejishushia heshima sana hapa jukwaani, hata angeandika kurasa elfu kumi kujikosha lakini haitasaidia, kwani sasa hivi ukiona bandiko lake hata kabla ya kulisoma unajua tu litahusu kuipiga madongo Chadema, kuhalalisha (kimtazamo) maovu ya utawala wa CCM mpya, kifupi ni mnazi kama wale Lumumba BK7. Inasikitisha sana, mtu aliyekuwa kioo cha jamii hapa jukwaani kugeuka kuwa muimba mapambio.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Namuomba Mungu aniepushe na Pasco wakati huu kipindi hiki ambacho nywila yake ya JF imeingia mikononi mwa hackers baada ya kuibiwa akiwa ulevini.
Pascal sio wa kuandika hivi unless madhara kichwani ya ile ajali ya pikipiki yawe yanatokea sasa hivi.
Tutabishana naye kwa hoja atakaporudisha nywila yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtupe na gharama mlizokodia ukumbi! Maana tuasikia ukumbi umekodiwa kwa 230ml. Nje ya gharama za kupamba.
Je nikweli? Kama siyo mtupe majibu.
 
Maana tuasikia ukumbi umekodiwa kwa 230ml. Nje ya gharama za kupamba.
Je nikweli?
Mambo mengine ya kijinga sana. Yaani wakati ule wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA walikodi huo ukumbi kwa siku 11 kwa shilingi milioni 110 leo kwa siku moja wanakodije kwa shilingi milioni 230!!?

Hivi nyie watu ni nani aliyewaloga hadi kuamini kila mnachoambiwa na CCM?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…