Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

Ni Jumapili tulivu ambayo ni siku ya Wanawake duniani.Katika Taifa letu Wanawake wa Chadema wanafanya Kongamano lao kubwa katika Ukumbi wa Mlimani City DSM.

Idadi kubwa ya wawakilishi wa Wanawake wa Chadema kutoka mikoa yote tayari wako DSM kuhudhuria Kongamano hili.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hili anatarajiwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Aikael Mbowe.

Sisi wa Molemo Media tutakuwa hapa kuwahabarisha watanzania na dunia kwa Ujumla yale yote yatakayojiri hususan hotuba ya Freeman Mbowe kwa wanawake na Taifa kwa ujumla.

Karibuni sana.

---------------------------------------------------

Ukumbi wa Mlimani City linakofanyika Kongamano hili kumepambwa vema huku akina mama wakiwa wanawasili kwa wingi maeneo haya wakiwa na sare maalum za chama kikuu cha upinzani nchini Chadema.

Ni furaha sana na shangwe kuu zimetanda hapa.Wengi wakijaribu kudadisi yatakayotokea hapa ikiwemo Hotuba inayosubiriwa kwa hamu ya mwanasiasa maarufu zaidi Afrika Mashariki Freeman Mbowe.ikumbukwe Mbowe aralihutubia Taifa kupitia Kongamano hili ikiwa ni siku moja kabla ya hukumu ya kesi ya kisiasa dhidi ya wanasiasa wakuu wa upinzani nchini.Wananchi wengi wakidhani hukumu hii huenda ikawa ndiyo kipimo cha imani ya wananchi dhidi ya mahakama hususan tuhuma za kuingiliwa na serikali.

Updates at 12.20pm

Sasa ndiyo viongozi wakuu wanaingia hapa Ukumbini.Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe na Katibu Mkuu John Mnyika wakisindikizwa na Mwenyekiti wa Bawacha Halima Mdee na viongozi wote wa Bawacha anapokelewa kwa shangwe kuu hoi hoi na nderemo.Wanawake wanampokea kiongozi wao kwa nyimbo za hamasa za kimapinduzi.

Kati ya watu mashuhuri waliohudhuria kongamano hili ni mwanaharakati maarufu Maria Sarungi Tsehai na Shangazi Fatma Karume mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume.Pia yumo Dr Azavel Lwaitama.

Limefuatia tukio la kuombea kongamano hili kutoka wawakilishi wa dini ya Kiislamu na Kikristo.Na baada ya hapo Katibu wa uenezi wa Bawacha Agnesta Lambert anatoa utambulisho kutoka mkoa kwa mkoa.

Baada ya hapo anakaribishwa Katibu Mkuu Bawacha Grace Tendega ambaye anatoa salaam za Baraza kisha anawaita wageni mbalimbali kutoka vyama vya siasa kuja kutoa salaam
kiongozi wa ‘malaika’ atakufa kwa roho mbaya
 
Hivi hiki chama hakifi tu?😀
 
Mkuu Molemo, kwanza asante kutuhabarisha and it's good to learn kuhusu Molemo Media, natumaini utatuletea live kupitia live streaming, naona kama umebeba mikoba ya Tumaini Makene, maana simsikii au na yeye ameisha jitambua?.

Hiki unachofanya sasa ndicho tulichowashauri mfanye toka ile 2015, mu invest into mass mobilization strategies za reaching out to reach the masses, mlipaswa muwe na redio yenu, TV yenu na interactive online media ya chama kabisa na sio kutegemea individual efforts.

Jamaa yangu alipokuja ile 2015 nilikuwa na matumaini makubwa
Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Hata hivyo asante kutuhabarisha.
P
Umeona hiyo nyomi ya kina mama? Aisee watu mna roho ngumu! Dah!🤦🏾‍♂️

Ujuwe mkitumia dola mtawauwa wengi.
 
Kwenye hoja hii
Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Sikumzungumzia kisiasa, nilizungumzia matumizi ya ukwasi wake to Chadema advantage, very unfortunately it didn't work out.

2015 ilikuwa Chadema ichukue nchi, ikakwamishwa na kitu kimoja tuu kidogo, reaching out mechanisms to the grassroots movement kutokana na Chadema kutokuwa na media zake. Sasa ni 2020, uchaguzi mwingine ndio huo just around the corner, matukio ya mass mobilization ndio haya, na media yenyewe ndio hawa kina Molemo wanafanya kusaidia tuu, unategemea nini?!.
P
Acha propaganda na uongo wa mchana kweupe. Eti upinzani walishindwa uchaguzi wa 2015 kwasababu hawana media?! Nawashangaa sana hao wanaokulaga matango pori yako.
 
Lengo la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Ndani ya Chadema kuna makundi mawili, wako wanaojitambua, na wasio jitambua. Wanaojitambua wakiisha gundua Chadema ipo ipo tuu na haina mpango wowote wala uwezo wa kushika dola, wanajiongeza na kutimka zao kujiunga na chama dola. Wasio jitambua wanaendelea kuishi kwa matumaini ila baada tuu ya Bunge kuvunjwa, kutatokea mass exodus, waliobakia ni wale wagumu kama wewe ambao mnajitambua na mnajua kabisa kuwa Chadema hivi ilivyo, kamee haiwezi kuja kushika dola, ila mnaendelea kuwepo kuonyeshea msimamo usio yumba, baada ya 2020, mnakwenda nayo chini!.
P
Wewe umedharauliwa hadi na vichaa , endelea kujidhalilisha zaidi lakini iko siku utakimbia jf kwa hiyari yako , Mungu hadhihakiwi , endeleeni na ukabila lakini mwisho wenu hauko mbali .

" AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU " Endelea kumuabudu Magufuli ukidhani udikteta wake utakunufaisha
 
Kwani Mbowe siyo mungu wa Ufipa?!!
 
Mshana Jr: nakuheshimu sana, huyo mnyama umemuingizaje hapa? Leo ni siku maalumu ya wanajangwani kushereheshe huu mkutano wa Bawacha, kwa kuifunga hii timu isio na uwanja magori 3-0.
Safi kabisa tuwaombee sana... Na tusisahau pia leo ni siku ya ushindi wa kihistoria wa mnyama...

Jr[emoji769]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom