Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

Umeona hiyo nyomi ya kina mama? Aisee watu mna roho ngumu! Dah!🤦🏾‍♂️

Ujuwe mkitumia dola mtawauwa wengi.
Jmoshi tupeni link basi na sisi huku Nyansa tushuhudie japo hata ka clip kidogo.
 
May God vest his merciful victorious power upon you, so that you will continue healing the nation and always be the peoples' choice.

You should never betray the people as your opponent does, so that you continue winning his merciful love from the wailling people in agony from the teasing opponent in the wilderness.

I believe the people are with you, may God grant my wish upon you.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
May God vest his merciful victorious power upon you, so that you will continue healing the nation and always as the peoples' choice.

You should never betray the the people as your opponent does, so that you continue winning his merciful love from the wailling people in agony from the teasing opponent in the wilderness.
I believe the people are with you, may God grant my wish upon you

Sent using Jamii Forums mobile app
Let us all say Amen!
 
Mkuu Ukuta wa Saka, kwanza naheshimu mawazo yako kuhusu shallow analysis ya ujio wa Lowassa Chadema. Mtu asiye na shukrani kwa madogo, hawezi kubarikiwa makubwa. Nimeuliza bila Lowassa, Chadema ingepata kura zaidi ya milioni 6!. Unajua Chadema imepata wabunge wangapi kwa ujio wa Lowassa?. Unajua hao wabunge wanaingiza ruzuku kiasi gani Chadema?.

Politics is a science and a game yenye malengo. Japo Lowassa aliingia Chadema kuitafuta fursa ya kuingia Ikulu, baada ya kukosekana, it was his right kurejea, ila alipokuja, hakuja mikono mitupu, he brought something, Chadema aliyoikuta sio Chadema aliyoiacha!. Mimi nimehudhuria mkutano Mkuu wa Chadema enzi hizo unafanyikia ukumbi wa Kiramuu, hadi sasa Chadema wanakodi ukumbi Mlimani City!. Nyinyi manazi wa Chadema ndio hamna shukrani na Lowassa lakini Mbowe anamheshimu na anamshukuru mpaka kesho!.
P

Paskali najua unamsifia Lowassa kwakuwa ulikuwa na huenda una maslahi yako binafsi kwake. Sina tatizo na huo mtazamo wako lakini acha nijibu huu upotoshaji wako hapa chini kama ifuatavyo.

Mara baada ya uchaguzi wa 2010-2015 cdm ndio chama cha siasa kilichofanya kazi ya kisiasa kuliko chama chochote hapa nchini. Ndio chama kilichozunguka na kufanya mikutano mingi kuliko chama chochote na kuleta hamasa kubwa nchi hii ya kisiasa. Operation mbalimbali ziliendeshwa na cdm kutoa elimu ya uraia na kuwa tayari kwa mabadiliko ya njia ya kura hiyo 2015. Wakati huo Lowassa alikuwa anazunguka kwenye nyumba za ibada akifanya ushawishi wa hela, ili kusaka madaraka na sio kupitia ushawishi wa kisiasa.

Wakati wa kujiandikisha kwa kura uchaguzi wa 2015 tuliona watu wengi walijiandikisha kwa sababu walitaka kuichagua cdm, na wote tulijua Dr. Slaa angekuwa mgombea wa cdm na kweli alistahili. Wengi wetu tulijua Lowassa atakuwa mgombea wa ccm, hivyo tulijiandikisha kwa hasira tukijua Lowassa atakuwa mgombea wa ccm. Hapo ndio kadi za kupigia kura ziliitwa kichinjio ili kumchinja Lowassa kwenye box la kura. Hata Magufuli kupata nafasi ya kugombea kupitia ccm ni ile hofu ya kuwa Membe au hasa Lowassa wasingemuweza Dr. Slaa, hivyo mgombea wangalau aliyewafaa wanaccm ni Magufuli japo kwa ndani hawakuwa wanamtaka.

Ccm wakamkata Lowassa, naye Lowassa akawa hana jinsi zaidi ya kutumia pesa zake kwenda sehemu ambayo ingemuwezesha kutimiza ndoto yake. Hapo ndio Mbowe na viongozi wenzake wakafanya jambo lilliloigharimu cdm kwa kupokea vipande 30 vya fedha toka kwa Lowassa. Mbowe akabadili gia angani, as a result tukampoteza mgombea wetu halisi wa nafasi ile Dr. Slaa.

Kwakuwa cdm ilikuwa inakubalika watu wakamshangilia bila kuhoji, lakini Lowassa alikuwa kama dereva aliyerukia kwenye usukani huku gari likiwa linashuka mlima, lakini hakustahili kugombea urais kupitia cdm. Cdm ikapata kura 6+ zilizotangazwa na tume ya uchaguzi. Lakini hazikuwa kwa uwezo wa Lowassa bali ni matokeo ya ile mkakati wa 2010-2015 wa chama kushawishi watu. Kumbuka wakati wa kampeni Lowassa alikuwa mgonjwa na hakuweza kuhutubia hata dakika 5. Kama kuhutubia dakika 5, tena ukiwa na miezi miwili ndani ya chama kabla ya uchaguzi kunaweza kukupa kura 6m, ukiwa na miaka mitano na kuhutubia zaidi ya lisaa si utapata kura 60m? Mbowe ni lazima amshukuru Lowassa kwani yeye na kundi lake walifaidika mno na pesa zake.

Hitimisho, Paskali sisi ni watu wazima na tuna akili zetu, kama kweli Lowassa aliweza kuleta kura 6m na wabunge kibao akiwa na miezi miwili tu, hebu tuambie alileta wabunge na madiwani wangapi ndani ya miaka yake 2+ akiwa cdm? Naweza kukupitia kesho ulipo unionyeshe hapa Dar au popote hapa nchini ambapo Lowassasa alifungua hata matawi matano tu ya chama? Angejenga hata ofisi ya hadhi ya cdm ningekuelewa. Hayo niliyokuambia ni ukweli usioacha shaka, kwa hiyo potosha, sifia au fanya ufanyalo Lowassa hakuwa na faida yoyote cdm zaidi ya baadhi ya kikundi cha watu ndani ya cdm.

Hili Katazo la mikutano ni hofu na madhara ya 2010-2015 kuwaruhusu cdm kuendelea kujitanua. Huyo Magufuli ana nongwa na ana chuki binafsi na cdm, kwakuwa anajua fika cdm ndio kinakubalika na kizazi hiki, huku ccm ilikubalika na watu wenye elimu duni na wa kizazi kilichopita, ndio maana kwa sasa kuna matumizi makubwa ya vyombo vya dola ili ccm iendelee kukaa madarakani. Siku zote Magufuli anapambana aiue cdm, akiamini kabisa iwapo cdm itakufa, basi anaamini automatically watu wataipenda ccm kitu ambacho hatafanikiwa, kwani ccm ni chama cha karne iliyopita (old generation)
 
You are absolutely right! Mimi sina ushabki wa kipuuzi! Lowasa ameijenga CDM, tena sana sana! Mfano, ingelikuwa Magufuli siyo kuua, kupoteza, kuwabambikia watu kesi ie persecutions, kuna mambo anayafanya mazuri. But as long as yanainvolve loss of life, to hell with the so called maendeleo! afadhali nile mavi kwenye uhuru kuliko keki kwenye utumwa

Mkuu kwanza nikupongeze kwa mchango wa kujiamini huku ukijisifia kuwa huna ushabiki wa kipuuzi. Unasema Lowassa aliijenga sana cdm, mkuu unajua maana maana ya kuijenga sana taasisi? Unaweza ukanionyesha alifungua matawi mangapi akiwa cdm kabla na na baada ya kuwa cdm? Ni mgombea gani angekosa kura akiwa cdm kwa ile hamasa iliyokuwepo? Yale mafuriko yaliyotokea kwenye vituo vya kujiandikisha kupiga kura yalikuwa ni kwasababu Lowassa yuko cdm? Kama aliijenga sana cdm, kipi kilichangia viongozi wengi wa kuteuliwa wa cdm kuondoka hata yeye akiwepo, hapo achia mbali yeye kurudi ccm. Ukiacha hizo kura 6m+ zinazopotoshwa kuwa zililetwa na Lowassa, je aliongeza kura ngapi baada ya uchaguzi ule mkuu maana kulifanyika chaguzi za marudio akiwa bado cdm.
 
Umeona hiyo nyomi ya kina mama? Aisee watu mna roho ngumu! Dah!🤦🏾‍♂️
Ujuwe mkitumia dola mtawauwa wengi.
Mkuu J Mushi, nyomi nimeiona, na huu ni mwaka wa uchaguzi, nikidhani sasa Chadema watahutubia issues serious kuhusu a way forward, lakini naona bado Chadema wanaendelea na siasa zile zile za matukio.

Mwenyekiti Mbowe amezungumzua mambo makubwa matano.

Jambo la kwanza ni Ziara ya viongozi wa kisiasa Ikulu. Hili ni tukio.

Jambo la Pili, Mwenyekiti Mbowe amezungumzia Barua kutoka kwa Msajili wa vyama vya siasa kwenda kwa vyama vyote kuhakiki uhai wao ili kutambua vyama vinavyostahili kushiriki uchaguzi. Hii ni hoja ya kiutendaji.

Jambo la Tatu, Mwenyekiti Mbowe amelaani vikali Tabia inayoshamiri ya watu wachache kutaka kutumia Ukabila kuligawa Taifa. Hili ni tukio.

Jambo la nne, Mbowe amezungumzia ushirikiano wa vyama na kusema chana chake kinathamini sana ushirikiabo na kitakuwa tayari kushirikiana na chama chochote chenye nia thabiti ya kulikomboa Taifa- hapa pekee ndio hoja ya msingi na ya maana, lakini bila kusema how, pia ni empty!.

Jambo la tano, Mbowe alikemea vikali kauli ya hatari na ya kibabe iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ally kwamba chama chake kitatumia Dola kushinda uchaguzi. Hili ni tukio.

Hizi siasa za matukio zitaifikisha wapi Chadema, wanawake ndilo kundi kubwa la wapiga kura, lini Chadema mtafanya mkutano na kuleta your own agendas na sio kuja kuhutubia kuhusu matukio, badala ya Chadema kuwa pro active kwa kutoa hoja zake, Chadema kazi yake ni kujibu tuu hoja za matukio.

Mtu anayezijua siasa za nchi hii kuelekea uchaguzi Mkuu akisikiliza hizo hoja 5 za Mwenyekiti, akisema Chadema hamna sera, mmeishiwa hoja, what are you standing for, ni hakuna, atakuwa anawaonea?.

Gap ya Chadema kutokuwa na watu ma strategists kama Zitto na Kitila, is very visibly seen!.

P
 
Back
Top Bottom