Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

Yanayojiri katika Kongamano la Wanawake wa CHADEMA katika Ukumbi wa Mlimani City DSM leo March 8, 2020

Ni Jumapili tulivu ambayo ni siku ya Wanawake duniani.Katika Taifa letu Wanawake wa Chadema wanafanya Kongamano lao kubwa katika Ukumbi wa Mlimani City DSM.

Idadi kubwa ya wawakilishi wa Wanawake wa Chadema kutoka mikoa yote tayari wako DSM kuhudhuria Kongamano hili.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hili anatarajiwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani nchini na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Aikael Mbowe.

Sisi wa Molemo Media tutakuwa hapa kuwahabarisha watanzania na dunia kwa Ujumla yale yote yatakayojiri hususan hotuba ya Freeman Mbowe kwa wanawake na Taifa kwa ujumla.

Karibuni sana.

---------------------------------------------------

Ukumbi wa Mlimani City linakofanyika Kongamano hili kumepambwa vema huku akina mama wakiwa wanawasili kwa wingi maeneo haya wakiwa na sare maalum za chama kikuu cha upinzani nchini Chadema.

Ni furaha sana na shangwe kuu zimetanda hapa.Wengi wakijaribu kudadisi yatakayotokea hapa ikiwemo Hotuba inayosubiriwa kwa hamu ya mwanasiasa maarufu zaidi Afrika Mashariki Freeman Mbowe.ikumbukwe Mbowe aralihutubia Taifa kupitia Kongamano hili ikiwa ni siku moja kabla ya hukumu ya kesi ya kisiasa dhidi ya wanasiasa wakuu wa upinzani nchini.Wananchi wengi wakidhani hukumu hii huenda ikawa ndiyo kipimo cha imani ya wananchi dhidi ya mahakama hususan tuhuma za kuingiliwa na serikali.
Wapigaadilii mtupeee na pesaa.mlizotumiaaa.mchabganuooo kufaa kufaaaan kama namwonaaaaaaaaa
Bosslady
 
Mkuu Molemo, kwanza asante kutuhabarisha and it's good to learn kuhusu Molemo Media, natumaini utatuletea live kupitia live streaming, naona kama umebeba mikoba ya Tumaini Makene, maana simsikii au na yeye ameisha jitambua?.

Hiki unachofanya sasa ndicho tulichowashauri mfanye toka ile 2015, mu invest into mass mobilization strategies za reaching out to reach the masses, mlipaswa muwe na redio yenu, TV yenu na interactive online media ya chama kabisa na sio kutegemea individual efforts.

Jamaa yangu alipokuja ile 2015 nilikuwa na matumaini makubwa
Elections 2015 - Mabadiliko Chanya ya Ujio wa Lowassa: CHADEMA Kuhama Ufipa!, Kuwa Makao Yake, Kituo cha TV na Redio!

Hata hivyo asante kutuhabarisha.
P
Kwanza nikushukuru kwa maoni yako nikuhabarishe soon utaviona vyote hewani
 
Pas
Usiwe watovu wa shukrani, naamini Lowassa alikuja Chedema kwa nia njema ya kusaidia na kiukweli amewasaidia sana!, mgombea gani wa Chadema angeweza kupata kura zaidi ya milioni 6?.

Hoja ya binaadamu yoyote atakufaje, iko nje ya uwezo wetu, sio mimi, sio wewe wa kusema, ni Mungu tuu pekee!.
P
pasco nimekutana na dada yako anakusalimia, anaitwa kwa ubini wa Mayalla nikamuliza Pascal mwandishi ni kaka yako?akanijibu Yule wa jamii forums? nikasema eeh! Basi tukaongea mengi sana.
 
Lengo la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Ndani ya Chadema kuna makundi mawili, wako wanaojitambua, na wasio jitambua. Wanaojitambua wakiisha gundua Chadema ipo ipo tuu na haina mpango wowote wala uwezo wa kushika dola, wanajiongeza na kutimka zao kujiunga na chama dola. Wasio jitambua wanaendelea kuishi kwa matumaini ila baada tuu ya Bunge kuvunjwa, kutatokea mass exodus, waliobakia ni wale wagumu kama wewe ambao mnajitambua na mnajua kabisa kuwa Chadema hivi ilivyo, kamee haiwezi kuja kushika dola, ila mnaendelea kuwepo kuonyeshea msimamo usio yumba, baada ya 2020, mnakwenda nayo chini!.
P
Paschal, tulia na ccm yako na sisi tuache na chadema yetu
 
Kama huo ndio ukweli wenyewe, nijirekebishe wapi?. Ukiwa mkweli wa type yangu, utausema ukweli jinsi ile ulivyo bila kujali ukweli huo utamfuruhisha nani na kumuudhi nani.

Sheria inayounda Tume ya Uchaguzi, NEC ni Tume huru, independent, sheria ikasema rais atateua Mwenyekiti, Mkurugenzi na Makamishna na wasimamizi wa Uchanguzi, returning officials bila kueleza hao makamisha watateuliwa kutoka wapi, hivyo hata akiteua makada watupu hakuna tatizo as long as watafuata sheria, taratibu na kanuni na ndio maana Lowassa kapata kura zaidi ya milioni 6 ambazo ni nyinyi kuliko hata zilizomuingiza JK ikulu ile awamu yake ya pili!.

Hoja ni Tume iwe more inclusive itende haki, uwanja wa ushindani uwe level.
P
Leo wamekulipa madai yako? toka uingie mkataba hujawahi kuchemka hivi.
 
Nendeni mkasome gazeti LA Mzalendo la Leo.Dk Slaa kawasiliba CDM vya kutosha
 
Lengo la chama chochote cha siasa ni kushika dola. Ndani ya Chadema kuna makundi mawili, wako wanaojitambua, na wasio jitambua. Wanaojitambua wakiisha gundua Chadema ipo ipo tuu na haina mpango wowote wala uwezo wa kushika dola, wanajiongeza na kutimka zao kujiunga na chama dola. Wasio jitambua wanaendelea kuishi kwa matumaini ila baada tuu ya Bunge kuvunjwa, kutatokea mass exodus, waliobakia ni wale wagumu kama wewe ambao mnajitambua na mnajua kabisa kuwa Chadema hivi ilivyo, kamee haiwezi kuja kushika dola, ila mnaendelea kuwepo kuonyeshea msimamo usio yumba, baada ya 2020, mnakwenda nayo chini!.
P
Please bakiza walau maneno machache.
"Don't talk confidential/discozidi issues in public"'.
Let them get what they deserve, maana walishauriwa lakini hawashauriki,ila nina Imani huko tuendako watabadilika.
" Chama cha siasa bora ni kile chenye mfumo madhubuti wa mawasiliano kwa wananchi"
 
Back
Top Bottom