Live coverage on JamiiForums
Iran wanashangilia mabomu waliyorusha kwenda Israel kama ambavyo Hamas walivyoshangilia Octoba 7 mwaka jana

Changamoto huja kwenye matokeo ya majibu ya Israel, ikumbukwe Iran ni kati ya mataifa yenye mfumo dhaifu wa ulinzi wa anga na hata ujasusi wao upo chini. Hivyo wakipata majibu huenda tukaona malalamiko yale yale kwamba Israel inaua wanawake na watoto.

Tumeshuhudia mara kadhaa wataalamu wake wa nyuklia wakiuawa ndani ya Tehran mji mkuu nk tumeshuhudia miezi kadhaa iliyopita kwenye maadhimisho ya kifo cha kamanda mkuu wa vikosi vya mapinduzi Qasim Soleimani walipigwa shambulio baya zaidi katika historia yao lililopelekea vifo vya zaidi ya watu 100

Wayahudi baada ya kumshinda Adolf Hitler na utawala wake wa wanazi walijiekea formula "We won't forget and we won't forgive" wakiwa na Maana hawatasahau mateso waliyopitia na kamwe hawatamsamehe ataethubutu kuwaumiza

Hii ina maana kwamba tukio la Iran lazima litajibiwa inavyostahili ni suala la muda tu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema uamuzi watakaochukua hakuna dola yoyote duniani itayoweza kuwazuia

 
Haya ndio madhara ya Baba wa Imani Ibrahim kuchepuka. Matokeo yake ameacha kizazi Cha ajabu sana Duniani.
 
Haya ndio madhara ya Baba wa Imani Ibrahim kuchepuka. Matokeo yake ameacha kizazi Cha ajabu sana Duniani.


Fafanua vizuri. Kwamba Ibrahimu ni mzinzi na bado anaitwa baba wa Imani? Umetumia vizuri ubongo wako kweli?? Au Bado upo katika utumwa wa akili ya kushikiliwa na waleta maandiko yaliyosimamia maslahi ya Wazungu!
 
Hana uwezo huo bila msaada. Kama isingekuwa msaada wa usiku kucha ndege za US, UK, Jordan na wengine wengi kwenye angala la mwarabu wa jordan, base nyingi za kijeshi z Israel zingewashwa moto maana Iron Dome ilianza kuchochwa na drones zilizotangulia.

Sio rahisi kihivyo mkuu
 
Wayahudi baada ya kumshinda Adolf Hitler na utawala wake wa wanazi walijiekea formula "We won't forget and we won't forgive" wakiwa na Maana hawatasahau mateso waliyopitia na kamwe hawatamsamehe ataethubutu kuwaumiza

Mayahudi gani walimshinda Hitler?

Hitler alipokea kipondo kutoka majeshi ya washirika wakiongozwa US, USSR, Britain na France.
 
Dola la kishia la Iran na dola la kizayuni ni mtu na ndugu yake. Allah awagonganishe wao kwa wao na awasalimishe Waislam na shari zao na awatoe waislam kati yao kwa salama.
 
Haya ndio madhara ya Baba wa Imani Ibrahim kuchepuka. Matokeo yake ameacha kizazi Cha ajabu sana Duniani.

Mtume wa Allah Ibrahim (Amani ya Allah iwe juu yake) hakuzini. Acha kumtukana. Yuko mbali na mnayomsingizia.

Wala hakuwa myahudi wala mkristo, bali alijisalimisha kwa Mola wake akamuabudu Yeye Peke yake wala hakuwa katika washirikina. Alikuwa ni mmoja wa Mitume wakubwa kabisa na alikuwa ni rafiki kipenzi wa Allah. Sio sababu ya matatizo kama unavyomsingizia.

Amani ya Allah iwe juu yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…