Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Leteni photoDuh, nimeiona '' nyomi''
Kwa haya yanayoendelea kwenye siasa watanzania tunasema asante Rais Samia Suluhu kwa kurejesha amani nchini pamoja na kuimarisha democrasiaNi Asubuhi tulivu siku ya Jumatano,
Katika Jiji hili kuu la Kibiashara la Dar es Salaam leo majira ya saa 7:35 mchana anatarajiwa kutua mwanamapinduzi wa kweli Tundu Antipas Lissu ambaye anarejea nchini mwake baada ya kulazimika kuwa uhamishoni kwa takriban miaka 6 kutokana na Jaribio la kutaka kumuua.
Tundu Lissu mpinzani mkuu wa aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania John Magufuli anarudi nchini baada ya mazungumzo ya Maridhiano ya kisiasa yanayoendelea kati ya CCM na Chadema yaliyoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitangaza mwanzoni mwa mwezi huu kuondolewa kwa zuio haramu la mikutano ya hadhara lililowekwa kinyume na Katiba na mtangulizi wake John Magufuli.
Mapokezi ya Mwanasiasa huyo mashuhuri yataongozwa na Jabali la Siasa za Tanzania na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Viongozi mbalimbali wa chama hicho na wafuasi wa Chadema waliojiandaa kufanya maandamano makubwa ya kumpokea.
Maandamano hayo ya Mapokezi yatakwenda moja kwa moja Mpaka Uwanja wa Bulyaga Temeke Mwisho ambapo umeandaliwa Mkutano mkubwa wa Hadhara utakaohutubiwa na Lissu kuanzia saa 8 mchana.
Kama kawaida yetu sisi wa Molemo Media tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri katika Mapokezi hayo tangu anabusu ardhi ya Tanzania na Kisha Mkutano mkubwa wa Hadhara katika viwanja vya Temeke Mwisho.
Akizungumza na waandishi wa Habari hapo Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mapokezi ya Lissu Home Coming Mchungaji Peter Msigwa aliyekuwa ameambatana na Katibu wa Kamati Catherine Ruge alisema maandalizi yote yamekamilika na Watanzania watarajie mapokezi makubwa kuwahi kutokea hapa nchini.
Msigwa alisema chama kimeandaa mapokezi hayo kutokana na mazingira yaliyomlazimisha Lissu kukimbia nchi yake na Sasa anarudi nyumbani baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuanza kurejesha nchi katika ustaarabu wa kisiasa unaotakiwa.
Kamati hiyo pia inaundwa na Baraka Mwago ambaye ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani.
Karibuni Sana!
Tundu Lissu Awasili
Ilipotimu majira ya saa 7 mchana Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu amewasili na kupokelewa na Viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu John Mnyika, Viongozi wa Kamati ya Mapokezi, Wajumbe wa Kamati Kuu na Viongozi wa Mabaraza.
Msafara kuelekea Temeke waanza
Tundu Lissu amelakiwa na maelfu ya watu waliojipanga nje ya Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, wengine wakiwa kando kando ya Barabara huku Kiongozi huyo akiwa amepanda gari ya wazi.
Vikundi kadhaa vya waimbaji wa nyimbo na ngoma vimeshiriki Mapokezi hayo yanayoonekana makubwa na ya aina yake
Katika msafara huu wa Mapokezi Kuna maelfu ya vijana waendesha bodaboda wakiwa wamefunga bendera za Chadema huku wakipiga honi mfululizo kuashiria Furaha ya ujio wa Kiongozi huyo.
Jambo jingine kubwa linalovutia kwenye Mapokezi haya ni idadi kubwa ya watu hususan kinamama waliojipanga kandakando mwa barabara huku wakipunga mikono na kupiga vigelegele.
Lissu Awasili Ullwanjani Temeke saa 10.00 Jioni
Msafara wa maandamano makubwa ya Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu umewasili hapa viwanja vya Bulyaga Temeke Mwisho.
Watu ni wengi kweli kweli na wengine wanashindwa kuingia ndani ya eneo la Uwanja.
Kamanda wa Kanda Maalum Jumanne Muliro yuko ndani ya Uwanja huu kusimamia na kuongoza zoezi la Usalama
Polisi wamefanya kazi kubwa Sana ya kusimamia Usalama kuanzia Uwanja wa Ndege Mpaka hapa Uwanjani Bulyaga
Mwenyekiti Mbowe awasili Uwanjani saa 10.15 Jioni
Mwenyekiti wa Chadema anawasili hapa viwanja vya Bulyaga na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na kukumbatiana kwa Furaha kubwa huku Umati mkubwa hapa Uwanjani ukilipuka kwa Shangwe
View attachment 2495165
View attachment 2495166
View attachment 2495167
View attachment 2495168
Duuh Watu wa Mungu walimwombea Mtishi wao. Wanalia kwa furaha
Ameni na Mungu ambariki sana Rais SamiaKwa haya yanayoendelea kwenye siasa watanzania tunasema asante Rais Samia Suluhu kwa kurejesha amani nchini pamoja na kuimarisha democrasia
Heee makubwa haya. Bila demokrasia haya tungeyajua wapi?LISSU:Katiba mbovu inaleta TOZO na kupunguza Ugali wa watoto mezani.
Mbowe: CDM inatafuta Watu LAKI 5 pekee DSM ambao,
wanatosha kuitoa CCM madarakani Kwa maandamano.
Hivyo kuharakisha upatikanaji wa KATIBA mpya b4 2025.
LISSU: Wamasai wameondolewa Roliondo Ili wanyama wetu wapelekwe sokoni uarabuni.
LISSU: Kesi ya UGAIDI ya Mbowe ilitengenezwa na s100 Ili kuzuia CHOKOCHOKO za KATIBA mpya.
Watu kama utitiri
Hivi hao wanafunzi walikokotwa kwa Tela?
Imependeza sana. Nderemo nderemo na vifijoTundu Lissu amelakiwa na maelfu ya watu waliojipanga nje ya Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, wengine wakiwa kando kando ya Barabara huku Kiongozi huyo akiwa amepanda gari ya wazi.
Vikundi kadhaa vya waimbaji wa nyimbo na ngoma vimeshiriki Mapokezi hayo yanayoonekana makubwa na ya aina yake
Hahaa, nategemea thread zianzishwe tuzijadili Kwa machache nilofanikiwa kuyasikia.Heee makubwa haya. Bila demokrasia haya tungeyajua wapi?
Ukute Rais kafanya makusudi ili mafisadi wapate kusemwa vizuri.
Kama mnavyojua kumsema Fisadi ndani mwako ni ngumu.
Hongera sana Jeshi la Polisi kwa kudumisha amani na utulivu.Watu ni wengi kweli kweli na wengine wanashindwa kuingia ndani ya eneo la Uwanja.
Kamanda wa Kanda Maalum Jumanne Muliro yuko ndani ya Uwanja huu kusimamia na kuongoza zoezi la Usalama
Polisi wamefanya kazi kubwa Sana ya kusimamia Usalama kuanzia Uwanja wa Ndege Mpaka hapa Uwanjani Bulyaga
Hahahaa sawa ngoja tusubiriHahaa, nategemea thread zianzishwe tuzijadili Kwa machache nilofanikiwa kuyasikia.
Si unajua JF kwanza.
Hazijachanwa kwa maelekezo ya DC ?? 🤣🤣enzi hizo.Nimepita hapa maeneo ya temeke naona hamasa ni kubwa sana ni sare na bendera za chadema zimeanza kupepea
Safi sanaKatibu Mkuu John Mnyika akimkaribisha Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na kutoa salamu za chama amepaza sauti kuhusu kilio Cha wananchi Cha kupanda Bei za bidhaa Karibu zote nchini na kuitaka Serikali kuchukua hatua za haraka na za muda mfupi kurekebisha Jambo hilo.
Chato pengineYule jamaaa anajiita countywide alileta Uzi kuwa hakuna watu,yeye alienda airport gani?
Ha haha[emoji23]Watasema ni Freemason
Hawadanganyiki na Uhuni wa CCM na Chawa waoWatanzania wa jana sio wa leo!