Yanayojiri Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu, na Mkutano wa Hadhara Temeke Leo Jumatano 25/1/2023

Yanayojiri Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu, na Mkutano wa Hadhara Temeke Leo Jumatano 25/1/2023

LISSU:Katiba mbovu inaleta TOZO na kupunguza Ugali wa watoto mezani.

Mbowe: CDM inatafuta Watu LAKI 5 pekee DSM ambao,

wanatosha kuitoa CCM madarakani Kwa maandamano.

Hivyo kuharakisha upatikanaji wa KATIBA mpya b4 2025.

LISSU: Wamasai wameondolewa Roliondo Ili wanyama wetu wapelekwe sokoni uarabuni.

LISSU: Kesi ya UGAIDI ya Mbowe ilitengenezwa na s100 Ili kuzuia CHOKOCHOKO za KATIBA mpya.

LISSU: Pasipokuwepo na nguvu ya UMMA mtaani, Mkt Mbowe atatulizwa ktk meza ya maridhiano.
 
Ni Asubuhi tulivu siku ya Jumatano,

Katika Jiji hili kuu la Kibiashara la Dar es Salaam leo majira ya saa 7:35 mchana anatarajiwa kutua mwanamapinduzi wa kweli Tundu Antipas Lissu ambaye anarejea nchini mwake baada ya kulazimika kuwa uhamishoni kwa takriban miaka 6 kutokana na Jaribio la kutaka kumuua.

Tundu Lissu mpinzani mkuu wa aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania John Magufuli anarudi nchini baada ya mazungumzo ya Maridhiano ya kisiasa yanayoendelea kati ya CCM na Chadema yaliyoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitangaza mwanzoni mwa mwezi huu kuondolewa kwa zuio haramu la mikutano ya hadhara lililowekwa kinyume na Katiba na mtangulizi wake John Magufuli.

Mapokezi ya Mwanasiasa huyo mashuhuri yataongozwa na Jabali la Siasa za Tanzania na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Viongozi mbalimbali wa chama hicho na wafuasi wa Chadema waliojiandaa kufanya maandamano makubwa ya kumpokea.

Maandamano hayo ya Mapokezi yatakwenda moja kwa moja Mpaka Uwanja wa Bulyaga Temeke Mwisho ambapo umeandaliwa Mkutano mkubwa wa Hadhara utakaohutubiwa na Lissu kuanzia saa 8 mchana.

Kama kawaida yetu sisi wa Molemo Media tunatarajia kuwaletea kila kitakachojiri katika Mapokezi hayo tangu anabusu ardhi ya Tanzania na Kisha Mkutano mkubwa wa Hadhara katika viwanja vya Temeke Mwisho.

Akizungumza na waandishi wa Habari hapo Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mapokezi ya Lissu Home Coming Mchungaji Peter Msigwa aliyekuwa ameambatana na Katibu wa Kamati Catherine Ruge alisema maandalizi yote yamekamilika na Watanzania watarajie mapokezi makubwa kuwahi kutokea hapa nchini.

Msigwa alisema chama kimeandaa mapokezi hayo kutokana na mazingira yaliyomlazimisha Lissu kukimbia nchi yake na Sasa anarudi nyumbani baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuanza kurejesha nchi katika ustaarabu wa kisiasa unaotakiwa.

Kamati hiyo pia inaundwa na Baraka Mwago ambaye ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani.

Karibuni Sana!

Tundu Lissu Awasili

Ilipotimu majira ya saa 7 mchana Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu amewasili na kupokelewa na Viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu John Mnyika, Viongozi wa Kamati ya Mapokezi, Wajumbe wa Kamati Kuu na Viongozi wa Mabaraza.

Msafara kuelekea Temeke waanza

Tundu Lissu amelakiwa na maelfu ya watu waliojipanga nje ya Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, wengine wakiwa kando kando ya Barabara huku Kiongozi huyo akiwa amepanda gari ya wazi.

Vikundi kadhaa vya waimbaji wa nyimbo na ngoma vimeshiriki Mapokezi hayo yanayoonekana makubwa na ya aina yake

Katika msafara huu wa Mapokezi Kuna maelfu ya vijana waendesha bodaboda wakiwa wamefunga bendera za Chadema huku wakipiga honi mfululizo kuashiria Furaha ya ujio wa Kiongozi huyo.

Jambo jingine kubwa linalovutia kwenye Mapokezi haya ni idadi kubwa ya watu hususan kinamama waliojipanga kandakando mwa barabara huku wakipunga mikono na kupiga vigelegele.

Lissu Awasili Ullwanjani Temeke saa 10.00 Jioni

Msafara wa maandamano makubwa ya Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu umewasili hapa viwanja vya Bulyaga Temeke Mwisho.

Watu ni wengi kweli kweli na wengine wanashindwa kuingia ndani ya eneo la Uwanja.

Kamanda wa Kanda Maalum Jumanne Muliro yuko ndani ya Uwanja huu kusimamia na kuongoza zoezi la Usalama

Polisi wamefanya kazi kubwa Sana ya kusimamia Usalama kuanzia Uwanja wa Ndege Mpaka hapa Uwanjani Bulyaga

Mwenyekiti Mbowe awasili Uwanjani saa 10.15 Jioni

Mwenyekiti wa Chadema anawasili hapa viwanja vya Bulyaga na kupokelewa na Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na kukumbatiana kwa Furaha kubwa huku Umati mkubwa hapa Uwanjani ukilipuka kwa Shangwe

View attachment 2495165
View attachment 2495166
View attachment 2495167
View attachment 2495168
Kwa haya yanayoendelea kwenye siasa watanzania tunasema asante Rais Samia Suluhu kwa kurejesha amani nchini pamoja na kuimarisha democrasia
 
LISSU:Katiba mbovu inaleta TOZO na kupunguza Ugali wa watoto mezani.

Mbowe: CDM inatafuta Watu LAKI 5 pekee DSM ambao,

wanatosha kuitoa CCM madarakani Kwa maandamano.

Hivyo kuharakisha upatikanaji wa KATIBA mpya b4 2025.

LISSU: Wamasai wameondolewa Roliondo Ili wanyama wetu wapelekwe sokoni uarabuni.

LISSU: Kesi ya UGAIDI ya Mbowe ilitengenezwa na s100 Ili kuzuia CHOKOCHOKO za KATIBA mpya.
Heee makubwa haya. Bila demokrasia haya tungeyajua wapi?

Ukute Rais kafanya makusudi ili mafisadi wapate kusemwa vizuri.

Kama mnavyojua kumsema Fisadi ndani mwako ni ngumu.
 
FnUtPYeXEAQVYoW

=
FnUtPYdWAAMD0Hx

=
FnUtPYeXkAIqMI9
Watu kama utitiri
 
Tundu Lissu amelakiwa na maelfu ya watu waliojipanga nje ya Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, wengine wakiwa kando kando ya Barabara huku Kiongozi huyo akiwa amepanda gari ya wazi.

Vikundi kadhaa vya waimbaji wa nyimbo na ngoma vimeshiriki Mapokezi hayo yanayoonekana makubwa na ya aina yake
Imependeza sana. Nderemo nderemo na vifijo
 
Heee makubwa haya. Bila demokrasia haya tungeyajua wapi?

Ukute Rais kafanya makusudi ili mafisadi wapate kusemwa vizuri.

Kama mnavyojua kumsema Fisadi ndani mwako ni ngumu.
Hahaa, nategemea thread zianzishwe tuzijadili Kwa machache nilofanikiwa kuyasikia.

Si unajua JF kwanza.
 
Watu ni wengi kweli kweli na wengine wanashindwa kuingia ndani ya eneo la Uwanja.

Kamanda wa Kanda Maalum Jumanne Muliro yuko ndani ya Uwanja huu kusimamia na kuongoza zoezi la Usalama

Polisi wamefanya kazi kubwa Sana ya kusimamia Usalama kuanzia Uwanja wa Ndege Mpaka hapa Uwanjani Bulyaga
Hongera sana Jeshi la Polisi kwa kudumisha amani na utulivu.

Pongezi kwa IGP
 
Katibu Mkuu John Mnyika akimkaribisha Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu na kutoa salamu za chama amepaza sauti kuhusu kilio Cha wananchi Cha kupanda Bei za bidhaa Karibu zote nchini na kuitaka Serikali kuchukua hatua za haraka na za muda mfupi kurekebisha Jambo hilo.
Safi sana
 
THE PRESIDENT IS BACK... Welcome home Tundu Lissu, magufuli alibaka na kulawiti uchaguzi mkuu 2020 na kutuletea bunge na utawala wa hovyo kabisa kuwahi kutokea nchini.
 
Back
Top Bottom