Mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi nchini Marekani Ronald Ernest Paul kutoka jimbo la Texas na ambaye kwa sasa ni mstaafu miaka ya nyuma aliwahi kusema maneno haya (Tizama video clip niliyoiambatanisha hapa) wakati akichangia hoja ya hali ya amani katika nchi za Mashariki ya Kati, haswahaswa baina ya Israeli na Palestina.
Ifuatayo ni summary ya aliyasema katika video hiyo.
#) Marekani inahusika moja kwa moja na haiwezi kujitenga na mgogoro baina ya Israeli na Palestina kwakuwa imekuwa ikiipa Israeli misaada ya kifedha na silaha kwa miaka mingi- fedha na silaha ambazo ndizo hutumika kuwaua Wapalestina.
#) Vile vile ukiangalia historia, taifa la Israel ndio muasisi wa kikundi cha Hamas. Kikundi hichi kilianzishwa na Israeli kwa lengo la kumdhoofisha Yasser Arafat,(aliyekuwa mwanaharakati na mpigania raisi wa Palestina) ambaye alikuwa ni m/kiti wa chama cha PLO.
#) Ni Marekani hiyo hiyo iliyoamua kusimika utawala wa kidemokrasia Mashariki ya Kati, ambapo wapalestina kwa kutumia demokrasia hiyo hiyo wakuchagua Hamas ambayo ilikuwa maarufu kipindi hicho iwaongoze.
#). Na mengine mengi utayasiki katika video hii.
View attachment 2778027