LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Mkuu, lengo la Israeli ni kuhakikisha wanajizolea sehemu ingine kubwa ya ardhi (Imperialism) maana uwingi wa wapalestina ni lazima udhibitiwe.

Ndo maana Israeli wanashutumiwa kwa kufanya mauaji ya halaiki au ya kupunguza idadi ya watu.

Kama umemsikiliza Netanyahu (bibi) amesema operesheni ya sasa ni ya kumaliza kazi ili Wapalestina wasiwe na nguvu yoyote.

Tayari nchi nyingi zailaumu Israeli kwa hatua nzito kupitiliza kuita wanajeshi 300,000 ili kukabiliana na wapiganaji wapatao 3000 kwenye taifa la wapalestina lenye watu milioni 2 na nusu.
Palestina sio gaza tu , kuna miji mingine ya west bank na ramallah, huko hamna vita wanaenddlea kuzaliana tu , huwezi wazuia wasizaane, waarabu wana asili ya kuzaa watoto wengi
 
Lakini mkuu si huwa tuna waambia kila siku ya kuwa mdhamini mkuu wa usalama Israel ni USA nyinyi mna bisha?
Kiufupi kwa hali ilivyo iwapo Hizibullah ikianzisha mashambulizi kamili na yenye nguvu bila msaada wa Marekani ni lazima Israel izidiwe.
Ni kweli US anagharamia mno ulinzi wa Israel, dola billion 3 kila mwaka ($3bn).

US anajaribu kuzuia huo mzozo usisambae zaidi na kuwa Vita ya kikanda.
 
Huenda baadhi ya wakubwa wa Mossad, Shinbet, IDF wakajiuzulu baadae kwa kushindwa kuzuia hili shambulio.
Kwa maoni yangu mimi naona kwamba watu wengi kwenye hiyo "system" hawampendi Netanyahu na kundi lake la wabaguzi na wenye msimamo mkali ndani ya serikali yake.

Kwani tayari alikuwa na kesi mahakamani hivyo huenda pia ni mpango wa kutaka kumuondoa kwa kutumia mashambulizi haya na hatua anazochukua kukabiliana na Hamas.
 
Mkuu, lengo la Israeli ni kuhakikisha wanajizolea sehemu ingine kubwa ya ardhi (Imperialism) maana uwingi wa wapalestina ni lazima udhibitiwe.

Ndo maana Israeli wanashutumiwa kwa kufanya mauaji ya halaiki au ya kupunguza idadi ya watu.

Kama umemsikiliza Netanyahu (bibi) amesema operesheni ya sasa ni ya kumaliza kazi ili Wapalestina wasiwe na nguvu yoyote.

Tayari nchi nyingi zailaumu Israeli kwa hatua nzito kupitiliza kuita wanajeshi 300,000 ili kukabiliana na wapiganaji wapatao 3000 kwenye taifa la wapalestina lenye watu milioni 2 na nusu.
Sasa hao Hamas kwanini walivyoanza vita walilenga kuwauwa raia ambao ni un armed na sio wanajeshi?

Unajua kumuua raia ambaye hana silaha wala sio kizuizi cha kukufanya ushindwe kufikia lengo ni uvunjifu wa sheria za kivita?

Kwanini wasiwashambulie wanajeshi wa mipakani kisha wasikilize respond ya Wayahudi?

Na hao Wayahudi ni kweli hilo eneo sio lao wametumia tu ubabe kukaa?

Hakuna namna nyingine ambayo Palestina wanaweza wakaitumia kama suluhu ya kupata haki yao ukiachana na majaribio ya vita ambayo katika historia hayajawahi kuwasaidia zaidi ya kuwatia hasara na kupoteza uhai kwa raia wake?
 
Kwa maoni yangu mimi naona kwamba watu wengi kwenye hiyo "system" hawampendi Netanyahu na kundi lake la wabaguzi na wenye msimamoi mkali ndaniya serikali yake.

Kwani tayari alikuwa na kesi mahakamani hivyo huenda pia ni mpango wa kutaka kumuondoa kwa kutumia mashambulizi haya na hatua anazochukua kukabiliana na Hamas.
Hii serikali ya sasa ya Netanyau ndio inatajwa imejaa wazuyuni wahafidhina mno, isitoshe ilikuwa kila mara inakabiliwa na maandamano ya raia kupinga mageuzi kwenye mfumo wa mahakama.

Ila usishangae hili shambulio likawaunganisha ili wapigane na Hamas, alafu baadae ndio wakawajibishana.
 
Palestina sio gaza tu , kuna miji mingine ya west bank na ramallah, huko hamna vita wanaenddlea kuzaliana tu , huwezi wazuia wasizaane, waarabu wana asili ya kuzaa watoto wengi
Palestina ina maeneo yake mawili (territories) yanotambulika kimataifa Ukanda wa Gaza ( Gaza Strip) na Ukanda wa Magharibi (West Bank)

Mji mkuu wa Gaza ni Gaza au Gaza City na mji mwingine ndani yake ni Khan Yunis

Ramallah ni mji ndani ya Ukanda wa Magharibi (West Bank) pamoja na miji mingine ya Jericho, Jerusalem, Bethlehem, Hebron, Tubas, Jenin, Nablus, Salfit, Turkam na Qualqiliya.
 
Sasa hao Hamas kwanini walivyoanza vita walilenga kuwauwa raia ambao ni un armed na sio wanajeshi?

Unajua kumuua raia ambaye hana silaha wala sio kizuizi cha kukufanya ushindwe kufikia lengo ni uvunjifu wa sheria za kivita?

Kwanini wasiwashambulie wanajeshi wa mipakani kisha wasikilize respond ya Wayahudi?

Na hao Wayahudi ni kweli hilo eneo sio lao wametumia tu ubabe kukaa?

Hakuna namna nyingine ambayo Palestina wanaweza wakaitumia kama suluhu ya kupata haki yao ukiachana na majaribio ya vita ambayo katika historia hayajawahi kuwasaidia zaidi ya kuwatia hasara na kupoteza uhai kwa raia wake?
Huu mzozo una sura nyingi sana, mazungumzo ya amani yamefanyika mengi sana Ila suluhu bado imekuwa ndoto kupatikana.

Pande zote mbili zimekuwa zikishambulia na kuua raia kila zinapopigana (japo Wapalestina ndio huumia zaidi maana hawana silaha za kisasa wala jeshi kama Israel)
 
US kapeleka ile aircraft carrier yake kubwa na ya kisasa zaidi ya Gerald Ford kuitisha Hezbollah wasijiingize kwenye mzozo.

T14 Armata
US haiendi sababu ya Hezbollah inaenda sababu ya Iran. Israel on its own inaweza pigana two fronts na vita zake zote huwa inakuwa na fronts mbili au tatu.

Hamas + Hezbollah wanaweza pigwa na Israel muhimu kuwepo ground offensive kotekote. Ford inaenda kuweka deterrence dhidi ya Iran, Syria na Iraq. Jordan sio wajinga kupigana na Israel, wala Egypt kwa sasa sio washamba kiasi hicho.
 
Palestina ina maeneo yake mawili (territories) yanotambulika kimataifa Ukanda wa Gaza ( Gaza Strip) na Ukanda wa Magharibi (West Bank)

Mji mkuu wa Gaza ni Gaza au Gaza City na mji mwingine ndani yake ni Khan Yunis

Ramallah ni mji ndani ya Ukanda wa Magharibi (West Bank) pamoja na miji mingine ya Jericho, Jerusalem, Bethlehem, Hebron, Tubas, Jenin, Nablus, Salfit, Turkam na Qualqiliya.
Poa hapo nimekupata, kwenye hili suala la vita West Bank ipo au haipo? Mi ninachojua kwenye vita ni Gaza strip pekee
 
US haiendi sababu ya Hezbollah inaenda sababu ya Iran. Israel on its own inaweza pigana two fronts na vita zake zote huwa inakuwa na fronts mbili au tatu.

Hamas + Hezbollah wanaweza pigwa na Israel muhimu kuwepo ground offensive kotekote. Ford inaenda kuweka deterrence dhidi ya Iran, Syria na Iraq. Jordan sio wajinga kupigana na Israel, wala Egypt kwa sasa sio washamba kiasi hicho.
Egypt wana mkataba wa amani na Israel,
 
Sio kwamba hiyo Ford inaenda kuisaidia Israel kuzuia silaha kuingia Gaza ?...

Usishangae wakashiriki kwenye kusaidia offensive dhidi ya Gaza kama itafanywa maana raia wao baadhi wametekwa na wengine wameuawa.

isitoshe Biden anajaribu kujijenga kisiasa maana ana uchaguzi mbeleni na republic wanamtupia lawama kwa hili tukio........hivyo atafanya hayo kuiridhisha Israel na wapiga kura wake

... isitoshe Israel imeshapewa baadhi ya silaha na ammunition kutoka US kwa ajili ya uvamizi wa Gaza.

Poa hapo nimekupata, kwenye hili suala la vita West Bank ipo au haipo? Mi ninachojua kwenye vita ni Gaza strip pekee
Kuna mada ingine nimeeleza uzuri tu.

Vita kwa sasa ipo Ukanda wa Gaza ambayo ndio makao makuu ya Hamas.

Ila Israeli jana walikosea makombora yao yakatua kusini mwa Lebanon na kuua wapiganaji wa Hezbollah.

Hezbollah wamejibu mapigo na Marekani wamewasihi wasijiingize kwenye huu mgogoro.

Ndo Israeli wajiandaa kufanya mashambulizi ya ardhini.

Ukanda wa Gaza unachukua kama maili 25 hivi kutoka kaskazini kwenda kusini kama saa moja hivi, ni sehemu ndogo sana.
 
Egypt wana mkataba wa amani na Israel,
Israeli ilipigana na Hezbollah mwaka 2006 sidhani kama ulifuatilia na hakupatikana mshindi.

Israeli hawezi kupigana vita ya ardhini ya mtaa kwa mtaa.

Ndo maana sasa hivi wameita wanajeshi 300,000 ili kuwe na mauaji ya kutisha kwa wapalestina.

Ndo maana ni lazima atumie ndege za F-16 kupiga mabomu makali na sasa hivi Israeli imeshutumiwa kutumia mabomu ya Phosphorus ambayo yamepigwa marufuku.

Lengo la Israeli kutumia mabomu hayo ni kutaka kufumua njia za chini kwa chini.
 
Hata wasingekuwa na mkataba, kuna sababu kwanini Egypt hawawazi kuipigania Palestina.
Egypt baada ya vita ya Yom Kipur waliingia mkataba na Egypt wa amani na Israel chini ya usimamizi wa Marekani. Mkataba uliosababisha mpaka rais wao Anwar Sadat akauwawa na Muslim Brotherhood. Egypt hawawezi kuingilia vita Palestina hata siku moja, mkataba unawabana.
 
Wanashambulia zaidi majengo yanayohifadhi silaha, nyumba za viongozi wa Hamas na miundombinu mingine tu Hamas na Islamic jihad tena baada ya kuwa na intelligence kuhusu kina nani wapo humo.

Hamas wametishia kuua mateka mashambulizi yakiendelea zaidi dhidi ya raia wao.

Mkuu Hamas sio wapuuzi kiasi hicho kuhifadhi silaha kwenye majengo hali ya kuwa wanajuwa Israel atayashambulia majengo hayo hamas silaha watakuwa wana ficha kwenye mahandaki.
 
🤣🤣🤣🤣🤣Marekani huwa inanichekesha sana. Kwanini hakwenda Urusi kuwakomboa wale watoto mwamba Putin aliowachukuwa toka Ukraine? Badala yake amekimbilia kwenda kufungua kesi mahakamani.

Hapo GAZA ameona ni kibonde na dhaifu mno, faster ameshatia mguu kuonyeaha dunia umwamba wake🤣🤣🤣🤣🙈🙈
Marekani vs Russia
Marekani vs China
Marekani vs North Korea
Haziwezi kupigana, wako makini sana busara ya hali juu hutumika.
Marekani hawezi kuingia vitani kwa kuingilia ugomvi usio wake.
 
Back
Top Bottom