LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Tuseme tu ukweli Israeli haiweza kupambana vita na Iran maana kwenye huu mgogoro Israeli imeonesha udhaifu mkubwa
IRAN anajijua sana inaviziwa na mataifa mengi kama USA na ulaya magharibi sasa akisema aingie vita na mtu pale itakuwa shida sana.
Afu kingine kutoka Iran mpk Israel pana mwendo ni mbali itampa shida sana.

Afu kingine Iran hana urafiki na Saudi Arabia.
Qatar yeye mwenyewe ananunua siraha marekani sasa wapi wapi Iran sina uhakika kama ataenda huku.
 
Yani mkuu ndo wale wanaosema North Korea inauwezo wa kupigana na USA?
Korea Kaskazini ina uwezo wa kurusha kombora la Nyuklia na likatua Marekani na kusababisha maafa makubwa.

Vilevile Marekani nao wana uwezo wa kurusha makombora kadhaa ya Nyuklia ambayo yataifuta Korea Kaskazini kwenye uso wa Dunia.

Ndo maana hadi leo Marekani na Korea Kaskazini waheshimiana.

Nchi yoyote yenye uwezo wa kuwa na silaha za Nyuklia ni ya kuogopwa na ni Iran tu ndo haujulikani imefikia wapi lakini yaaminika kuwa tayari imefikisha kiwango cha makali ya bomu lake.

Ndo maana nikasema Israeli hawawezi kupigana na Iran peke yao bila msaada wa mataifa ya magharibi na Marekani.
 
Mkuu iran wanagoma kwamba wao hawajahusika wakati equipment za hamas wanazotumia ni za Iran.
Nafikili hizo mbinu ni Iran waliwapa kuna kitu walilenga sasa naona mpango umegoma.
Mossad wapo kazini tayari kuna taarifa kulikuwa na kikao kizito mjini Beirut na ramani nzima imechorwa pale.

Wengi wamejiuliza sana jinsi Hamas walivyofanya operesheni yao ambayo imeonekana ni "unique" yaani ya kipekee.

Wayahudi wengi waliuawa usiku wa kuamkia jumamosi na hadi kufikia asubuhi idadi ilikuwa kubwa.

Kwenye vitongoji kama Be'er Sheva watu wamechinjwa sana na hawa wapiganaji na wameonekana ni wenye kupata mafunzo khasa.
 
Mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa mjumbe wa baraza la wawakilishi nchini Marekani Ronald Ernest Paul kutoka jimbo la Texas na ambaye kwa sasa ni mstaafu miaka ya nyuma aliwahi kusema maneno haya (Tizama video clip niliyoiambatanisha hapa) wakati akichangia hoja ya hali ya amani katika nchi za Mashariki ya Kati, haswahaswa baina ya Israeli na Palestina.

Ifuatayo ni summary ya aliyasema katika video hiyo.

#) Marekani inahusika moja kwa moja na haiwezi kujitenga na mgogoro baina ya Israeli na Palestina kwakuwa imekuwa ikiipa Israeli misaada ya kifedha na silaha kwa miaka mingi- fedha na silaha ambazo ndizo hutumika kuwaua Wapalestina.

#) Vile vile ukiangalia historia, taifa la Israel ndio muasisi wa kikundi cha Hamas. Kikundi hichi kilianzishwa na Israeli kwa lengo la kumdhoofisha Yasser Arafat,(aliyekuwa mwanaharakati na mpigania raisi wa Palestina) ambaye alikuwa ni m/kiti wa chama cha PLO.

#) Ni Marekani hiyo hiyo iliyoamua kusimika utawala wa kidemokrasia Mashariki ya Kati, ambapo wapalestina kwa kutumia demokrasia hiyo hiyo wakuchagua Hamas ambayo ilikuwa maarufu kipindi hicho iwaongoze.

#). Na mengine mengi utayasiki katika video hii.

Your browser is not able to display this video.
 
Nchi yoyote yenye uwezo wa kuwa na silaha za Nyuklia ni ya kuogopwa na ni Iran tu ndo haujulikani imefikia wapi lakini yaaminika kuwa tayari imefikisha kiwango cha makali ya bomu lake.
Iran siraha za nyukria hana ila Israel wanazo.

Iran alipigwa vita sana kuhusu hizo siraha. Kuna kipindi mpka wanasayansi wa Iran wa atomic waliuwawa wengi sana na USA pamoja na mossad , walipukutika kama mchanga mkavu uliopo kwenye lorry afu lipo speed 150km/h.

Mpaka wakaomba wataalamu kutoka urusi.
 
Marekani huyo huyo anazid kupeleka silaha.. na kuwazuia palestina kupokea zao
 
Mkuu, hakuna aliethibitisha kuwa Iran haina silaha za Nyuklia kwa sababu wamegoma kutoa access.

Lakini yajulikana mfadhili mkubwa wa mradi wa nyuklia kwa Iran ni Urusi.

Pia Iran sasa hivi yatengeneza makombora mbalimbali pamoja na ndege za Shahed wazifahamu zatumika kule Ukraine.

Hivyo heshima kwa Iran na kuogopwa ipo.

Tatizo Israeli imeshindwa kupenyeza majasusi wake ili kupata taarifa za kuhusu nyuklia maana kama hufahamu, Israeli wamewaua sana wataalam na wanasayansi wa Iran wanoshiriki kwenye mpango wa nyuklia.

Iran imekuwa ikiwakamata majasusi kadhaa wa Israeli na kuwaua au kuwafunga jela kwa makosa ya espionage.
 
Mchana wa leo, Israeli imeripotiwa kulipua kanisa la Kikristo la Mtakatifu Porphyrius lililopo kwenye Mji wa Gaza.

Kanisa hilo la Mtakatifu Porphyrius, linatajwa kuwa ni kanisa kongwe na kubwa zaidi katika ukanda nzima wa Gaza ambalo linaendelea kutoa huduma ya kiroho mpaka sasa.Kanisa hilo linapatikana katika Kota za Mtaa wa Zaytun zilizopo kwenye Mji Mkongwe wa Gaza.

Hapo awali, kanisa hilo lilipewa jina la askofu wa wa kwanza wa karne ya tano (5) wa ukanda huo wa Gaza (Mtakatifu Porphyrius) ambaye kaburi lake limejengwa kwenye kona ya kaskazini-mashariki mwa kanisa hilo.
 
Bora tunaongeza maarifa km hivi🤝
 
Mkuu unajua akili za Iran.
Iran ni wafadhili wa Hezbollah kwa kila kitu mafunzo, pesa na silaha.

Iran ni wafadhili wa Hamas kwa mafunzo, pesa na silaha.

Inasemwa ni Iran lakini wahusika wakuu wa jamaa wa Revolutinary Guards ambao husaidia pia harakati za Syria inopigana na Israeli kule kaskazini kwenye milima ya Golan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…