Watu waliobaki Gaza ya kaskazini kwa makisio ni karibu laki nne.Hiyo ni idadi ya wakazi wa mkoa mzima fulani wa Tanzania.Na walioko kusini kila giza likiingia wanatiririka kurudi makwao.Sababu wanayosema ni kuwa hakuna sehemu salama Gaza hivyo ni afadhali wabaki na kama ni kuuliwa wawe majumbani mwao au kwenye magovou ya nyumba zao.
Jana kuna bibi mmoja aliyezaliwa mwaka 1944 ambaye alikaa nje ya nyumba yake IDF wakamuua.Mwanzoni alikwenda kusini halafu akarudi nyumbani kwake kaskazini.wako wengi kama yeye.Tuseme idadi ya watu mjini Gaza inaongezeka kwa kasi.Hali hiyo ina maana Israel itakuwa imeshindwa kuikalia Gaza na imeshindwa kuwafuta Hamas hapo.Hata kama chakula hakipelekwi lakini wanakula japo kwa shida.
Dah inasikitisha sana hali wanayopitia Palestine hasa wa ghaza
Ila huo ndio ukweli hakuna sehem salama kwasasa kule ghaza popote tu unakufa
Mwanzoni waliambiwa waende kusini wakapigwa huko huko wakaambiwa sijui khan younis wakapigwa huko huko
Kiufupi israhell alikua target zake awaje kule rafah karibu na misri ili wakimbilie huko ghaza itokomee
Ila wamesahau kuna muda mtu ukimpa mateso anakua anaona bora tu aishi nayo maana hakuna namna
Nawakumbusha tena wanaowaza kufutwa kwa hamas wakae wakijua hili hakitakaa litokee labda kama mazayuni watapiga nyuklia
Na hali inapoendea huko mazayuni watakubali matakwa ya hamas rasmi mana hakuna namna
Walijua miezi mitatu baada ya kuingia ghaza hamas itakua dhoofu ila kila leo hamas inaingia nguvu na hamasa
Kwakweli kwa mpaka sasa walilofanikiwa hamas nikuua raia wasio na hatia nakubomoa majumba pale ghaza
Hivi vifaru vya merkava vimeishia wapi maana sijasikia kusifiwa na wachafuzi uchwara
Na yale maji ya bahari waloanza kuyajaza walifikia wapi
Hamas kundi teule