LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Kwa jinsi shirika la kijasusi la Israeli la mossad lilivyo na uwezo mkubwa Basi hii inanifanya niamini huenda hili jambo walikua wanalijua litatokea hivyo wameacha kwa makusudi kabisa litokee ili kuonyesha dunia uchokozi wa hamas na kupata sapoti kubwa pale watakapoanza kujibu mapigo, na hili linaenda sambamba kabisa na suala la Saudi Arabia na Israeli kutaka kuestablish diplomatic relationship. Hivyo Kuna mchezo Hamas na palestina wanachezewa bila kujua.
 
Israel ilikuwa inaenda kufanya makubaliano na Saudi Arabia. Kuna mkono wa mtu kuyasimamisha makubaliano hayo na inajulikana ni nani hawataki Israel na Saudi waongee lugha moja.

Hii coordination ya Hamas sio ya kwao peke yao kuna baraka za wafadhili wao. Hamas wameshambulia raia zaidi kuliko jeshi, visingizio hamna Israel ikijibu. Ila Hezbollah bora isiingie maana uchumi wa Lebanon utayumba zaidi, uachwe utengamae kidogo. Pale Gaza ni kama hawana cha kupoteza sana maana ni kama ghetto kubwa.
 
Alaf wameamua kuwashambulia leo sabato kwa sababu wanajua Israeli nzima wamepumzika, ngoja jua lizame sabato iishe, wataona kila rangi.
 
Lakini at least wanafurukuta,siyo kama sisi hapa Tanzania kudai tume huru tu ya uchaguzi kwa maandamano bila hata bunduki tunashindwa.
 
Muda wa Israel kulaumiwa umefika. UN, Human Rights Watch, Save The Children na mashirika kibao ya haki za binadamu muda wao huu wa kuandika nyaraka nyingi.

Collateral damage itakuwa kubwa soon kuna watu watalalamika Israel ikijibu mashambulizi
Waache wapambane tu, hakuna mafanikio yasio lipwa kwa damu hata hao wayahudi kufika hapo wamepitia kwenye madhira makubwa kwa zaidi ya mamia ya miaka lakini hilo hali kuwafanya wakate tamaa kupambana
 
Hii ni mbaya sana bora wangetulia vita si vya kukurupuka mtaisha vibaya mno ,raia bora waanze kukimbia kabisa wale wajomba wakianza kurusha yao hawajui huruma ina rangi gani ...
Waache wapambane maana wasinge kuwa wana pambana wenda hata hichi kidogo walicho nacho wange kuwa wamenyanganywa.
 
Majibu ya Israel huwa ni ya kikatili mark my words huu ndo mwisho wa hamas na mwanzo wa maisha mabaya sana kwa wapalestina
Tuwaombee heri hayo yasiwafike,nadhani haijathibitika bado vifo kwa hiyo ni vizuri tuombe utulivu uwepo.

Shida ya vita haina mwenyewe mimi ninaechokoza najua mbinu za kujificha wakati wanaonizunguka hawazijui hizo plan adui akijibu wanaoumia ni wale ambao hawajui A wala B ya mashambulizi hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…