LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Sasa mama hana hatia sio gaidi,hana silaha ya aina yoyote alafu apigwe kweli kuna watu hamna akili.
Kama alivyokuwa Joshua ila wakamuua.
Hawa wametumia ubinadamu sana kwa huyu mama.

Btw, hii clip ni fupi sana kutoa taswira ya tukio zima.
Katika ulinzi kuna mazingira yasiyoruhusu mijadala.
 
Ukanda wa Gaza: Makumi ya roketi yarushwa kuelekea Israeli.

Makumi ya roketi yamerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel Jumamosi asubuhi, Oktoba 7, na kusitisha makubaliano ya usitishwaji mapigano yaliyoheshimishwa kwa ujumla tangu kumalizika kwa vita vya siku tano mwezi Mei. Tawi la kijeshi la Hamas limetangaza kuwa limeanzisha operesheni iitwayo "Mafuriko ya Al-Aqsa" dhidi ya Israel.

Ufyatulianaji wa risasi, kuanzia maeneo kadhaa katika Ukanda wa Gaza, ulianza kabla ya 6:30 asubuhi saa za Mashariki ya Kati na kuendelea karibu dakika arobaini na tano baadaye.

Nchini Israeli, ving'ora vya onyo vimesikika katika miji kadhaa karibu na Palestina, pia huko Jerusalemu lakini pia ndani zaidi katika eneo hilo, kaskazini na mashariki, kulingana na jeshi.

Roketi imeanguka kwenye mji wa Yavne, kusini mwa Tel Aviv, ambapo mtu mmoja amejeruhiwa kidogo, kulingana na Magen David Adom, sawa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Israel. Mwanamke mwenye umri wa miaka sitini ameuawa "kwa pigo la moja kwa moja", na watu wengine 15 wamejeruhiwa kusini mwa Israeli, linasema shirika la Magen David Adom.

Jeshi la Israel limeripoti kupenya kwa "idadi isiyojulikana ya magaidi" kwenye ardhi ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza. "Wakazi katika maeneo jirani ya Ukanda wa Gaza wametakiwa kusalia nyumbani," jeshi limeongeza.

Mwezi Mei, Israel ilianzisha mashambulizi dhidi ya Islamic Jihad ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha vita vya siku tano kati ya jeshi la Israel, Islamic Jihad na makundi mengine yenye silaha katika eneo hilo, na kugharimu maisha ya Wapalestina 34 na mwanamke mmoja wa Israel.

Zaidi ya roketi elfu moja zimerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel, nyingi zikiwa zimenaswa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel. Israel kwa upande wake ilikuwa imeongeza mashambulizi ya anga katika eneo hilo dogo.

Hamas, ambayo ilichukua mamlaka huko Gaza mwaka 2007, ilikuwa imejitenga na mzozo huu.

Imechapishwa: 07/10/2023 - 08:13 Na:RFI

Video na TRT AFRIKA
View attachment 2786228
We mr uharo acha ujinga bwana mbona heading na video ni tofauti🤣🤣🤣🤣
 
Sijasema kama inauhusiano ila imekua inatoa taarifa
Ishu taarifa wanazotoa ni za kweli ama sio zakweli
Hatujasema kama zina uhusiano ama laa
Taarifa nyingi xina ukweli. Nime share taarifa yao ikisema waliouawa ni 9, ila mleta mada kaleta taarifa tofauti akidai imeandikwa na hao ak7dai waliuawa ni 100, wakati waliuawa ni 9 waliuawa kwenye mlipuko uliotokea kwenye factory ya silaha Hamas
Screenshot_20240109-143759_Chrome.jpg
 
Jeshi la Israel kupitia msemaji wake lasema linapajua alipo kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar kazungukwa na mateka wa Israel waliowateka anawatumia kama ngao yaani human shield ili asishambuliwe na jeshl la Israel wameshapaina alipo
 
Basi wamue tu

USSR

Sent from my Infinix X6511G using JamiiForums mobile app
 
Israel kama inataka kuendelea kubaki lazima ikubali yaishe kwa kukubali kuundwa taifa la Palestina waishi kwa ujirani.Kinyume na hivyo hawana nafasi ya kubaki salama kwa kutumia ubabe iliojiamini nao.

Tathmini hiyo inazingatia kwamba upande wa Gaza imebaki jeshi la IDF kutolewa tangazo tu la kushindwa japo kwa uhakika wameshashindwa.

Tangazo hilo bila shaka kwa aibu halitotolewa na IDF bali litajitangaza lenyewe.

Sababu ya tathmini yangu mbali na Gaza ni kuwa upande wa kaskazini ya Israel waliko Hizbollah kumechafuka.Kwa mara ya mwanzo wapiganaji hao wameanza kutumia zile droni za Kamikaze ambapo jana walishambulia makao makuu ya jeshi la Israel yanayoongoza jeshi upande wa kaskazini. Jeshi la IDF limethibitisha kupigwa kwa kambi yake hiyo na bila kutoaji kiwango cha hasara.Muhimu ni kuwa hizo droni zimefika hapo bila kizuizi chochote na zina uwezo wa kupiga sehemu nyengine yoyote ya Israel.

Upande wa ukingo wa magharibi kwenye maeneo mengi vijana wanapigana kabisa na kulitia hasara jeshi la Israel badala ya kukimbia na kujificha kama ilivyokuwa zamani.

ikikumbukwa kuwa kuna kuna kundi jengjine kubwa la Houth linalonyemelea baharini na kwamba washirika wake wako taabani, itaonekana kuwa Israel katika vita vinavyoendelea hatoweza kuishi kwa ubabe na uhasama kwa muda mrefu bila kudhurika kwa maangamizi kamili.

Ni mambo machache upande wa Gaza nimeyataja ijapokuwa kwa sasa kwa matangazo ya channel zao na za mashirika mengine ya habari ni kuwa Hamas wamepata kasi sana katika kuwapiga askari wa Israel kuliko ule muda majengo yalipokuwa yanabomolewa.
 
Israel kama inataka kuendelea kubaki lazima ikubali yaishe kwa kukubali kuundwa taifa la Palestina waishi kwa ujirani.Kinyume na hivyo hawana nafasi ya kubaki salama kwa kutumia ubabe iliojiamini nao.
Tathmini hiyo inazingatia kwamba upande wa Gaza imebaki jeshi la IDF kutolewa tangazo tu la kushindwa japo kwa uhakika wameshashindwa.
Tangazo hilo bila shaka kwa aibu halitotolewa na IDF bali litajitangaza lenyewe.
Sababu ya tathmini yangu mbali na Gaza ni kuwa upande wa kaskazini ya Israel waliko Hizbollah kumechafuka.Kwa mara ya mwanzo wapiganaji hao wameanza kutumia zile droni za Kamikaze ambapo jana walishambulia makao makuu ya jeshi la Israel yanayoongoza jeshi upande wa kaskazini.Jeshi la IDF limethibitisha kupigwa kwa kambi yake hiyo na bila kutoaji kiwango cha hasara.Muhimu ni kuwa hizo droni zimefika hapo bila kizuizi chochote na zina uwezo wa kupiga sehemu nyengine yoyote ya Israel.
Upande wa ukingo wa magharibi kwenye maeneo mengi vijana wanapigana kabisa na kulitia hasara jeshi la Israel badala ya kukimbia na kujificha kama ilivyokuwa zamani.
ikikumbukwa kuwa kuna kuna kundi jengjine kubwa la Houth linalonyemelea baharini na kwamba washirika wake wako taabani, itaonekana kuwa Israel katika vita vinavyoendelea hatoweza kuishi kwa ubabe na uhasama kwa muda mrefu bila kudhurika kwa maangamizi kamili.
Ni mambo machache upande wa Gaza nimeyataja ijapokuwa kwa sasa kwa matangazo ya channel zao na za mashirika mengine ya habari ni kuwa Hamas wamepata kasi sana katika kuwapiga askari wa Israel kuliko ule muda majengo yalipokuwa yanabomolewa.
Israel sasahivi ipo phase ya kuua viongozi makundi ya kigaidi imeshamuua kiongozi mwingine wa Hamas aliyekuwa akirusha maroketi Israel ameuawa akiwa Syria na kiongozi mwingine wa Hezbollah ameuawa jana
 
Back
Top Bottom