Kabla ya Isaka kuna mtoto alizaliwa tena wa kiume, unaweza kutueleza alienda wapi? Je alirithi nini?? La pili, Yakobo na kizazi chake walienda Misri, je kizazi cha Essau kilienda wapi?? Kumbuka mtoto wa kwanza wa Ibrahim naye alipata uzao.
Kabla ya Isaka mtoto Alie zaliwa alikua anaitwa Ishmael ambaye Ibrahim alizaa na kijakazi wake ambaye alikua akiitwa hajira
Soma👇
Mwanzo 16 : 2 Sarai akamwambia Abramu, Basi sasa, Bwana amenifunga tumbo nisizae, umwingilie mjakazi wangu labda nitapata uzao kwa yeye. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.
Mwanzo 16 : 15 Hajiri akamzalia Abramu mwana wa kiume; Abramu akamwita jina lake Ishmaeli, yule mwanawe, ambaye Hajiri alimzaa.
Baada ya hapo Sarah akamchukia Yule kijakazi ambaye ni Hajira akamtesa mpaka yule Kijakazi akakimbia lakin hata hivyo Biblia inasema Mungu alimrudisha.
So Kibiblia haionyeshi alienda wapi Ishmael alienda wapi lakin ukisoma history yake alienda inaonyesha Ishamel aliishi pande za Shuru kuelekea Misri!! Soma👇
Mwanzo 25 : 17 Na hii ndiyo miaka ya maisha ya Ishmaeli, miaka mia na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.
Mwanzo 25 : 18 Wakakaa toka Havila mpaka Shuri, unaoelekea Misri, kwa njia ya kwenda Ashuru. Akakaa katikati ya ndugu zake wote.
Hapa inaonyesha baada ya kufa so alipo zikwa Sasa na hii inaonyesha hayo ndo makao yake na kunaa baadhi ya Wana theology huwa wanasema Ishmael ndo alikua Babu wa Mohammad yule wa Waislamu na ndo Chimbuko la Kislmu limetokea hapo na pia wanasema ndo mtu wa kwanza Kuzungumzia Ki-arabu.
Kuhusu Urithi wa Ishmael Mungu alimbariki sana alimpa aridhi na aliapa atamfanya Kuwa Taifa kubwa soma👇
Mwanzo 17 : 20 - Na kwa habari za Ishmaeli nimekusikia, nimembariki, nitamzidisha, nami nitamwongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nami nitamfanya awe taifa kuu.
Lakini pia unaweza soma Mwanzo hiyo Sura 25 nzima utaona uzao wa Ishmael
Unaweza fuatilia Mkuu Ili ujue kiundani zaidi.
Esau inaonyesha baada ya Kuwa na Ugomvi Mkubwa na ndugue Esau alihama kutoa nchi ya ndugue akaelekea katika Nchi ya Seiri katika Nyika ya Edomu ambayo kwa Sasa ipo Yordani .
Soma👇
Mwanzo 36 : 8 Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu.
Piah ukisoma hapa inaonyesha Kuwa Ujumbe unatumwa kwenda Esau ambaye alikua ktka makazi yake.
Mwanzo 32 : 3 Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.
Unaweza fuatilia ujue zaidi Mkuu