T14 Armata
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 12,362
- 41,886
Israel hawafanyi kazi kwa nguvu pekee, akili haziachani na nguvu zao.Aliuliwa Ahmad Yassin yule kiongozi wao kipofu na Hamas ikaendelea atakua huyo Ismael Haniya ndg
Huwezi ona Israel inapendelea Bashar al Assad aondoke, labda ijue Syria itafeli zaidi ya sasa endapo atakuja Rais mwingine pale Syria.
Sheikh Ahmad aliuwawa sababu alikuwa mwiba, huyu Haniyeh na Ahmad nani alikuwa mkorofi zaidi?
Israel ilifurahia mapinduzi ya Rais Mohamed Morsi pale Egypt, sababu yeye ni Muslim Brotherhood kundi korofi kwa Israel badala yake kaja General El-Sisi hana shida na Israel.
Wala Israel haipendi Rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas aondoke. Wewe uliwahi ona Abbas anafanya nini la maana? Unaweza mlinganisha Abbas na mtangulizi wake Yasser Arafat? Na kwanini kifo cha Arafat kina utata hadi leo.