LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

LIVE Yanayojiri vita ya Israel dhidi ya Palestina na HAMAS

Live coverage on JamiiForums
Katika hali isiyo ya kawaida israel imelazimika kufanya mobilization ya askari zaid ya 300000 ili kukabiliana na uvamizi wa wapigania uhuru kutoka palestine yaani HAMAS. Kilichonishangaza ni askari hawa waakiba yaani reservist kuitikia wito bila waswas wowote tena wengine wakiletwa na wazazi wao.

Kilichonivutia zaidi ni ujio wa reservists ambao walikua mataifa ya nje kula bata wamerudi nyumbani kuungana wenzao kwenda kwenye uwanja wa medani. Hali hii inatufundisha uzalendo sio maneno ila ni vitendo. Mpaka reservest wa miaka hamsini nao wako comfortable kabisa tayari kupokea order tayari kwenda front kwenye uwanja wa medani
Ni 360k siyo 300k.

Lakini yote tisa ukweli ni kwamba Israel ndiyo inayofanya wapalestina wawe na roho za kigaidi
 
Unaweza enda upande wa Hamas maana kuna waarab wa Qatar na Iran wanatoa wanatoa mpunga allah anapopambaniwa na ikitokea umeuwawa basi utaenda peponi kuinjoy mabikira 70 na mito ya pombe
Kumbe unajadili kwa mihemko ya kishabiki,
Ndio maana umeandika kitu usichokijua kwenye post yako #3
 
Hali ya Jeshi la Israeli (IDF) ni mbaya tunaweza sema hivyo kutokana na kupungukiwa baadhi ya vifaa muhimu kama vile bullet proof vests, boots, mpaka sare za jeshi (combat gears), jambo lililopelekea kuomba misaada kwa nchi rafiki wakati wakisuburia oda ya vifaa hivyo waliyoagiza kurokat China ambayo itachukua siku kadhaa kukamilika.

Zile Stori za vijiwe vya gahawa kwamba hakuna kama jeshi la Israel zinazidi kupoteza mvuto.

+++--++++-++++-++++-++++-++++-+++-+++

Chanzo: The timess of Israel
IMG_20231012_075502.jpg
 
Uzalendo unaupata kama Taifa ni moja ambalo halina ubaguzi wa aina yoyote. Kazi ya Kiongozi bora ni kuliunganisha taifa lake - Juzi tumesikia Waziri Mkuu wa Islael ameunda Serikali mpya ambayo itafanya kazi pamoja kwa kipindi hiki huku akimkaribisha hasimu wake mkuu wa kisiasa kuwa ndani ya Serikali hiyo.
 
Gaza War, Day 6:
Heavy Israeli strikes in Gaza overnight, dozens dead; Air Force bombs operational command centers, kills senior member of Hamas naval force; IDF now focusing on bombing Gaza's terror tunnels.
 
Ukanda wa Gaza: Makumi ya roketi yarushwa kuelekea Israeli

Makumi ya roketi yamerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel Jumamosi asubuhi, Oktoba 7, na kusitisha makubaliano ya usitishwaji mapigano yaliyoheshimishwa kwa ujumla tangu kumalizika kwa vita vya siku tano mwezi Mei. Tawi la kijeshi la Hamas limetangaza kuwa limeanzisha operesheni iitwayo "Mafuriko ya Al-Aqsa" dhidi ya Israel.

Ufyatulianaji wa risasi, kuanzia maeneo kadhaa katika Ukanda wa Gaza, ulianza kabla ya 6:30 asubuhi saa za Mashariki ya Kati na kuendelea karibu dakika arobaini na tano baadaye.

Nchini Israeli, ving'ora vya onyo vimesikika katika miji kadhaa karibu na Palestina, pia huko Jerusalemu lakini pia ndani zaidi katika eneo hilo, kaskazini na mashariki, kulingana na jeshi.

Roketi imeanguka kwenye mji wa Yavne, kusini mwa Tel Aviv, ambapo mtu mmoja amejeruhiwa kidogo, kulingana na Magen David Adom, sawa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Israel. Mwanamke mwenye umri wa miaka sitini ameuawa "kwa pigo la moja kwa moja", na watu wengine 15 wamejeruhiwa kusini mwa Israeli, linasema shirika la Magen David Adom.

Jeshi la Israel limeripoti kupenya kwa "idadi isiyojulikana ya magaidi" kwenye ardhi ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza. "Wakazi katika maeneo jirani ya Ukanda wa Gaza wametakiwa kusalia nyumbani," jeshi limeongeza.

Mwezi Mei, Israel ilianzisha mashambulizi dhidi ya Islamic Jihad ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha vita vya siku tano kati ya jeshi la Israel, Islamic Jihad na makundi mengine yenye silaha katika eneo hilo, na kugharimu maisha ya Wapalestina 34 na mwanamke mmoja wa Israel.

Zaidi ya roketi elfu moja zimerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel, nyingi zikiwa zimenaswa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel. Israel kwa upande wake ilikuwa imeongeza mashambulizi ya anga katika eneo hilo dogo.

Hamas, ambayo ilichukua mamlaka huko Gaza mwaka 2007, ilikuwa imejitenga na mzozo huu.

Imechapishwa: 07/10/2023 -
 
Kuna nguo kuchanika au kuharibika katika mapamano, na pia kunanjeshi la akiba wamekuja kusadia IDF!.
Kwahy muda wote huo kabla ya vita walikuwa wanavaa nguo za majumbani wakiwa jeshini.?
 
Ni 360k siyo 300k.

Lakini yote tisa ukweli ni kwamba Israel ndiyo inayofanya wapalestina wawe na roho za kigaidi
Ukishakuwa mfuasi wa munyaazi mungu tu bas unaanza kuwa trained mapema kuwa na roho ya kikatili maana unaanza kumezeshwa chuki dhidi ya watu wa Imani nyingine mfano Alshabaab, Boko Haram, ISIS, Zanzibar nk
 
Ukanda wa Gaza: Makumi ya roketi yarushwa kuelekea Israeli

Makumi ya roketi yamerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel Jumamosi asubuhi, Oktoba 7, na kusitisha makubaliano ya usitishwaji mapigano yaliyoheshimishwa kwa ujumla tangu kumalizika kwa vita vya siku tano mwezi Mei. Tawi la kijeshi la Hamas limetangaza kuwa limeanzisha operesheni iitwayo "Mafuriko ya Al-Aqsa" dhidi ya Israel.

Ufyatulianaji wa risasi, kuanzia maeneo kadhaa katika Ukanda wa Gaza, ulianza kabla ya 6:30 asubuhi saa za Mashariki ya Kati na kuendelea karibu dakika arobaini na tano baadaye.

Nchini Israeli, ving'ora vya onyo vimesikika katika miji kadhaa karibu na Palestina, pia huko Jerusalemu lakini pia ndani zaidi katika eneo hilo, kaskazini na mashariki, kulingana na jeshi.

Roketi imeanguka kwenye mji wa Yavne, kusini mwa Tel Aviv, ambapo mtu mmoja amejeruhiwa kidogo, kulingana na Magen David Adom, sawa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Israel. Mwanamke mwenye umri wa miaka sitini ameuawa "kwa pigo la moja kwa moja", na watu wengine 15 wamejeruhiwa kusini mwa Israeli, linasema shirika la Magen David Adom.

Jeshi la Israel limeripoti kupenya kwa "idadi isiyojulikana ya magaidi" kwenye ardhi ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza. "Wakazi katika maeneo jirani ya Ukanda wa Gaza wametakiwa kusalia nyumbani," jeshi limeongeza.

Mwezi Mei, Israel ilianzisha mashambulizi dhidi ya Islamic Jihad ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha vita vya siku tano kati ya jeshi la Israel, Islamic Jihad na makundi mengine yenye silaha katika eneo hilo, na kugharimu maisha ya Wapalestina 34 na mwanamke mmoja wa Israel.

Zaidi ya roketi elfu moja zimerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel, nyingi zikiwa zimenaswa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel. Israel kwa upande wake ilikuwa imeongeza mashambulizi ya anga katika eneo hilo dogo.

Hamas, ambayo ilichukua mamlaka huko Gaza mwaka 2007, ilikuwa imejitenga na mzozo huu.

Imechapishwa: 07/10/2023 - 08:13 Na:RFI

View attachment 2774147
Israel inapigana na hamas na sio palestina nyie ndio wapotoshaji wakuu. Mnaingiza mkenge wajinga wengi wasiojua kutofautisha hamas na palestina.
 
Muda wa Israel kulaumiwa umefika. UN, Human Rights Watch, Save The Children na mashirika kibao ya haki za binadamu muda wao huu wa kuandika nyaraka nyingi.

Collateral damage itakuwa kubwa soon kuna watu watalalamika Israel ikijibu mashambulizi.
Wakishalaumiwa ndio inasaidia waliokufa kufufuka?
 
Gaza boarder, Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant amewaambia wanajeshi wake alipokuwa anawaaga kuingia Gaza.

Tunahamia kwenye kosa kamili lililosababisha sisi kuwepo hapa, Hamas ilitaka mabadiliko katika mji wa Gaza na itabadilika digrii 180 kutoka kwa kile ilichofikiria.

Watajuta wakati huu sababu Gaza haitarudi kama ilivyokuwa, hii historia itaandikwa katika vitabu na hata vitabu vitakatifu vya dini.

Kuandika historia haijawahi kuwa jambo rahisi kama wengi wanavyodhani.

View attachment 2778443

Moderator naomba usiunganishe uzi huu na zile nyingine sababu hii statement haipo katika muendelezo.
Binafsi naona kama muda wa kwenda huko bado maana naona bado magorofa yamesalia ilipaswa wayadondoshe yote ili uwe uwanja ndipo waingie!
 
Back
Top Bottom