Yanga atafika hatua ya robo fainali tena kwa kujihakikishia nafasi mapema kabisa

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kwa kikosi walichonacho na uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja bila kusahau wanavyoendelea kurekebisha makosa yao, naiona Yanga hii ikitinga hatua ya robo fainali mapema tu. Hata msimamo katika kundi lao, bado unatoa nafasi kwa kila timu kusonga mbele huku nikiamini Yanga yuko katika nafasi nzuri zaidi.

CRB anakwenga kufungwa Cairo katika mechi ijayo kwani Al Ahyl atataka kujihakikishia nafasi mapema tu kupitia mechi ya nyumbani huku Yanga ama akitoa sare huko Ghana au hata kushinda. Medeane akija Bongo, anachapika, kwahiyo tuna uhakika wa pointi 4 mpaka 6.CRB akija Bongo nae tunamaliza hesabu kujihakikishia ushindi/nafasi ya kufuzu.

Pia, Yanga atacheza mechi ya mwisho na Al Ahyl ambae atakuwa ameshafuzu wakati huo na atakuwa hana cha kupoteza na hivyo kuongeza uwezekano wa Yanga kutoka nae sare na hata kumfunga akiwa kwao(Cairo).

Muda utathibitisha,
 
Kila ushindi au sare ni motivation kwa mechi inayofuata ukizingatia msimamo katika kundi kwani timu hazijaachana sana kipointi.
Kwenye hatua ya makundi ukisubiri mechi ya mwisho ili uvuke unakuwa umeshachelewa. Sijaelewa unaposema Yanga itakuwa imejihakikishia nafasi mapema hata kwa kutoka sare mechi inayofuata wakati akipata natokeo hayo itabidi apate matokeo dhidi ya CRB na Al Ahly. Hiyo mapema ni ipi?
 
Mpira wa mdomoni na kwenye keyboard unanoga sana. Kazi uwanjani sasa.
 
hilo liko dhahiri kabisa mechi za maokoto imewadia Medeama anatoa 4 au 6,CRB ataacha 3 hapa tunashika nafasi ya pili kitu pwani...
 
Baada ya usajili wa dirisha dogo kumsajili namba 9 mwenye weledi wa kutosha
 
Mzee acha kuropoka mpra huchezwi mdomoni😝😝
 
Serikali inapiga marufuku ramli chonganishi kila siku
 
Yanga anashinda mechi zake mbili zinazofata na Medeama, pia Beleuzdad akija dar anafungwa yanga anafikisha point 10.

AL ahly hata akishinda misri. hamzuii yanga kufuzu
Kwahyo akishinda mechi mbili anakua na alama 10?
1+6 = 7~ ikaja 10 duhπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…