kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Mungu kajalia mechi ya Simba na Yanga ndiyo iliyoamua ubingwa. Mungu amejalia pia timu inayodhaminiwa na GSM imeifunga timu ambayo imekataa kudhaminiwa na GSM kwenye mechi ya maamuzi nani awe bingwa wa ligi. Mungu huyu wa ajabu amezidi kuonyesha maajabu yake kwa mechi ya Simba na Yanga kuchezeshwa na waamuzi wa kigeni.
Hoja ya kuwa GSM kadhamini timu nyingi kwenye ligi haina nguvu tena kisayansi na kiitifaki. Watakaoendelea kuileta hiyo hoja wanataka kuendelea kuidhoofisha Simba isiyaone mapungufu yake ya kweli dhidi ya Yanga na kuyatafutia ufumbuzi.
Yanga ni bora kuliko Simba katika nyanja ya wachezaji, uongozi na benchi la ufundi. Yanga kuifunga Simba mechi 5 mfululizo sio fluke. Simba warudi kwenye uhalisia wa mpira badala ya kupoteza muda na fedha zao kwenye mambo yanayoenda kinyume na sayansi za mpira.