Yanga ichukuliwe hatua kwa uharibifu iliyofanya juzi uwanja wa Mkapa


View: https://twitter.com/Tanganyikan/status/1731583096904933552?t=unY9MuR9N6TEWNKJQuA0FQ&s=19
 
Taasisi imara huwaga haisusi bali washikadau wote hushikamana na kuwa pamoja, kinyume chake taasisi yenu sio imara.
Hadi mambele huko watu wanagoma ili kuleta shinikizo na mabadiliko yanafanyika kutokana na mashinikizo hayo. Ni huko kwenu mlikolelewa kwenye mitazamo ya hovyo ndiyo mnadhani viongozi ni miungu watu hawawezi kukosea au kukosolewa.

hapo kwenye "5imba" simu yangu ikifikia hilo neno "s" hai-respond.
Utoto raha saaana
 
Hadi mambele huko watu wanagoma ili kuleta shinikizo na mabadiliko yanafanyika kutokana na mashinikizo hayo. Ni huko kwenu mlikolelewa kwenye mitazamo ya hovyo ndiyo mnadhani viongozi ni miungu watu hawawezi kukosea au kukosolewa.


Utoto raha saaana
Mbele wapi.....!!! labda hapo kwenye timu yenu, Newcastle kishashuka daraja mara mbili, ila sijawahi kuona wakisusa kwenda uwanjani,Nottingham Forest pamoja na historia yake ya UEFA tatu,imeporomoka huko imeangaika kupanda ila sijawahi kuona wakisusa kwenda uwanjani. Leeds sijui kama unaijua na inawezekana ni kawa na bishana na kijana mdogo,ila ndio timu iliyo mtoa Rio Ferdinand na Mark Viduka,hiyo timu ilikuwa inatoa changamoto Kwa Arsenal,Liverpool,Man Utd ikaporomoka ila sijawaona mashabiki wakisusa. Arsenal kala nane,Liverpool kala saba na Aston Villa,Man Utd kala sita na City,Barca kampiga Madrid sita nyumbani kwake na tano ugenini hawajawahi kususa.

Sijajua labda unapazungumzia mbele gani,hivi unawaona Chelsea na Man Utd matokeo wanayo yapata sasa hivi,ushaona mashabiki wake wakisusa uwanjani.

Ni nyinyi tu kwakuwa hamjitambui, mmeshushiwa kingilio buku tano mpaka tatu bado mmesusa, yaani hiyo mechi yenu mtakayo cheza na Wydad Dar hapa,kuna uwezekano mzunguko ukawa kipande cha sabauni na MoXtra, ukiwa na katoni moja ya MoXtra au mche wa sababuni unakaa VIP.

Kuhusiana na 's' simu yangu inashindwa kutambua hasa nikiandika "5imba" na vilevile hii simu inatumia AI kujua watu waliosusa, hata wewe mwenyewe ushaisusa timu yako na ndio maana wengi mnataka kujifariji na matokeo ya Yanga.
 
Kuhusiana na 's' simu yangu inashindwa kutambua hasa nikiandika "5imba" na vilevile hii simu inatumia AI kujua watu waliosusa, hata wewe mwenyewe ushaisusa timu yako na ndio maana wengi mnataka kujifariji na matokeo ya Yanga.
Unatumia nguvu kubwa kwa jambo lisilo na maana

Ila sijawaona mashabiki wakisusa
Wewe unafuatilia tu mambo ya viwanjani EPL, hayo mambo ya kususa utayajuaje ukiwa huko Nanjilinji? Kuna njia nyingi za kususa au kuonyesha hisia zako kwa mambo usiyoyakubali. Bahati mbaya katika kanchi kenu, baada ya kutishiwa na kutishika, mmeshindwa hata kubuni njia mbadala za kuzibana taasisi katika changamoto nyingi ambazo zimeshindwa kuzitatua. Huko EPL ulipotolea mifano ndiyo mabingwa wa kususa na kupinga, hao Simba unaowasema ni afadhali. Hii mitandao itumie vizuri utajifunza mengi, usibaki tu unatetea ujinga wa timu yako na kuongea mambo usiyoyajua.

Ngoja nimalizie kwa kukupa mifano michache halafu nikuache ukakojoe ulale.

Mashabiki wa EPL walipinga na kuandaa aina mbalimbali za kususa taratibu za kutangaza mechi za ligi hadi ikapelekea taratibu rafiki tuanza kutumika. Mashabiki wa Newcastle waliwahi kuamua kuchanga pesa kwa ajili ya hisani badala ya kulipia PPV kuiona timu yao dhidi ya Man U kupinga bei ya tiketi. Hiyo ni aina moja ya kususa. Mfano mwingine, mashabiki wa Borussia Dortmund waliwahi kususa kwa dakika 20 za mwanzo za mchezo halafu wakarusha mipira ya tennis uwanjani kupinga bei za tiketi. Mfano mwingine, karibia mashabiki 10,000 wa Liverpool waliwahi kususa kwa njia ya kuingia uwanjani halafu wakatoka kabla ya mechi kupinga bei ya tiketi. Mashabiki wa Man U walisusa kupinga mambo ya umiliki wa timu. Na kuna yale maandamano makubwa kule Brazil kabla ya Kombe la Dunia 2014. Utayajulia wapi haya?

Na nikwambie pia nilipokuwa naongelea mambele, sikuwa namaanisha tu kwenye mpira, kwenye sehemu za watu wanaojitambua njia tofauti zinaweza kutumika kuonyesha kutoridhishwa na mambo yanayoendelea. Halafu unaongelea kususa, unajua kuna wanachama wa Yanga waliwahi kuiteka timu kutoka katika mikono ya viongozi?
 
Uharibigu ufanywe na Makolo Dunduka NGANDA 5 G halafu adhabu ipewe YANGA.
We RAGE wee, MUNGU anakuona.
 
Sasa viwanjani si naona mashabiki wanaisupport timu yao na uzuri wenzetu attendance wanaitoa wakati uleule wa mechi ikiendelea. Man U washaifanyia fujo familia ya Glazer ila hawajawahi kususa kuiangalia, timu yao.

Haya hayo maandanano ya huko Brazil ya nini?Maana huko Brazil ndipo kuna machizi wa mpira.

Arsenal washabeba mabango ya kumtukana Kroenke mpaka uwanjani, ila sijawahi kuona wakisusa kuingia uwanjani.

Newcastle na aliyekuwa tajiri wao Ashley ,mashabiki wamemtukana sana Ashley ila sijawahi kuona wakisusa kuingia uwanjani na wameshuka daraja mara mbili. EPL kuna kipindi mashabiki wanakodi mpaka Chopa na kubeba ujumbe wao kama kitu fulani hawakitaki ila hawasusi kuingia uwanjani.

MBELE WATATAFUTA NJIA YA KUFIKISHA UJUMBE WAO,ILA HAWASUSI KUINGIA UWANJANI, SIJAWAHI KUONA NA UTAMADUNI HUO UPO KWA WAZUNGU WOTE.

Matatizo ya viongozi wao huwaga hawataki kuyahamishia kwenye mahudhurio viwanjani.

Nyie kama mmeamua kususa ni utoto na uchanga wenu wa kwenye soka,kwani njia zipo nyinyi za kufikisha ujumbe kuliko kususa.
 
Kumbe ni serikali sio nyie?
 
Nimekutolea mifano ambayo inaonyesha mashabiki wamesusa kwenda viwanjani bado unabisha tu. Na nimekuonyesha wengine wanakwenda uwanjani halafu wanatoka, hiyo yote ni kuonyesha wako serious na jambo lao. Kwani unadhani hao mashabiki wa Simba waliosusa wamesusa milele? Nia ni kufikisha ujumbe kama wanavyofanya huko unakotolea mifano na unaona kitendo walichofanya kimezaa matunda kwa hatua stahiki kuchukuliwa. Wewe kinachokuuma mashabiki wa Simba kususa ni nini, mbona umelivalia njuga halafu ni jambo limeshapita? Na nyie mlisusa kwenye mechi na Al Ahly mbona uwanja haukujaa hata nusu, tena hapo mmelishwa supu na kuletewa msanii mkubwaa kutoka Congo lakini wapiiii?
 
Brother mpira sisimuliwi na naviona na rudia tena ulaya hamna mbamba ,attendance wanaweka wakati uleule mechi ikiendelea. Ulaya hamna utoto huo wa kususasusa kwani inaonyesha ww ni mchanga.

Sasa kwani 5imba haijasusa baada ya kula tano,yaani unabisha mpaka vinavyo onekana.Hivi wewe mechi unatizama magoli tu,mbona mtangazi kama sikosei alikuwa Mzinga,wakati akitangaza mechi Al Ahly na nyinyi alisema serikali ndio iliwapangia waingie kwa idadi ile.

Al Ahly alikula tano na Mamelod ila sijasikia Al Ahly wakisusa kwenda uwanjani. Wydad finalist wa AFL na CAF championship 2023 kapigwa mechi mbili mfululizo tena moja kwake na timu ambayo hakuitegemea, sasa subiria hapo Jmosi uone hilo nyomi lake akicheza na ww.

Kususa ni utoto na inaonyesha bado hujapevuka.
 
Brother mpira sisimuliwi na naviona na rudia tena ulaya hamna mbamba ,attendance wanaweka wakati uleule mechi ikiendelea. Ulaya hamna utoto huo wa kususasusa kwani inaonyesha ww ni mchanga.
Unachobisha ni nini hasa? Unabisha hiyo mifano niliyoitoa kwamba hayo hayajatolea au ni nini hasa unachobisha unaposema Ulaya mashabiki hawasusi? Kukusaidia tu kususa kwa kiingereza rahisi ni "boycott", basi tumia bando lako vizuri ujielimishe, ingia google andika "fans boycott in EPL" uone mkeka utakatandikwa hapo. Maneno mengii halafu hakuna unachosema.

Halafu usidhani umetutoa kwenye reli, mada kuu bado ni uharibifu mlioufanya uwanjani, naona unajaribu kubadili mada kwa kukazia mambo yaliyopita.

mtangazi kama sikosei alikuwa Mzinga,wakati akitangaza mechi Al Ahly na nyinyi alisema serikali ndio iliwapangia waingie kwa idadi ile.
Hahahah, daah! Unazungumza kitu gani sasa?
 
Kwani mimi hapa sijatoa mifano?
Nimekujliza hayo maandanano ya Brazil ya wapi huja ni jibu,tena huko Brazil watu ni machizi wa mpira.

Sijamtoa mtu kwenye reli uzuri clip si zipo ...... jambo lipo serikalini,nilicho shangaa kuituhumu Yanga ila kwenye ile Clip wanaopiga fataki na kurukaruka kwenye viti ni waarabu wa mkopo walio kula tano.Mechi haiwahusu njooni mtizame mpira kiustaraabu mwisho wa siku mnafanya mashabiki wote walio enda uwanjani waonekane hawana maana.

Ulaya mashabiki hawasusi kuingia uwanjani,ila wana njia zao za kufikisha ujumbe wanapo chukizwa.Ndio maana nimekuuliza ww mpira unatizamaga magoli,ila attendance ile wanayo tangazaga husikiagi.

Ni udogo na uchanga wenu wa kwenye soka ndio unawafanya msuse.
 
Kwa hiyo hiyo unasema mifano niliyotoa ya Newcastle, Man U na Liverpool haikutokea au unataka kusema nini? Na hii ni mifano ya haraka tu ila najua nikisema niikumbuke mingine au kuitafuta mingine nitapata mingi tu.
 
Kwa hiyo hiyo unasema mifano niliyotoa ya Newcastle, Man U na Liverpool haikutokea au unataka kusema nini? Na hii ni mifano ya haraka tu ila najua nikisema niikumbuke mingine au kuitafuta mingine nitapata mingi tu.
Umetoa mifano ya Newcastle, Man Utd na Liverpool ya kususia kuingia uwanjani....... ?

Kweli unakumbuka ukicho kiandika..........

Ninacho kikumbuka ni hiki ulicho kiandika ww.

"Nimekujliza hayo maandanano ya Brazil ya wapi huja ni jibu,tena huko Brazil watu ni machizi wa mpira."

Hulijui taifa la Brazil linavyo penda mpira timu zao, kule kuna machizi na wendawazimu wa soka.
 
Umetoa mifano ya Newcastle, Man Utd na Liverpool ya kususia kuingia uwanjani....... ?

Kweli unakumbuka ukicho kiandika..........
Nilikwambia toka hapo juu, tatizo lako hausomi mada unarukia tu kwa mihemko. Pitia post za juu hapo na ukaniquote kabisa ila ukakimbilia kujibu halafu unanihoji kama nakumbuka nilichoandika? Hata mada hii haukusoma post ya kwanza kujua hasa inahusu nini ndiyo maana unaongelea habari za mafataki, wewe umeona kwenye kichwa cha habari timu yako imesemwa umerukia kuitetea. Unanipotezea muda wangu.

Humu JF kuna watu kama watatu nilishawamark, huwa mnapenda kubisha hata kama mnachobisha hakieleweki. Najua hapa tunaweza kukaa hadi asubuhi ili mradi tu usionekane umeshindwa kutetea hoja yako.
 
Wewe ndiye usomi kabisa nilicho kipost kwenye comment yangu ya kwanza unarukaruka kama bisi. Sasa ureply vip comment ya kwanza ,hivi ulikielewa nilicho kicoment na hoja yangu niliandika based on kitu gani au ndio unapayuka kama umekunywa maji ya mtaroni.

Refer comment namba tatu na namba saba halafu ujione ulivyo hujielewi. Umetoa hoja iliyojaa chai,ila kuna clip inapingana na ulicho kileta so mimi nimechagua upande wa hiyo clip maana ndio reality.
 
Ulimwengu umebadilika kuna camera za kisasa kbs za kutambua wahalifu, waliofanya uharibifu ni mashabiki sio timu, watambuliwe wachukuliwe hatua, tusitake kuua mhakifu kwa kupiga kivuli chake.
 
Aiseee! Uzi ni wangu halafu unanihoji kama nakumbuka nilichoandika? Ndiyo maana nakushangaa unakazania mambo ambayo hata hayahusiani na mada husika tena kwa hoja zisizokuwa na kichwa wala mguu. Eti unashangaa watu kususa. Unadhani protests na boycott zimeanzia wapi, wazungu waweze kususa kwenda makazini washindwe kususa mambo ya mipira? Unajidai unawajua wazungu wakati unawaona tu kwenye TV
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…