Yanga ikiingia robo fainali inaweza kuipaisha Simba katika rank za CAF na FIFA

"Theory" yangu inaenda kutimia na nawashukuru "wazee" walioona maono yangu haya yanafaa na kuyafanyia kazi kwa manufaa ya taifa.
Wewe ni usiyejua mpira na uliyekosa akili ya mpira Yanga wamefanya kwa jitihada zao na kwa malengo yao wala hakuna kikao kilichokalika baina ya Simba na Yanga kushirikiana katika hili. Acha ujinga basi badilika. Na kingine ni kwamba Es Tunis kaongeza point 3 wakati timu yako imepata point moja.
Hao Belouizdad mpaka sasa mmepunguza point moja tu kwake.
 
Huu unaweza kuwa uzi wangu wa mwisho kwa mwaka 2023 na nataka nimalize mwaka kwa ujumbe chanya. Wenye akili zao watausoma na yale watakayoona ni mazuri wataenda kuyafanyia kazi.

Yanga na Simba bado wako kwenye mbio za kufuzu kwenda katika robo fainali ya klabu bingwa ya Afrika. Yanga hajacheza robo fainali ya Klabu Bingwa toka mwaka 1970. Matokeo ya mechi ya kiporo ya CR Belouizdad vs Al Ahly yatatoa mwanga wa ugumu iliyonayo ili kusonga mbele. Vyovyote itakavyokuwa, CRB itakuja kucheza na Yanga ikiwa inahitaji matokeo kwa njia yoyote ile.

Wakati huo huo, kama mnakumbuka mwaka 2018, Mo Dewji aliwahi kutamka kwamba nia na ndoto yake ni kuiona Simba ikiwa moja ya timu 10 bora barani Afrika, malengo ambayo yameshafikiwa katika rank zote za CAF na FIFA.

Ukiangalia rank za CAF na FIFA (rank ya CAF ya miaka 5 na rank ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa vilabu), CRB akitolewa na Yanga hatua hii ya makundi halafu Simba akashinda mechi zake 2 za makundi na akasogea walau nusu fainali, kwa kuzingatia point itakazokuwa imekusanya Simba itapanda katika rank zote za CAF na FIFA hadi nafasi ya 5 kwa ubora Afrika. Kuna uwezekano mkubwa wa Simba kukutana na TP Mazembe hatua ya robo fainali, timu ambayo Simba inaimudu.

Kwa manufaa mapana ya mpira wetu, unaona wazee wa Kariakoo wakikaa chini na kusuka mbinu za pamoja kwa faida ya pande zote mbili? Kufungwa kwa CRB dhidi ya Al Ahly na Yanga inaweza isiwe sababu ya huzuni sana kwa wanasimba na badala yake inaweza kuwa ni chanzo cha furaha kwetu kama Simba itacheza mechi zake zinazofuata vizuri na kuwa timu ya 5 kwa ubora Africa. Na hauwezi jua, tunaweza kukutana nusu fainali tukamkanda uto vizuri tu kiutu uzima.

Niliwahi kuuliza nini kinazuia timu hizi mbili kushirikiana?
Kila mtu ashinde mechi zake hamna kusafiria nyota
 
"Theory" yangu inaenda kutimia na nawashukuru "wazee" walioona maono yangu haya yanafaa na kuyafanyia kazi kwa manufaa ya taifa.
Kwahiyo umekaa hapo ukaamini kuwa Simba na Yanga wakakaa chini kushirikiana kumfunga Belouizdad? Basi una matatizo makubwa sana kichwani aisee
 
Huu unaweza kuwa uzi wangu wa mwisho kwa mwaka 2023 na nataka nimalize mwaka kwa ujumbe chanya. Wenye akili zao watausoma na yale watakayoona ni mazuri wataenda kuyafanyia kazi.

Yanga na Simba bado wako kwenye mbio za kufuzu kwenda katika robo fainali ya klabu bingwa ya Afrika. Yanga hajacheza robo fainali ya Klabu Bingwa toka mwaka 1970. Matokeo ya mechi ya kiporo ya CR Belouizdad vs Al Ahly yatatoa mwanga wa ugumu iliyonayo ili kusonga mbele. Vyovyote itakavyokuwa, CRB itakuja kucheza na Yanga ikiwa inahitaji matokeo kwa njia yoyote ile.

Wakati huo huo, kama mnakumbuka mwaka 2018, Mo Dewji aliwahi kutamka kwamba nia na ndoto yake ni kuiona Simba ikiwa moja ya timu 10 bora barani Afrika, malengo ambayo yameshafikiwa katika rank zote za CAF na FIFA.

Ukiangalia rank za CAF na FIFA (rank ya CAF ya miaka 5 na rank ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa vilabu), CRB akitolewa na Yanga hatua hii ya makundi halafu Simba akashinda mechi zake 2 za makundi na akasogea walau nusu fainali, kwa kuzingatia point itakazokuwa imekusanya Simba itapanda katika rank zote za CAF na FIFA hadi nafasi ya 5 kwa ubora Afrika. Kuna uwezekano mkubwa wa Simba kukutana na TP Mazembe hatua ya robo fainali, timu ambayo Simba inaimudu.

Kwa manufaa mapana ya mpira wetu, unaona wazee wa Kariakoo wakikaa chini na kusuka mbinu za pamoja kwa faida ya pande zote mbili? Kufungwa kwa CRB dhidi ya Al Ahly na Yanga inaweza isiwe sababu ya huzuni sana kwa wanasimba na badala yake inaweza kuwa ni chanzo cha furaha kwetu kama Simba itacheza mechi zake zinazofuata vizuri na kuwa timu ya 5 kwa ubora Africa. Na hauwezi jua, tunaweza kukutana nusu fainali tukamkanda uto vizuri tu kiutu uzima.

Niliwahi kuuliza nini kinazuia timu hizi mbili kushirikiana?
Halafu cha ajabu uzi mzima Unazungumzia tu Belouizdad, utafikiri ndio timu pekee ambayo ipo juu ya Simba, umewaacha kuzungumzia Petro Atletico ambao ndio kidogo mmelingana point na kwa bahati mbaya kaishafuzu robo fainali. Umeacha kuzungumzia Es Tunis ambao ndio kwa Simba ndio wanamlima mkubwa wa point (point 75 vs point 45) naishia hapo hapo sitaki kwenda juu huko kwa Mamelod.

Sasa unakazana kuandika mawazo ya kijinga tu hata kufikiria wala hufikirii kwahiyo tokea ucheze je kwa huyo Belouizdad unayemuwazia kichwani kwako umepunguza point ngapi kwake?
 
Back
Top Bottom