Hapo ndio utaona hawa watu wameamua kushea akili ndogo na mashabiki wao. Yaani SP hawana haki lakini waliwa consult. Wanasema wakataka waweke SPLivescore, maana yake nini? Maana yake walijua ana haki ndio maana walituma maombi. Lakini hawaonyeshi baada ya kushindwana kwenye Visit Tz ilikuwaje wakaibuka na nembo nyingine. Hawaonyeshi kama walifikia muafaka wowote na mtu mwenye haki.
SP walitaka Yanga ionyeshe ushahidi wa Livescore kukataliwa. Yanga hawajafafanua hiyo.
Blah blah za kutosha eti SP kikanuni hairuhusiwi na CAF. Hayo maelezo yana tija gani wakati sio sehemu ya malalamiko ya SP. SP inasema inajua yote hayo ila kwa nini mmeweka main sponsor mpya bila ridhaa yao?
Mashabiki wanachoshabikia ni taarifa tu lakini yaliyomo kwenye taarifa hawajui