Yanga inasumbuliwa na timu iliyoshika nafasi ya pili ligi ya Djibouti

Yanga inasumbuliwa na timu iliyoshika nafasi ya pili ligi ya Djibouti

Yanga kusumbuliwa na timu zinazoshika nafasi ya pili ni kitu cha kawaida, maana hata Simba ambayo ndiye bingwa wa kombe la ngao ya jamii wamesumbuana hadi kwenye matuta. Tukumbuke tu hii timu ndio inayojinadi ipo nafasi ya tisa kwa ubora na pia ndio mwakilishi wa super league lakini wamepelekana na Yanga hadi matuta.
Haya mchambuzi endelea na uchambuzi wako nilikuwa nakukumbisha tu mpira hauna formula
Muulize dodoma jiji yupo nafasi ya ngapi kwenye rank ya fifa?? Asas djibout kamzidi mbali sana dodoma jiji....enh mbona yy hajamfunga magoli 10 dodoma...kashinda mbili?
 
Hili ni jambo la kusikitisha sana na najua wanayanga wengi limewafedhehesha.

ASAS Djibouti au kwa jina lingine "AS Ali Sabieh" ni timu ambayo msimu uliopita ilimaliza nafasi ya pili katika ligi ndogo na dhaifu ya Djibouti lakini jana imeisumbua sana Yanga. Ingekuwa na mshambuliaji mmoja wa kati mzuri, kuna watu jana wangelia.

ASAS pia walinyimwa penati ya wazi baada ya Diara kupigwa chenga akaamua kumsukumia mbali mshambuliaji wa ASAS tena mbele ya refa. Yule jamaa anayeripoti matukio ya mpira na kupeleka UN na Interpol asilisahau na hili tukio.

Kwa kumalizia Yanga isiseme ilikuwa ugenini wakati tiketi za mechi iliuza yenyewe na hata bei ya tiketi inaonyesha ilipangwa na Yanga, umbali kutoka Chamazi hadi Kimbiji ni mfupi kuliko wao kutoka Chamazi kurudi kwao. Pia sitashangaa kama hata malazi mliwapa nyie. Najua mechi ya pili mtajipigia tu hao wasomali ila round ijayo hamtoboi.
Umelogwa
 
Back
Top Bottom