Mpira haupo hivyo mkuu, je Konikon Kombole, Birigimana, n.k ambao walilazimika kivunjiwa mikataba walifanya vizuri? Kufanya vizuri kwa Yanga hakuna uhusiano na Nabi bali ni kazi nzuri ya watu wa scouting kuleta benchi la ufundi lililo sahihi na replacement zilizo sahihi. Anaondoka Nabi, Mayele, Bangala, Djuma Shaban lakini hauoni pengo. Kama Nabi ndio sababu basi turejee kwa alichokifanya Nabi alipoenda Rabat. Rabati ilitengenezwa na mtangulizi wake na ikawa timu tishio Morocco na ikabeba taji la ligi kuu lakini huyo Nabi kashindwa kuendeleza mafanikio yale badala yake klabu bingwa kstolews hatua ya awali, ligi kuu kakosa na FA kakosa. Usidhani ni jambo rahisi kuendeleza ubora wa timu hata mtangulizi wako amekuanzishia.