Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tutajie wachezaji wa waliokuwa wakitamba na kikosi cha Nabi wakati ule ambao hata sasa nado wapo? Maana hata Aziz Ki alikuwa siyo chaguo la kwanza la NabiMchukue mchezaji mmoja yoyote muweke pale kwa wanabatiki lazima afanye vizuri sababu Yanga kupitia Nabi ilitengeneza timu ya kikosi cha dhahabu ambacho kiko kwenye peak kwa sasa. Huu ni wakati wao.
Simba ina kikosi kipya, ikiwa kocha atakuwa smart kuunganisha timu na wachezaji wakajituma na mabadiliko ya kuondoa wasiofaa yakafanyika kwa haraka na kuboresha kikosi na yenyewe ikifika kwenye peak itasumbua muda mrefu mno sababu ya umri wa kikosi.
Try Again amesema kile kikosi cha msimu huu thamani yake ni bil 7,kwa hiyo kuweni wapole, wapeni muda.Hata kusalimia sisalimii kifua kimenibana kwa uchungu ,hivi hawa Utopolo wanapata wapi wachezaji jamani haiwezekani kila mchezaji wakichukua anakua moto yaani hawakosei na kama wakikosea basi kidogo sana.
Mfano nimzungumzie namba 3 yao ,yule Boka dah lile jamaa refu,lina control,spidi na lina maamuzi sahihi na linafanya pressing muda wote.
Yanga hii ya sasa ubora walionao hata Simba ile bora ya miaka 4 haijafikia hata nusu ya ubora huu,ndo maana hatukuwahi kuwanyanyasa bado walitufunga pia. Naweza sema sasa ubora wao wako sawa na Al ahly na nina uhakika kwa sasa Yanga ndo timu ambayo magiant wa afrika wote wanaiohofia kukutana nayo kwa sasa. Spirit ya ushindi ya ushindi walio nayo ni hatari sana kwa afya ya ligi yetu itageuka ligi ya kipuuzi sasa.
Soma Pia: Sibishani tena kuhusu ubora wa Yanga Africans, nimekubali yaishe
Angalia MVP wao waliomchukua msimu juzi kiwango chake halafu fananisha na MVP wetu tuliomchukua sisi msimu jana dah yaani yaaani.
Hongera mtani mmejua kutonyoosha🙌🙌
Moyo unaniuma sana😡 ,#UBAYA UBWELA
Wewe Kaka acha tu ,yaani Kuna muda nilijikuta nashangilia goli laoNoma sana wale jamaa jana niliumia kinoma jinsi walivyonyanyasa tegemeo letu.
Ishu sio kizazi ishu ni benchi bora la ufundi, kwani Pep ni kocha wa kawaida? Kizazi cha dhahabu bila kuwa na benchi zuri la ufundi wachezaji wanashuka viwango. Swala la msingi ni kuwa na management iliyo bora.Yanga naifananisha na Barca ya Frank Rijkaard akaja kurithiwa na Pep. Kile kizazi Pep anamtoa mtu kama Toure na pengo lake halionekani, kilikuwa kizazi bora kabisa na kikakaa kwenye peak kwa muda mrefu mpaka kupotea.
Kwa hiyo jina la timu ndio linawafanya wacheze vizuri na sio vipaji vyao?Hukunielewa. Nilisema mchezaji hata wa kawaida akiwekwa katikati ya wanaofanya vizuri uwezekano wa yeye kufanya vizuri ni mkubwa.
Upo sawa.Ishu sio kizazi ishu ni benchi bora la ufundi, kwani Pep ni kocha wa kawaida? Kizazi cha dhahabu bila kuwa na benchi zuri la ufundi wachezaji wanashuka viwango. Swala la msingi ni kuwa na management iliyo bora.
Yanga ni neno lenye sifa ya jina?Kwa hiyo jina la timu ndio linawafanya wacheze vizuri na sio vipaji vyao?