Yanga inatoa wapi wachezaji? Inaniuma sana aisee, jana nimeshindwa kulala

Asante kwa kuliona hili.. mimi nimeshangaa sana Simba kubaki na Kapombe na Hussein msimu huu.. wale jamaa wamechoka.. tatizo letu tunaendekeza siasa kwenye kazi. Kikosi hakija tulia kabisa.
 
Asante kwa kuliona hili.. mimi nimeshangaa sana Simba kubaki na Kapombe na Hussein msimu huu.. wale jamaa wamechoka.. tatizo letu tunaendekeza siasa kwenye kazi. Kikosi hakija tulia kabisa.
Ilikua ngumu kuondoa wachezaji waandamizi wote kwa wakati mmoja japo nilishangaa kumuondoa Mwenda na kumuacha kapombe wakati ndo ulikua wakati mzuri kapombe asepe mwenda abaki apambane na kijiri na uzuri mwenda kuna muda anaweza kucheza hata left back.
 
Mkuu unataka kusema ukimchukua Kapombe, Mzamiru, Tshabalala, Mukwala watachukua namba mbele ya Aucho, Boka, Yao na Dube kisa tu Yanga ipo ktk ubora wao?

Sidhani, Yanga imefanya vyema ktk usajili. Wachezaji wao ni watu wenye uwezo haswa uwanjani, ni talented na well trained.
 
Mpira haupo hivyo mkuu, je Konikon Kombole, Birigimana, n.k ambao walilazimika kivunjiwa mikataba walifanya vizuri? Kufanya vizuri kwa Yanga hakuna uhusiano na Nabi bali ni kazi nzuri ya watu wa scouting kuleta benchi la ufundi lililo sahihi na replacement zilizo sahihi. Anaondoka Nabi, Mayele, Bangala, Djuma Shaban lakini hauoni pengo. Kama Nabi ndio sababu basi turejee kwa alichokifanya Nabi alipoenda Rabat. Rabati ilitengenezwa na mtangulizi wake na ikawa timu tishio Morocco na ikabeba taji la ligi kuu lakini huyo Nabi kashindwa kuendeleza mafanikio yale badala yake klabu bingwa ikatolewa hatua ya awali, ligi kuu kakosa na FA kakosa. Usidhani ni jambo rahisi kuendeleza ubora wa timu hata kama mtangulizi wako amekuanzishia.
 
Muda ni kitu kizuri sana,watagongwa na IHEFU halafu mtataka kuilaumu TFF kama ilivyo ada kwenu
 
Hukunielewa. Nilisema mchezaji hata wa kawaida akiwekwa katikati ya wanaofanya vizuri uwezekano wa yeye kufanya vizuri ni mkubwa.
 
Peak ipi karibia kila msimu simba wanaanza upya
 
Yanga naifananisha na Barca ya Frank Rijkaard akaja kurithiwa na Pep. Kile kizazi Pep anamtoa mtu kama Toure na pengo lake halionekani, kilikuwa kizazi bora kabisa na kikakaa kwenye peak kwa muda mrefu mpaka kupotea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…