Yanga komaeni kushinda mechi zenu: Hii ndoto ya kutaka Al Ahly amfunge CRB ugenini ni ndoto ya bafuni wakiwa wanaoga!!

Kwamba ndo uto atashinda gemu zake mbili zilizobaki
Ndugu mbumbumbu pumzika, Yanga isikufanye ukose usingizi.
Nakukumbusha Juzi 19/12/2023 Pyramids amefungwa kwao wakati alipata sare kule south.
Upe mpira heshima yake
 
Mmeanza Tena Wana Utopolo kuongea baada ya kumfunga medeama ila kuwa shabiki yanga ni mtihan sana
 
Kwa michezo iliyobaki Yanga akijitahidi ataongeza point 3 tu toka kwa Belouzdad na kufikisha 8.

Wakati huo Belouzdad atakuwa na point 10 , tatu kutoka kwa vibonde mediama , tatu toka kwa aly Ahly.

Aly Ahly atakuwa na point 11 , tatu toka kwa kibonde mediama , tatu tena toka kwa Yanga .
Hivyo yanga ataaga mashindano kwa stahili hiyo na kurudi Dar kuanza Kazi yake ya kupokea wageni wa simba airport.
 
Hii comment naitunza...
 
Umeni quote je unajua kilichokuwa kinajadiliwa kuhusu comment yangu au umeidakia tu juu juu? Nimesema hivi " Yanga kama atashinda michezo yake yote iliyobakia, hata kuwa na sababu ya kumuombea fulani afungwe na fulani bali atakuwa amefuzu. Kuna mtu akanikatalia, akasema hata Yanga akishinda mechi zake zote bado kufuzu kwake kutategemea na matokeo ya timu zingine. Ndipo nikampa idadi ya point kama ikitokea Yanga atashinda michezo yote iliyosalia.
 
Kushinda mechi zake tu haitoshi
Lazima waombe CRB afungwe na Al Ahly
Simba ndio wanatakiwa kushinda mechi zao bila kuangalia matokeo ya wengine
Yanga akishinda Mechi zake anafuzu haijalishi wenzake matokeo yamekuwaje.
 
Yanga anatakiwa ashinde michezo iliyobaki yote anapita. Atakuwa na p11.
 
Kama Medeama ni kibonde alimfungaje CRB?
 
Usipende kutumia neno "hawezi" kwenye mchezo wa soka. Namjua uliamini Jwaneng Galaxy "hawezi" kumfunga Wydad pale Morocco.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…