SI KWELI Yanga kucheza na As Vita Chamazi Complex, Agosti 6, 2023 siku ya Simba Day

SI KWELI Yanga kucheza na As Vita Chamazi Complex, Agosti 6, 2023 siku ya Simba Day

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Yanga nao wamekuja na mechi dhidi ya As Vita siku ya Simba day jumapili hii. Wanasema ukimwaga ugali wao wanamwaga mboga

59F9E6BE-7E66-4793-8B00-765CCF618052.jpeg
 
Tunachokijua
Klabu ya Simba itafanya tamasha lake la Simba Day Agosti 6, 2023 katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni Rasmi.

Aidha, Simba SC itacheza na timu ya Power Dynamos ya Zambia.

Katika kuelekea siku hii, kumekuwepo na uvumi kwenye mitandao unaosema mahasimu wao, timu ya Yanga SC itacheza na AS Vita Club, timu kutoka Kongo siku hiyohiyo hali iliyoamsha hisia tofauti miongoni mwa wadau wa soka.

JamiiForums imezungumza na Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ili kupata uthibitisho wa taarifa hii. Amesema

“Kocha wetu anahitaji mechi mbili kabla ya Ngao ya Jamii, kuna uwezekano mechi moja ikachezwa asubuhi nyingine jioni au ratiba inaweza kuwa tofauti na hivyo.

“Kuhusu kucheza na AS Vita hawapo kwenye ratiba lakini kwa kuwa Benchi la Ufundi linahitaji mechi mbili kama nilivyosema lolote linaweza kutokea.”


Hivyo, kutokana na ufafanuzi huu wa Afisa Habari wa Yanga picha inayosambaa kuonesha Yanga ina mchezo wa kirafiki siku ya Jumapili ni ya uzushi.

Uzushi huu umeibuka siku kadhaa tangu Yanga SC ifanye tamasha lake maarufu kama Siku ya Mwananchi Julai 22, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine, ilicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kaizer Chief kutoka Afrika Kusini na kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0.
Sidhani kama hili litazuia mashabiki wa Yanga wasiende kwa Mkapa. Wanaenda kuaibika tena. Watashindwa kuujaza hata uwanja wa Azam maskini ya M.....

Yaani uache kwenda kumuangalia Ngoma, Onana, Miq uende kumuangalia Skudu?
 
Hatari siku hiyo tv zitang'aa ila friendly trh 6 wakati trh 9 game ngumu na Azam so baada ya game tunaondoka kuelekea Tanga!?
 
Hii sio kweli
Young Africans ni timu kubwa kwenye hizi propaganda uchwara tushatoka
Hatuwezi kuwaza makolo
Sisi mipango yetu mechi ya tanga trh 9
 
USIWE UNAWEKA VITU AMBAVYO HUVIJUI.

yanga Wana Official platforms ZAO za kutoa habari, Hiyo habari yako umeitoa wapi??????

Unajisikiaje kutoa taarifa isiyo na Ukweli.
Dhambi nyingine mnazichuma kwa vitu vidogo kama mpila zisizo na faida hata kidogo.

ACHA UTOTO.

MUOGOPE SANA MUNGU WAKO KIJANA.
JEHANAMU IPO.

MUNGU AKUKEMEE
 
Club ya yanga imepanga kucheza mechi ya kirafiki ya As Vitar tarehe 6.8 siku ambayo ni kilele cha simba day.Uamuzi huo umepokelewa hisia tofauti na wadau wa michezo Nchini
IMG_4121.png
 
Haina shida..uwanja wa Mkapa siku ya Wananchi ulitakiwa ujazwe na mashabiki wa Utopolo na hivyo hivyo siku ya Simba uwanja wa Mkapa unatakiwa ujazwe na mashabiki wa Simba...Hivyo, hata hao Utopolo watakuwa na hiyo mechi bado Simba wataujaza uwanja na hakuna athari yeyote.
 
USIWE UNAWEKA VITU AMBAVYO HUVIJUI.

yanga Wana Official platforms ZAO za kutoa habari, Hiyo habari yako umeitoa wapi??????

Unajisikiaje kutoa taarifa isiyo na Ukweli.
Dhambi nyingine mnazichuma kwa vitu vidogo kama mpila zisizo na faida hata kidogo.

ACHA UTOTO.

MUOGOPE SANA MUNGU WAKO KIJANA.
JEHANAMU IPO.

MUNGU AKUKEMEE
 
Back
Top Bottom