SI KWELI Yanga kucheza na As Vita Chamazi Complex, Agosti 6, 2023 siku ya Simba Day

SI KWELI Yanga kucheza na As Vita Chamazi Complex, Agosti 6, 2023 siku ya Simba Day

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Yanga nao wamekuja na mechi dhidi ya As Vita siku ya Simba day jumapili hii. Wanasema ukimwaga ugali wao wanamwaga mboga

59F9E6BE-7E66-4793-8B00-765CCF618052.jpeg
 
Tunachokijua
Klabu ya Simba itafanya tamasha lake la Simba Day Agosti 6, 2023 katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni Rasmi.

Aidha, Simba SC itacheza na timu ya Power Dynamos ya Zambia.

Katika kuelekea siku hii, kumekuwepo na uvumi kwenye mitandao unaosema mahasimu wao, timu ya Yanga SC itacheza na AS Vita Club, timu kutoka Kongo siku hiyohiyo hali iliyoamsha hisia tofauti miongoni mwa wadau wa soka.

JamiiForums imezungumza na Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ili kupata uthibitisho wa taarifa hii. Amesema

“Kocha wetu anahitaji mechi mbili kabla ya Ngao ya Jamii, kuna uwezekano mechi moja ikachezwa asubuhi nyingine jioni au ratiba inaweza kuwa tofauti na hivyo.

“Kuhusu kucheza na AS Vita hawapo kwenye ratiba lakini kwa kuwa Benchi la Ufundi linahitaji mechi mbili kama nilivyosema lolote linaweza kutokea.”


Hivyo, kutokana na ufafanuzi huu wa Afisa Habari wa Yanga picha inayosambaa kuonesha Yanga ina mchezo wa kirafiki siku ya Jumapili ni ya uzushi.

Uzushi huu umeibuka siku kadhaa tangu Yanga SC ifanye tamasha lake maarufu kama Siku ya Mwananchi Julai 22, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine, ilicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kaizer Chief kutoka Afrika Kusini na kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0.
HIYO NI FAKE NEWZ.

HABARI YA UONGO.

URONGO MTUPU

UPUMBAVU +UJINGA.
 
USIWE UNAWEKA VITU AMBAVYO HUVIJUI.

yanga Wana Official platforms ZAO za kutoa habari, Hiyo habari yako umeitoa wapi??????

Unajisikiaje kutoa taarifa isiyo na Ukweli.
Dhambi nyingine mnazichuma kwa vitu vidogo kama mpila zisizo na faida hata kidogo.

ACHA UTOTO.

MUOGOPE SANA MUNGU WAKO KIJANA.
JEHANAMU IPO.

MUNGU AKUKEMEE
Hamna jehanamu
 
Umepokelewa kwa hisia zipi hizo,
Zibainishe,

#Wananchi tukutane Azam Complex tarehe 6.8 Friendly Match [emoji169][emoji172][emoji3060][emoji3060][emoji3060][emoji3060]
Umenifanya nicheke Kwa nguvu ..
Anyway mwananchi mmoja ajitokeze nimkatie tiketi tukaujaze uwanja wa chamazi [emoji28]
 
Baada ya Yanga SC kwa Makusudi kabisa kuandaa Mechi yake ya Kirafiki dhidi ya AS Vita Club Siku ya Simba Day tarehe 6 August, 2023 katika Uwanja wa Chamazi ili Kuliteka Tamasha la Simba Day na Kuififisha Siku yenyewe Klabu ya Simba imeamua kujibu Mapigo na kuwaonyesha Yanga SC kuwa kwa Tanzania nzima Timu Bingwa wa Umafia na Jeuri ya Fedha ni Simba Sports Club pekee.

Taarifa ikufikie kutoka kwa Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally aliyeko mubashara (live) sasa 107.3MhZ U-live ( Uhai FM ) ni kwamba Klabu ya Simba imeamua Kukodi Viwanja vingine Viwili vya Uhuru na Chamazi ambako huko kutafungwa Screen Kubwa ili Mashabiki waingie na Kuangalia Simba Day.

Hivyo kama kuna Timu ya Roho Mbaya Wendawazimu FC ilipanga Kucheza na AS Vita Club Mechi ya Kirafiki waje huku Kawe Uwanja wa bure wa Tanganyika Packers wacheze au waende Msoga Stadiun kwa anayewapa Jeuri wakacheze pale.

Timu ya Tajiri Mo ina Jeuri ya Fedha.
 
Unashindana na kivuli?, Tiketi za aftatutatu ndio kuwe na kiburi Cha pesa?. Kwani haiwezekani Simba kuwa na siku yenu ya kubleed na yanga kucheza mechi ya kirafiki?
 
Jeuri siku zote haikupeleki mahali pema asa mambo yote haya ambayo simba anafanya anapata faida gani kwa kukodisha viwanja viwili ili kuwakomoa yanga jichungeni msije mkalia msimu huuu na mbeleni tena halafu kisha mna mlalamikia mungu kuwa hafanyi haki kumbe wenyewe mdomo unawaponza na matendo yenu kwa namna hii mtasota sana kutafuta nusu fainali na kuchukua makombe yote ya ligi hata mkiwa mna kikosi gani cha muhimu ni nidhamu
 
Jirekebisheni kuanzia mashabiki wa simba mpaka viongozi ndipo mtakapo ona mafanikio ya klabu ila mkiendelea hivi mungu siku zote hayupo pamoja na watu wa aina hiii
 
Kazi inaanzia ngao ya hisani Simba na Azam huu msimu utawaacha mkiwa na majonzi sana
 
Back
Top Bottom