SI KWELI Yanga kucheza na As Vita Chamazi Complex, Agosti 6, 2023 siku ya Simba Day

SI KWELI Yanga kucheza na As Vita Chamazi Complex, Agosti 6, 2023 siku ya Simba Day

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Yanga nao wamekuja na mechi dhidi ya As Vita siku ya Simba day jumapili hii. Wanasema ukimwaga ugali wao wanamwaga mboga

59F9E6BE-7E66-4793-8B00-765CCF618052.jpeg
 
Tunachokijua
Klabu ya Simba itafanya tamasha lake la Simba Day Agosti 6, 2023 katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni Rasmi.

Aidha, Simba SC itacheza na timu ya Power Dynamos ya Zambia.

Katika kuelekea siku hii, kumekuwepo na uvumi kwenye mitandao unaosema mahasimu wao, timu ya Yanga SC itacheza na AS Vita Club, timu kutoka Kongo siku hiyohiyo hali iliyoamsha hisia tofauti miongoni mwa wadau wa soka.

JamiiForums imezungumza na Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe ili kupata uthibitisho wa taarifa hii. Amesema

“Kocha wetu anahitaji mechi mbili kabla ya Ngao ya Jamii, kuna uwezekano mechi moja ikachezwa asubuhi nyingine jioni au ratiba inaweza kuwa tofauti na hivyo.

“Kuhusu kucheza na AS Vita hawapo kwenye ratiba lakini kwa kuwa Benchi la Ufundi linahitaji mechi mbili kama nilivyosema lolote linaweza kutokea.”


Hivyo, kutokana na ufafanuzi huu wa Afisa Habari wa Yanga picha inayosambaa kuonesha Yanga ina mchezo wa kirafiki siku ya Jumapili ni ya uzushi.

Uzushi huu umeibuka siku kadhaa tangu Yanga SC ifanye tamasha lake maarufu kama Siku ya Mwananchi Julai 22, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine, ilicheza mchezo wa kirafiki na timu ya Kaizer Chief kutoka Afrika Kusini na kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa 0.
Jeuri siku zote haikupeleki mahali pema asa mambo yote haya ambayo simba anafanya anapata faida gani kwa kukodisha viwanja viwili ili kuwakomoa yanga jichungeni...
Fedha ni zako na Yanga SC yako au ni za Simba SC yetu na Tajiri yetu Mo Dewji? Zinakuuma nini? Vipi Magodoro yenu yenye Kunguni ya MSG yameanza Kununulika kwani yalianza Kudoda Masokoni.
 
Klabu ya Simba imeamua Kukodi Viwanja vingine Viwili vya Uhuru na Chamazi ambako huko kutafungwa Screen Kubwa ili Mashabiki waingie na Kuangalia Simba Day.

Mzee baba huu ni upotevu wa fedha tu, hiyo fedha ni bora hata ingetumika kufanya shughuli ya kijamii kwa watu wenye uhitaji...
 
Kama ni kweli Yanga walipanga kufanya huu upumbavu basi wanasikitisha sana kwa kukosa Moyo wa Kiuanamichezo na kuwaingiza wenzao gharama na usumbufu usio na ulazima. Hizi timu zinatakiwa zitoke huko soka la gizani na wajikite kwenye transformations walizo zianza
Nani kakuambia Tajiri Mo Dewji na Timu Tajiri ya Simba SC huwa wanaingizwa Gharama? Waonee Huruma Yanga SC ( Timu yako Mbovu mbovu ) na siyo yetu ya Simba SC sawa?
 
Kama Fedha hiyo siyo yako inakuuma nini? Simba SC imewahi Kukupigia hodi Kukuomba Msaada wa Fedha?

Acha Ubwege sawa?

Kama ambavyo wewe umeweka maoni mzee baba, hata sis wengine tuna mitazamo tofauti tofauti, ni mawazo tu...

😁
Genta vipi tena kamanda? si tulikubaliana hakuna kutoleana maneno haya
 
Wmetangaza kuandika kitabu cha historia na kuzindua makala halafu wanasema hii haijawahi kutokea. Kaduguda aliandika kitabu cha Simba miaka mingapi imeshapita sasa?
 
Ni ukweli kwamba yanga waliandaa mechi hii ya kirafiki,na ilikuwa ichezwe same day same place,ila kocha gamondi alivyoskia taatifa hizo akakataa katakata,sababu yake ikiwa ni kwamba wao watacheza na azam,kwenye ngao ya jamii,halafu nyie mnataka tucheze na vita tena pale pale kwa azam ,hamuoni kama tutauza silaha za kivita,jamaa akawaambia kama wanataka mechi basi wacheze na timu ya ndani tena iwe avic town,bila shabiki kushuhudia.

My take:HIVI VIONGOZI WA YANGA WANAWAZA KWA KUTUMIA NINI??MNAWEZAJE PELEKA MECHI CHAMAZI COMPLEX,AFU MNA MECHI NA HAO HAO AZAM KWENYE NGAO YA JAMII SIKU CHACHE TU..MNAFANYA HAYO KUMKOMOA TU SIMBA,AND SO WHAT??????
 
Back
Top Bottom