Yanga kwa sasa inafaidika nini na kumng'ang'ania Feitoto?

Umejibiwa swali lako vizur tu ila umeachagua kutoelewa kwa maana ulikuwa na majibu yako binafsi lakini unataka Yanga wakujibie unavyotaka wewe. Sio kila jambo ndani ya Club lazima lilete faida ya kifedha, bali kuna matukio yanatakiwa kufanywa kulinda taswira ya Club hata kwa kupata hasara. Kwa kutumia akili ndogo tu, unadhani Yanga wamekosea? Unaamua kuondoka kwenye Club kienyeji tu ulitaka Yanga wabariki huo ujinga kisa Fei ametaka hivyo? Yanga akiruhusu huu ujinga kuna siku Kambini atabaki Erick Johora tu na timu itakuwa imekufa rasmi.
Yanga inafahamu ipo kwenye vita, kila timu inataka mafanikio, ukiruhusu huu ujinga, timu pinzani zitakuja kukupoteza kupitia huu ujinga, Wapinzani wa Yanga kesho watkusanya Fedha kibao kuja kuwarubuni kina Mayele, Diara, Aziz Ki, Aucho, Job, Kubwana, Djuma, Sasa hapo ubingwa umeuuza kwa wapinzani wako kisa huruma kwa wajinga. Mjinga atajibiwa kijinga.
 
Tatizo Usimba na Uyanga (personal issues) unawasumbua,..yaani mchezaji hafiki mazoezi, hachezi mechi na analipwa stahiki zake zote. Yanga wanamtime tu usizani ni wapumbavu kiasi hicho.
 
Wakili Fatma kashafichua kuwa Mkataba wa Fei una mapungufu mengi yanayomruhusu kuwa huru. Na akiamua kuyafichua inaweza ikasababisha wachezaji wengine wa Yanga nao wakaanza kukagua haya mapungufu kama ya Fei.

Kamati imetumia busara sana kumuacha Fei aendelee kula ugali na Sukari. Akichoka kulamba sukari ya Dar aende na unga wake tu kule Kagera au Mtibwa, Sukari ataikuta kwa wingi.
 
Kama ashajua hayo mapungufu kwanini asitumie hayo mapungufu kumtetea fei? Aende cas akapate haki yake kama anaonewa, siyo analia na ttf wakati chombo cha haki kipo
 
Sababu za maana ndio zipi?
Huwa zinapimwaje?
Nani wa kuzipima hizo sababu kuwa zina maana ama la?

Swali linabakia pale pale, Yanga kwa sasa inafaidika nini na kuendelea kumng'ang'ania Feitoto?
Yanga wanasubiri aliyenyuma ya Fei Toto ajitokeze wapige pesa
 
Hizo akili ndo kitu YANGA wamekosa
Mchezaji mtoro unaendelea kumng'ang'ania wa nini?
Kwani Yanga ni klabu ya kufuga wachezaji watoro?
Kwanini uendelee kumlipa mshahara na marupuru mchezaji mtoro?
Mtoro anapaswa afukuzwe ili apoteze haki zake.
 
Kama ashajua hayo mapungufu kwanini asitumie hayo mapungufu kumtetea fei? Aende cas akapate haki yake kama anaonewa, siyo analia na ttf wakati chombo cha haki kipo
Wameshasema Wanasubiri barua rasmi (sio taarifa ya twiter) kisha wanaenda CAS.
 
Pale Brighton kuna kijana mmoja raia wa Ecuador anaitwa Moises Caicedo yupo moto kweli kweli kiasi kwamba dirisha dogo Club kubwa duniani zilituma offer za kumnunua. Kijana wa watu analipwa mshahara mdogo kabisa pale Brighton na kwa upole na hekima nyingi aliiomba hadharani Club yake imuuze ili akalipwe mshahara mkubwa atakako enda na vile vile Club ivune fedha nyingi. Dirisha dogo Brighton wamekataa offer nyingi sana wakitaka kulipwa £ 80 Milioni huku wao walimnunua chini ya £ 30 Million. Najaribu kupiga picha kijana huyu angekuwa Mtanzania hali ingekuwaje mtandaoni kwenye page za Brighton maana maisha yetu tulishazoea kuonewa huruma badala ya sheria na taratibu. Kwenye ligi za Ulaya wapo vijana wengi wanacheza Club ndogo na wanalipwa mishahara midogo vile vile lakini wanasubiri muda sahihi. Hatuoni vituko kama vya kijana wetu huyu.
 
Umemaliza.. Ningependa mtu afungue uzi kumhusu huyo jamaa ili watu wapate uelewa
 
Fatuma K amepata wapi access ya mikataba yote ya wachezaji wa Yanga?
 
Roho mbaya
 
Analipwa ili baadae afunguliwe kesi.
Ili kujenga kesi ni lazima uonyeshe kuwa juhudi zote kuwa wewe ulijitahidi kadri ya uwezo wako kuheshimu mkataba na kutaka maridhiano.
Baada ya hapo ni maumivu, na timu itakayotaka kumchukua itabidi iipe Yanga hela ndefu, au yeye atoe mfukoni mwake.
Matokeo yake anaweza kuwa mchezaji ambaye thamani yake ya kumsajili (awe na uwezo ama la) itakuwa hailipi.
 
Bado tu hujaagizia mbili, tatu hapo kwa Mtogole nimeshakulipia...[emoji119][emoji3]
 
Mijitu inabadili logo za watu kimakusudi kisa rangi ndio itaweza kuheshimu vipengele vya mkataba vya mchezaji?

Nb tff wanafanya wanayofanya ili kubalance wasionekane ni simba
Hujui chochote kaa kimya we Makolokolo/Mbumbumbu/Makelele/Malalamiko/Mikia/Manyaunyau/Ngada/Zuwena/Kolowizards/Kinyume nyume/Madunduka FC.....[emoji23]

Mbona ninyi Mbumbumbu hamkufata usahihi wa malipo ya pesa za Marehemu Mafisango, au unajitekenya na kucheka mwenyewe ukiwa umejikalia tu kama furushi la bangi hapo kwa Shemeji yako?
 
Mijitu inabadili logo za watu kimakusudi kisa rangi ndio itaweza kuheshimu vipengele vya mkataba vya mchezaji?

Nb tff wanafanya wanayofanya ili kubalance wasionekane ni simba
Ulivyo zumbukuku umejisahaulisha hata Dubai mliruhusiwa kwa mbeleko za wazi kabisa baada ya mechi yenu dhidi ya Mbeya City kuhairishwa kwa sababu za kipuuzi kabisa ilihali YANGA FC ilikataliwa ilipotoka kucheza michuano ya kimataifa (Shirikisho) Tunisia.

Endelea tu kukaza fuvu maana upumbavu ni kipaji.
 
Kwa sasa tumemfanya kama demo ili kuwafundisha mabush lawyer maana ya mikataba.
 
Kwani feitoto hajafuata mkataba?
Mkataba umeweka vigezo vya kuuvunja ni fei kulipa million 100 na mshahara wa miezi mitatu
Kuna utaratibu gani tena?
Bush lawyer, wajinga kama wewe ndio mmeharibu maisha ya Feisal.

Kwahiyo leo Chama akiwaingizia Benki pesa zao Simba kesho anaondoka?
 
Sikio halizidi kichwa.
 
Unaelewa lakini maana ya mkataba au unaandika tu usichokijua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…