Yanga kwa sasa inafaidika nini na kumng'ang'ania Feitoto?

Yanga kwa sasa inafaidika nini na kumng'ang'ania Feitoto?

Kwani feitoto hajafuata mkataba?
Mkataba umeweka vigezo vya kuuvunja ni fei kulipa million 100 na mshahara wa miezi mitatu
Kuna utaratibu gani tena?
Hio it's valid only with mutual agreement..
 
Watu mnajitoa ufahamu tu.

Hivi itakuwa ni ligi ya namna gani siku Aziz Ki, Mudathir, Mayele, Djuma, Chama, Moses Phiri etc wakiamua wote kwa pamoja kudai hawana furaha na wanataka kuvunja mkataba?

Yanga anachofanya sasa ni kwa manufaa ya Ligi ya Tanzania. Basically Yanga hawana tena mpango na Fei ila wanataka kuweka utaratibu ukae sawa kwa future reference
 
Kwa kadri Yanga wanavyoendelea kumng'ang'ania Feitoto maana yake wanapaswa kumlipa haki zote (ikiwemo mishahara na marupurupu yake) na wakati huo huo hawamtumii.

Na kadri mchezaji anapokuwa hachezi huwezi kuja kumuuza kwa thamani kubwa.

Swali, linabakia pale pale, nini mantiki ya Yanga kuendelea kumng'ang'ania Feitoto wakati haiwezi kumtumia tena?
Amka haraka kitandani uache kuota ndoto huku unaharibu godoro kwa mkojo kabla sijakubabua mkofi...[emoji87]
 
Hio it's valid only with mutual agreement..
According to you or according to the contract??
By definition a contract ni mutual agreement, sasa pale walikaa wakakubaliana mutually terms za kuterminate mkataba na wakasaini hizo conditions ambazo ni kulipa hyo hela na mshahara wa miez mi3...Unataka mutual agreement nyingine ipi tena? Au mpaka wewe uwepo?
 
Huenda kuna kitu sikifahamu au labda nimepitwa. Mchezaji Feitoto alishaamua kuachana na Yanga na akawaaga na mashabiki, lakini klabu yake ya Yanga imeendelea kumng'ang'ania lakini haiwezi kumtumia, haimchezeshi, haimwamini nk

Nini mantiki ya Yanga kuendelea kumng'ang'ania Feitoto?
Nasikia mnalazimisha apigwe faini, angalieni msije peleka hili suala kwenye kero za muungano, Fei kuna watu wapo nyuma yake wanamlisha matango pori nae anayala na kuyameza aende Yanga wazungumze kuliko kutumia njia haramu
 
Kwa kadri Yanga wanavyoendelea kumng'ang'ania Feitoto maana yake wanapaswa kumlipa haki zote (ikiwemo mishahara na marupurupu yake) na wakati huo huo hawamtumii.

Na kadri mchezaji anapokuwa hachezi huwezi kuja kumuuza kwa thamani kubwa.

Swali, linabakia pale pale, nini mantiki ya Yanga kuendelea kumng'ang'ania Feitoto wakati haiwezi kumtumia tena?
Alisaini mkataba na Inabidi atumike.. mkataba hauvunjwi kwa upande Mmoja kuamua lazma kuwe na makubaliano ya pande pande mbili... Sasa fei analazimisha kusiwepo mutual agreement...huyo staa wenu mwambieni afate taratibu za soka ,huku Tanzania atapotezwa kwenye ramani..walikuepo Kama yeye na pengine hata kumzidi Kwan sasa wako wapi...amuulize singano alirubuniwa na Azam hivohivo!!
 
Umejibiwa swali lako vizur tu ila umeachagua kutoelewa kwa maana ulikuwa na majibu yako binafsi lakini unataka Yanga wakujibie unavyotaka wewe. Sio kila jambo ndani ya Club lazima lilete faida ya kifedha, bali kuna matukio yanatakiwa kufanywa kulinda taswira ya Club hata kwa kupata hasara. Kwa kutumia akili ndogo tu, unadhani Yanga wamekosea? Unaamua kuondoka kwenye Club kienyeji tu ulitaka Yanga wabariki huo ujinga kisa Fei ametaka hivyo? Yanga akiruhusu huu ujinga kuna siku Kambini atabaki Erick Johora tu na timu itakuwa imekufa rasmi.
Yanga inafahamu ipo kwenye vita, kila timu inataka mafanikio, ukiruhusu huu ujinga, timu pinzani zitakuja kukupoteza kupitia huu ujinga, Wapinzani wa Yanga kesho watkusanya Fedha kibao kuja kuwarubuni kina Mayele, Diara, Aziz Ki, Aucho, Job, Kubwana, Djuma, Sasa hapo ubingwa umeuuza kwa wapinzani wako kisa huruma kwa wajinga. Mjinga atajibiwa kijinga.
Bado hujajibu swali la hoja iliyopo.
Suala lipo wazi kabisa, Feitoto hataki tena kuwepo Yanga, na Yanga haina tena mpango wa kumtumia kwenye mechi zake. Sasa wa nini kuendelea kumng'ang'ania?

Kama hoja ni kuwa iwe funzo kwa wachezaji wengine ndani ya Yanga, sasa mantiki ni nini ikiwa klabu itaendelea kukaa na wachezaji waliopoteza mapenzi na timu yao lakini kwa kuogopa kukomolewa kama Feitoto basi waendelee kubakia tu Yanga?
 
Mkataba unatakiwa useme hivyo, mkataba wa Feitoto umesema Feitoto anatakiwa kulipa around 100m ili kuvunja mkataba wake (na amezilipa tayari), issue ambayo Yanga wanasimamia ni kuwa, utaratibu wa kufikia hapo haukufuatwa na Feitoto. Sasa suala lilllopo hapa ni kuwa, ni vipi Yanga wanafaidika na Feitoto kwa sasa?
Hebu tuoneshe huo mkataba wa huyo fei jinga tuone hicho kipengele au unaropoka tu?
 
Nasikia mnalazimisha apigwe faini, angalieni msije peleka hili suala kwenye kero za muungano, Fei kuna watu wapo nyuma yake wanamlisha matango pori nae anayala na kuyameza aende Yanga wazungumze kuliko kutumia njia haramu
Wakati Feitoto anahamia Yanga, ni akina nani walikuwa nyuma yake wakimlisha matango pori?

Wakati Feitoto anakubali kuingia mkataba na Yanga wenye maslahi duni kwake , wakina nani walikuwa wanamlisha matango pori?

Kabla ya kufikiri kuwa Feitoto anashauriwa vibaya sasa, anza kutafakari pia nani walikuwa wanamshauri Feitoto hapo kabla.
 
Wakati anakuja Yanga hao wanaomrubuni leo hawakumuona viunga vya Mchambawima? Wakati anakuja Yanga kipato alichokuwa anapata kilikuwa kikubwa kuliko alikokuwa kwenye timu za Zenji
 
Alisaini mkataba na Inabidi atumike.. mkataba hauvunjwi kwa upande Mmoja kuamua lazma kuwe na makubaliano ya pande pande mbili... Sasa fei analazimisha kusiwepo mutual agreement...huyo staa wenu mwambieni afate taratibu za soka ,huku Tanzania atapotezwa kwenye ramani..walikuepo Kama yeye na pengine hata kumzidi Kwan sasa wako wapi...amuulize singano alirubuniwa na Azam hivohivo!!
Naona uko nje ya hoja.
Kinachoendelea sasa ni kuwa Feitoto hawezi tena kuichezea Yanga (haitaki na hana tena mapenzi nayo), na Yanga hawawezi tena kumtumia Feitoto (hawamuamini tena na wana chuki naye). Sasa katika hali hiyo, wengi tungetegemea Yanga wangefungua ukurasa mwingine wa kuachana na mchezaji huyo kwa hali yoyote ile.

Sasa nini mantiki ya Yanga kuendelea kumng'ang'ania mchezaji ambaye hana kazi yoyote kwao?
 
Bado hujajibu swali la hoja iliyopo.
Suala lipo wazi kabisa, Feitoto hataki tena kuwepo Yanga, na Yanga haina tena mpango wa kumtumia kwenye mechi zake. Sasa wa nini kuendelea kumng'ang'ania?

Kama hoja ni kuwa iwe funzo kwa wachezaji wengine ndani ya Yanga, sasa mantiki ni nini ikiwa klabu itaendelea kukaa na wachezaji waliopoteza mapenzi na timu yao lakini kwa kuogopa kukomolewa kama Feitoto basi waendelee kubakia tu Yanga?
Afuate taratibu tu za kuvunja mkataba...mkataba hauvunjwi Instagram kwa condition ya Feisal ilibidi kuwepo mutual agreement both sides
 
Naona uko nje ya hoja.
Kinachoendelea sasa ni kuwa Feitoto hawezi tena kuichezea Yanga (haitaki na hana tena mapenzi nayo), na Yanga hawawezi tena kumtumia Feitoto (hawamuamini tena na wana chuki naye). Sasa katika hali hiyo, wengi tungetegemea Yanga wangefungua ukurasa mwingine wa kuachana na mchezaji huyo kwa hali yoyote ile.

Sasa nini mantiki ya Yanga kuendelea kumng'ang'ania mchezaji ambaye hana kazi yoyote kwao?
Hilo liko Wazi eng hersi alishasema wanaomtaka mchezaji Feisal waje meza ya mazungumzo ,lkn mpaka sasa hamna kiongoz yoyote aliyejitokeza kumtaka Feisal , Feisal mwenyewe haoneshi kutaka mazungumzo ya pande mbili ...
 
Hili Jambo tukieleza Kisheria tunaonekana mashabiki wa Yanga. Lakini Hakuna popote duniani timu/Taasisi itaruhusu mchezaji/mwajiwake aache kazi anavyojisikia bila kufuata taratibu kisa tu kalipa hela ya kununuliwa au mshahara wa mwezi mmoja.
Sheria gani uliyojaribu kuelezea ukaonekana mshabiki wa Yanga?
 
Yanga ni taasisi mkuu.

Wanaendesha mambo yao kutokana na ethics na principles.

Ikitokea leo yanga wakalifanya swala la Fei toto kienyeji watajenga picha gani kwa mashabiki na wadau wengine wa michezo.

Ndio maana unaona kama Yanga wamekomaa vile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Taasisi inaweza kukosea pia

Na ndio maana kwenye ishu ya Haier raisi wa Club amekiri kufanya kosa

Kinachotuacha njia panda kwenye hii kesi ni swala la TFF kuiweka confidential kuzuia watu wasiweze kujua sheria iliyokiukwa tofauti na mashauri mengine yaliyowahi kutolewa ufafanuzi na kutoa fursa kwa wadau kuuliza maswali
 
Back
Top Bottom