Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
- Thread starter
- #101
Nisome vizuri ndio utanielewa.Wakati anakuja Yanga hao wanaomrubuni leo hawakumuona viunga vya Mchambawima? Wakati anakuja Yanga kipato alichokuwa anapata kilikuwa kikubwa kuliko alikokuwa kwenye timu za Zenji
Feisal wakati anakuja Yanga, nyuma yake kulikuwa kuna familia yake (hususani mama yake) na wanasheria wake. Na sasa anapotaka kuondoka Yanga, nyuma yake ipo familia yake na wanasheria wake. Ni ajabu kusema leo hii kuwa hao watu wanamdanganya Feisal wakati ni watu hao hao jana walikuwa nyuma yake.
Ukweli halisi, uwezo wa kisoka wa Feisal ni mkubwa huenda kuliko mchezaji mwingine yoyote wa Yanga, lakini mkataba wake kimaslahi ni mdogo kupita maelezo. Hivyo mchezaji kutafuta kuhama lilikuwa ni jambo ambalo haliwezi kuepukika.