Yanga kwa sasa inafaidika nini na kumng'ang'ania Feitoto?

Yanga kwa sasa inafaidika nini na kumng'ang'ania Feitoto?

Wakati anakuja Yanga hao wanaomrubuni leo hawakumuona viunga vya Mchambawima? Wakati anakuja Yanga kipato alichokuwa anapata kilikuwa kikubwa kuliko alikokuwa kwenye timu za Zenji
Nisome vizuri ndio utanielewa.
Feisal wakati anakuja Yanga, nyuma yake kulikuwa kuna familia yake (hususani mama yake) na wanasheria wake. Na sasa anapotaka kuondoka Yanga, nyuma yake ipo familia yake na wanasheria wake. Ni ajabu kusema leo hii kuwa hao watu wanamdanganya Feisal wakati ni watu hao hao jana walikuwa nyuma yake.

Ukweli halisi, uwezo wa kisoka wa Feisal ni mkubwa huenda kuliko mchezaji mwingine yoyote wa Yanga, lakini mkataba wake kimaslahi ni mdogo kupita maelezo. Hivyo mchezaji kutafuta kuhama lilikuwa ni jambo ambalo haliwezi kuepukika.
 
Hilo liko Wazi eng hersi alishasema wanaomtaka mchezaji Feisal waje meza ya mazungumzo ,lkn mpaka sasa hamna kiongoz yoyote aliyejitokeza kumtaka Feisal , Feisal mwenyewe haoneshi kutaka mazungumzo ya pande mbili ...
Hakuna mtu (klabu) yoyote aliyesema anamtaka Feisal, lakini Feisal yeye mwenyewe alisema anataka kuvunja mkataba wake na Yanga ili akatafute maisha yake mengine. Huo ni uhuru wake, na mkataba wake ulionyesha hilo linawezekana.
 
Yes linawezekana lakn mazungumzo hayakwepeki.. ingikeua ni hivyo bas wachezaji wengi wangevunja mikataba Yao pind wanapopata ofa na donge nono
 
Mwambieni basi afuate kilichoandikwa kwenye mkataba, siyo kuchomoa tu mstari mmoja na kukomaa nao.

Hata Biblia na Quran ukichomoa mstari mmoja tu ukatembea nao, lazima utapotosha watu
 
Huenda kuna kitu sikifahamu au labda nimepitwa. Mchezaji Feitoto alishaamua kuachana na Yanga na akawaaga na mashabiki, lakini klabu yake ya Yanga imeendelea kumng'ang'ania lakini haiwezi kumtumia, haimchezeshi, haimwamini nk

Nini mantiki ya Yanga kuendelea kumng'ang'ania Feitoto?
Wamegoma kuachika 😅😅mautopolo yanatia aibu sana
 
Yes linawezekana lakn mazungumzo hayakwepeki.. ingikeua ni hivyo bas wachezaji wengi wangevunja mikataba Yao pind wanapopata ofa na donge nono
Hujui kitu kuhusu release clause wewe, fatilia ishu ya Neymar, sio kila kuvunja mkataba eti lazima mkae mezani
 
Taasisi inaweza kukosea pia

Na ndio maana kwenye ishu ya Haier raisi wa Club amekiri kufanya kosa

Kinachotuacha njia panda kwenye hii kesi ni swala la TFF kuiweka confidential kuzuia watu wasiweze kujua sheria iliyokiukwa tofauti na mashauri mengine yaliyowahi kutolewa ufafanuzi na kutoa fursa kwa wadau kuuliza maswali
Watu kina nani? TFF wamesema tarehe 6 March watatoa mwenendo wa kesi ulivyo kua by the way hii sio public case hata wasipotoa cha msingi wahusika wameridhika vitu vingine mnavikuza
 
Watu kina nani? TFF wamesema tarehe 6 March watatoa mwenendo wa kesi ulivyo kua by the way hii sio public case hata wasipotoa cha msingi wahusika wameridhika vitu vingine mnavikuza
Umma

Namimi najua tarehe 6 wanatoa ila kwa wahusika na kesi tu

Hata Morrison haikuwa public case lakini haikuzuia kutoa taarifa kwa umma kuelezea namna walivyo hukumu kesi
 
Umma

Namimi najua tarehe 6 wanatoa ila kwa wahusika na kesi tu

Hata Morrison haikuwa public case lakini haikuzuia kutoa taarifa kwa umma kuelezea namna walivyo hukumu kesi
Umma wa nini? Kwani hili ni shauri la Umma? pia usitegemee TFF wakuwekee hadharani kila kitu kumbuka hayo ni mambo yanayohusu masilahi ya mtu binafsi hata habari za kuutoa mshahara wa Feisal hadharani ni makosa
 
Kesi ya Morrison ilikuwa ya Umma?
 
Dogo feitoto asipokuwa makini atashuka kiwango angefuata utaratibu tu
 
Katika hali ya kawaida, suala la ufanisi wa timu linategemea mahusiano ya hiari yaliyopo baina ya Timu na mchezaji husika. Timu ikimchoka mchezaji itatafuta namna ya kumuacha mchezaji na mchezaji akiichoka timu atatafuta namna ya kuondoka, kwa namna yoyote ile hiyo hali lazima ifikiwe.
Feitoto haitaki tena Yanga......
Yanga haina tena mpango wa kumtumia Feitoto.....

Sasa Yanga wanamng'ang'ania mchezaji wa namna hiyo wa nini?
Nilichgundua kwako unakaza fuvu tu mkuu,, jibu lipo wazi yanga haina nia ya kuwa na fei tena wala kumtumia ktk team yao ila wanachokisimamia yanga ni kulinda taasisi dhidi ya upumbavu.

Leo yanga wakikubali kumuacha kama unavotaka ww kesho wachezaji wengine wanaweza kutumia njia hii isiyo sahihi, wachezaji wengine wanaweza kuona ni njia sahihi kumbe wanakosea.

Kingine mbona mambo yapo wazi kwakua fei haitaki Yanga na yanga hawamtaki lkn ni mchezaji wao basi team inauomtaka iende ikaongee na yanga ili wauziwe mchezaji.
 
Kesi ya Morrison ilikuwa ya Umma?
Brother kesi ya Morrison ni moja ya mamia ya kesi hapo TFF unapo itumia kama reference labda uniambie kesi hizi zilikua public?
1. Ramadan Kesi Vs Simba
2. Emmanuel Okwi Vs Yanga
3.Yondani Vs Simba
 
Kesi ya Morrison ilikuwa ya Umma?
Wasi wasi wako ni nini hasa? umeambiwa tarehe 6 watatoa press release unaufahamu na mambo ya mahakama au unaleta ubishi wa vijiweni?
 
Brother kesi ya Morrison ni moja ya mamia ya kesi hapo TFF unapo itumia kama reference labda uniambie kesi hizi zilikua public?
1. Ramadan Kesi Vs Simba
2. Emmanuel Okwi Vs Yanga
3.Yondani Vs Simba
Point ilikuwa ni kukuonesha kuwa kesi ya mchezaji na Club haizuuii TFF kutoa ufafanuzi kwa Umma
 
Wasi wasi wako ni nini hasa? umeambiwa tarehe 6 watatoa press release unaufahamu na mambo ya mahakama au unaleta ubishi wa vijiweni?
Wewe ndio hujaelewa inaonekana hujasoma vizuri tangazo la TFF

TFF hawajasema kesho watatoa press release

Wamesema sababu za kiundani zitatolewa kwa wahusika wa pande zote mbili (Yanga na Feisal)

Screenshot_20230305-212507.png
 
Kwani feitoto hajafuata mkataba?
Mkataba umeweka vigezo vya kuuvunja ni fei kulipa million 100 na mshahara wa miezi mitatu
Kuna utaratibu gani tena?
Unafikiri kamati ya haki za wachezaji haina ethics mpaka wakaamua vile? Kimsingi watu wanachanganya mambo kwenye suala hili, hoja iko hapa kesi ilifunguliwa na Yanga sc wakiomba tff ithibitishe uvunjaji mkataba wa Feitoto ni halali?
Na tff wamesema mara mbili mbili kuwa haikuwa halali bali feisal bado mchezaji wa Yanga.
Sasa mwenye hoja hapo aende huko fifa aombe Yanga imwachie feisal bure aende Club aitakayo tuone kama fifa nao watakubaliana na uhuni huo.?
 
We jamaa ni mkali wa media?
 
Back
Top Bottom