Yanga kwenda kucheza CAF champions Zanzibar, JKU na UHAMIAJI wamekataa kuchezea Zanzibar, Kuna nini?

Yanga kwenda kucheza CAF champions Zanzibar, JKU na UHAMIAJI wamekataa kuchezea Zanzibar, Kuna nini?

Hao Uhamiaji na JKU kuhamisha mechi zao walipopangwa na waarabu wanajua wao nini kilichowasikuma kufanya hivyo. Lakini kikanuni uwanja wa Amani hauna changamoto yoyote kutumika katika mashindano ya CAF. Yanga hutumia uwanja wa Mkapa lakini kwasasa umezuiwa kutumika sababu ya kupisha ukarabati unaoendelea. Hivyo wana option ya kutumia uwanja wa Azam complex.

Kuamua kwenda Zanzibar kuchezea mechi yao, inaweza kuwa ni kutokana na uwepo wa mashabiki kwa idadi kubwa Zanzibar wanaoshabikia Yanga. Hata Zanzibar kuna shabiki wa Yanga
Irrellevant,ongelea kwa nini hizo timu za zanzibar zilikwepa kuchezea zanzibar
 
Yanga ni timu ya ligi ya Tanzania bara, Zanzibar Wana ligi yao. Ingekuwa sawa unachosema kama ligi ya Tanzania nzima ingekuwa Moja. Lakini kama Zanzibar imeruhusu JKU na UHAMIAJI wahamishe mechi zao Misri na Libya maana yake hawakujali faida (uchumi na kijamii) zote za timu kucheza mechi nyumbani. Faida hizo haziwezi kufidiwa na Yanga kwa mtindio wa strengthen the weakest by weakening the strongest. Unaweza kufanya hivyo kwenye ngao ya jamii, kiusalama au kupata mapato mengi kwa mechi kuchezea mji fulani.
Mbona una kichwa kigumu mzee, hayo sio mashindano ya ligi bali ni ya CAF na kama ni CAF hawana kanuni inayokataza timu isihame nchi yake. Mashindano ya CAF yapo huru sana, hata kama Yanga ingeamua kwenda kuchezea mechi yao nchini Tunisia.
 
Irrellevant,ongelea kwa nini hizo timu za zanzibar zilikwepa kuchezea zanzibar
Niongelee sababu za Uhamiaji na JKU wakati ni maamuzi yao binafsi ikiwa CAF hawakuweka sheria ya kutokuhama nchi? Uwanja wa Amani una hadhi ya kuchezewa mashindano ya CAF na isitoshe Zanzibar hakuna vita sasa unataka niseme nini kama sio mapenzi yao kuhama? Unless uje na maelezo kuwa uwanja wa Amani haukuruhusiwa kutumika ama Zanzibar ipo kwenye migogoro ya kivita.
 
Zanzibar ukiweka kiingilio 10,000 tu hawajazi uwanja uchumi wao uko chini wanategemea serikali zaidi.asilimia kubwa ya mechi hizi uwanja unajazwa na watu wa bara ingawa wanalazimika kuingia gharama kubwa za usafiri na malazi.
Labda kama kuna agenda nyingine.

Mechi zinazochezwa Dar, mashabiki wote hutokea Dar? Hakuna mashabiki wanaotoka Sumbawanga au Kigoma kuangalia mechi? Je hao wakitoka huko kuja Dar hawaingia gharama za usafiri na malazi?
 
Kaka ndio maana kila mkoa unapambana kupata timu ya ligi kuu ili kupata faida za kiuchumi na kijamii kupitia timu yao. Kilevi TU huwezi kuhamisha Fursa za watu wa dar ukazipeleka sehemu nyingi kwa utashi TU wa mwenyekiti.
Ondoa kwanza dhana ya kuichukulia kama Yanga ipo kwaajili ya Dar bali Yanga ipo kwaajili ya mashabiki wote dunia nzima. Sio watu wote waliopo Dar ni mashabiki wa Yanga hilo ulijue, na Yanga sio kitega uchumi cha watu wa Dar bali Yanga ni timu ya kuwapa burudani mashabiki zake waliopo kila pembe ya dunia. Acha kuwa mbaguzi wa timu, hizo mkoa hata zikipambana kuwa na timu ligi kuu lakini mtaji wao mkubwa ni Simba na Yanga basi. Kule Zanzibar kuna mashabiki wa Yanga wacha na wao wakapelekewe fursa.
 
Cha msingi yanga washinde magoli angalau 3 kule abebe Bikila maana uwanja wa amani yanga Haina bahati nao ni Ina struggle sana kupata matokeo
 
Mbona una kichwa kigumu mzee, hayo sio mashindano ya ligi bali ni ya CAF na kama ni CAF hawana kanuni inayokataza timu isihame nchi yake. Mashindano ya CAF yapo huru sana, hata kama Yanga ingeamua kwenda kuchezea mechi yao nchini Tunisia.
Huna ulichokisema cha maana. Yanga ni timu ya dar es Salaam, wanataka kufaidika na timu yao directly na indirectly. Kuna wanaonufaika directly kama waajiliwa, serikali (mapato na Kodi), uwanja, TFF, DRFA, TEFA nk na Kuna wanaonufaika na mechi za kimataifa za Yanga indirectly ( mahoteli, mamalishe, daladala, bodaboda, machinga, nk). Hawa wooooote huwezi kuwapiga mswaki eti kiongozi mmoja wa timu ana mahaba na kwao. Aliyesema Yanga ni timu ya Muungano ni nani?
 
Gharama nafuu kiveepe? Timu kwenda Zanzibar maana yake utalipa usafiri wa wachezaji, benchi la ufundi na msululu wa viongozi. Watu wote hao watalipiwa malazi, chakula na fedha za kujikimu (per diem) kwa siku zote watakazokuwepo Zanzibar na wakati huohuo bill za pango za Avic ziko palepale. Lakini Kuna watu Dar ambao walikuwa wapate Fursa za kibiashara kutokana na uwepo wa mechi uwanja wa Benjamin Mkapa watakosa hiyo fursa, na watu wa DSM na mikoa jirani ambao wanakuja dar kuona mechi hawatakuja.

Timu haina uwanja wa mazoezi lazima tujali kupunguza gharama za uendeshaji ili tujenge hostels na uwanja.
Kwa ajira kuna kitu kinaitwa kutengeneza activities zenye maslahi ya staffs kwanza then taasisi...wakati mwingine huwa kuna fungu lipo mahali flani sasa watu wanaangalia watalichomoaje ndo hapo inapopangwa mechi nchi ya kituo wakijua kwamba watalamba perdiem etc. (hapa inakuwa ufisadi)

Japokuwa kwa upande mwingine hizi timu zina mashabiki kila kona ya nchi hivyo kwa kuipeleka mechi kule inaweza ikachagiza kupata wanachama wengi in future pamoja na kwamba gharama iliyotumika kuwa kubwa hivyo mbeleni huko gharama zitakuwa zinarudi kupitia mauzo ya jezi na wanachama
 
Kama nchi walikubaliana kuwa JKU na UHAMIAJI wahamishe mapato na furaha nje ya nchi yao , ila watafanya mpango kuyapata mapato hayo kutoka Yanga, nonsense.
Niongelee sababu za Uhamiaji na JKU wakati ni maamuzi yao binafsi ikiwa CAF hawakuweka sheria ya kutokuhama nchi? Uwanja wa Amani una hadhi ya kuchezewa mashindano ya CAF na isitoshe Zanzibar hakuna vita sasa unataka niseme nini kama sio mapenzi yao kuhama? Unless uje na maelezo kuwa uwanja wa Amani haukuruhusiwa kutumika ama Zanzibar ipo kwenye migogoro ya kivita.
w
 
Hao Uhamiaji na JKU kuhamisha mechi zao walipopangwa na waarabu wanajua wao nini kilichowasikuma kufanya hivyo. Lakini kikanuni uwanja wa Amani hauna changamoto yoyote kutumika katika mashindano ya CAF. Yanga hutumia uwanja wa Mkapa lakini kwasasa umezuiwa kutumika sababu ya kupisha ukarabati unaoendelea. Hivyo wana option ya kutumia uwanja wa Azam complex.

Kuamua kwenda Zanzibar kuchezea mechi yao, inaweza kuwa ni kutokana na uwepo wa mashabiki kwa idadi kubwa Zanzibar wanaoshabikia Yanga. Hata Zanzibar kuna shabiki wa Yanga
Umemaliza Mkuu.

Uzi Closed!
 
Mechi zinazochezwa Dar, mashabiki wote hutokea Dar? Hakuna mashabiki wanaotoka Sumbawanga au Kigoma kuangalia mechi? Je hao wakitoka huko kuja Dar hawaingia gharama za usafiri na malazi?
Kwahiyo wanatoka sumbawanga waende Zanzibar kutazama mechi? Kwanini timu za Zanzibar haziji kucheza bara, Kuna nini? Nani anajikomba hapo?
 
Me naona ni sawa
Zanzibar Kuna wanachama wengi wa Yanga
Na hao wanachama wanalipia kadi kama wanavolipa wa Dar, kwahiyo kuwapelekea team Yao siyo jambo baya.
 
Aliyesema Yanga ni timu ya Muungano ni nani?

Kwani Zanzibar hakuna mashabiki wa Yanga? Unaposema sio timu ya muungano inamaana Yanga inapaswa kushabikiwa na wabara peke yao na kitendo cha kule Zanzibar kuwa na matawi ya Yanga ni makosa, kitendo cha viongozi wa Yanga kusajili mashabiki kule Zanzibar ni makosa?

2)Mjumbe wa baraza la wadhamini (Fatuma Karume) yupo Yanga kimakosa kwavile Yanga sio ya muungano?

3) Kama Yanga sio ya muungano imekuaje lile jengo la Yanga limejengwa kwa ushirika wa raisi wa Zanzibar Karume?

4) Kama Yanga sio ya muungano imekuaje wanaYanga wakawa na ushirikiano wa karibu na African Association ya Zanzibar, ukaribu ambao uliingia mpaka kwenye siasa za kutafuta uhurui wa bara na wa Zanzibar?
 
Me naona ni sawa
Zanzibar Kuna wanachama wengi wa Yanga
Na hao wanachama wanalipia kadi kama wanavolipa wa Dar, kwahiyo kuwapelekea team Yao siyo jambo baya.
Hao wanachama wapo nchi nzima na walikuwepo tangau enzi hizo lakini haikuwa hivi, hii ni mpya Yanga kugeuka taasisi ya muungano.
 
Kwahiyo wanatoka sumbawanga waende Zanzibar kutazama mechi? Kwanini timu za Zanzibar haziji kucheza bara, Kuna nini? Nani anajikomba hapo?
Hii mechi ya klabu bingwa ilichezewa bara
IMG_20240826_095814.jpg
 
Hao wanachama wapo nchi nzima na walikuwepo tangau enzi hizo lakini haikuwa hivi, hii ni mpya Yanga kugeuka taasisi ya muungano.
Yanga ni team ya wanachama
Na Zanzibar Kuna wanachama wengi wa Yanga wanaowajibika kulipia ada za uanachama
Kwanini unapambana wasione timu yao
 
Timu za JKU na UHAMIAJI ni timu za Zanzibar kindaki ndaki kuliko Yanga. Hatukuelezwa kwanini JKU na UHAMIAJI hawakutaka mechi zao za mashindano ya CAF wachezee Zanzibar, lakini Yanga wanataka kwenda kucheza CAF championship mzunguuko wa pili Zanzibar. Kuna nini hasa hapo?

Ufafanuzi unahitajika juu ya jambo hili. Michezo ni furaha, uchumi na undugu, kwanini JKU na UHAMIAJI walihamisha furaha, uchumi na undugu unaotokana na michezo kwenda Egypt na Libya na Yanga kupeleka Zanzibar furaha, uchumi na undugu Zanzibar kutoka dar es salaam?

Je, unawaweza kuwa mkatoliki safi kumzidi Pope?; muislam fafi kuliko mufti?
Labda Zanzibar kuna vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Wenye kwa hawapatiki halafu unakuta kuna timu kutoka bara ina jezi zimeandikwa Visit Zanzabar wakati Zanzibar wenyewe wanazuia fursa ya wageni kwenda kwao.
 
Back
Top Bottom