Yanga wameweka financial statements report yao juzi kwenye mkutano wao mkuu.
Ila kwa sisi wana uchumi wa brat na trap kuna sehemu haijaeleweka na tena viongozi wao wanajisifu kabisa.
Ni kwamba kwa mwaka wa fedha 2022/23 wameingiza faida ya million 500.
View attachment 2669309
Ukiangalia kwenye mapato yao wana deni la zaidi ya billion 4.8 ambalo ni sawa na 26.9% ya jumla ya mapato yao ya mwaka uliopita wa fedha.
Na ukiangalia hapo kwneye matumizi deni halijalipwa. Yaani ni nje ya mkopo mapato yao hayakuweza kutoshea matumizi yao so wakakopa. Kwa hiyo hiyo 500 millions ni kiasi kilichobaki kwenye mkopo.
Nnajua humu kuna wahasibu na wazoefu wa hesabu za fedha naomba kujuzwa hapa.
Ukiwa na deni unaweza kusema una faida ilhali deni hilo halijalipwa?
Au ni kujisahulisha tu lakini lazima deni liipwe mwaka mwingine wa fedha.