Yanga Sc 0-0 Simba SC| Ligi Kuu NBC | Benjamini Mkapa Stadium

Yanga Sc 0-0 Simba SC| Ligi Kuu NBC | Benjamini Mkapa Stadium

Jamani mbona hatuletewi vikosi ili sisi wachambuzi tuanze kuchambua mchezaji mmoja mmoja hadi na familia zao pamoja na michepuko yao
 
Kwa kweeli Mtani japo mmezidi kujihami aisee. 🤣🤣🤣
Raund ya kwanza kikosi kilikuwa ovyo sijui wachezaji wetu walichanganyikiwa kuondoka konde na Cham🤣. Angalau sasa tunaweza kunena kwa lugha japo tunawatisha kisaikolojia na uchawi wa moshi.

Si unajua mtani hata Bwana Yesu alisema, mtu akikupiga shavu kulia mgeuzie na la kushoto. Akiomba umsindikize mita 100 mpeleke 200. Sasa ndicho tunafanya, mnatusingizia uchawi ngoja tuwarahisishie muamini kuwa tunaroga. Tunawawashia moto live moshi utoke ili wachawi waamini wamerogwa.
 
Kwa kweeli Mtani japo mmezidi kujihami aisee. 🤣🤣🤣
Dakika 90 mtani ndio mwamuzi. Haya mambo haya utashagaa watu wanarukaruka tu uwanjani tofauti na matarajio ya mashabiki. 🤣

Tusubiri tuone, mwenye kisu kikali atakula nyama
 
Yanga kikosi
IMG_20220430_162535.jpg


Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
 
Mimi na washakaji zangu tunafanya rehearsal huku.😄😄
 

Attachments

  • 1636029012007.mp4
    1.4 MB
Mpira wa kibongo hovyo sana Imagine hata kutoa lineup wanategeana na wanajua kabisa sheria line up inatakiwa Azam media saa moja kabla ya game.
 
Back
Top Bottom