Yanga Sc 0-0 Simba SC| Ligi Kuu NBC | Benjamini Mkapa Stadium

Yanga Sc 0-0 Simba SC| Ligi Kuu NBC | Benjamini Mkapa Stadium

20220430_134200.jpg
 
Bikra ya yanga inaenda kalutobolewa hadharan na mkung wa mnyama
 
Naaam wasalam wakuu,

Ile siku maalumu iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu hatimaye imefika..Pambano la watani wa jadi katika soka la bongo, leo mtoto hatumwi dukani

Karibuni katika matukio mubashara(live updates) ya mtanange huu wa kukata na shoka baina ya mahasimu wa Soka la bongo, #KariakooDerby Yanga na Simba utakaochezwa saa 11 jioni Estadio De Benjamin Mkapa.

Huu ni mchezo wa namba 160 ligi kuu ya NBC 2021/2022 Yanga akiwa ni mwenyeji wa mchezo wa leo dhidi ya mtani Simba.. mchezo uliopita wa ligi kuu uliochezwa December 11, 2021, timu hizi zilitoshana au kuchoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana/Suluhu...0-0

Pia Simba mechi ya mwisho kimashindano imetoka kupoteza Penalti 4_3 kutoka Orlando Pirates mnamo tarehe 24/4/2022 na hivyo kufurumushwa nje ya mashindano ya kimataifa yaani katika kombe la Shirikisho Afrika. CAFCC.

Yanga ilicheza mechi ya mwisho ligi kuu na Namungo Fc tarehe 24/4/2022 na kushinda 2_1.

Watabiri wa mambo wanasema huu mchezo wa watani wa jadi unaweza kutoa taswira juu ya Ubingwa wa ligi kuu msimu huu..Yanga ikiwa kileleni mwa ligi na point 54 huku Simba akiwa na alama 41 (Tofauti ya point 13). Ni mchezo ambao unatarajiwa kuwa wa kasi, nguvu, akili, maarifa na uzoevu mwingi hasa ukizingatia timu hizi zinapokutana haijalishi nani yuko vizuri kwa form au kiwango, wachezaji hubadilika na kucheza soka la kiushindani sana....

Nani ataibuka kidedea? kaa nami hapa mwanzo, kati na mwisho kupata kila kinachojiri kutoka katika dimba hili lenye kumbukumbu nzuri ya Hayati Benjamin Mkapa Dar es salaam


NB: Je 'watatetema' au 'watatetemeka' tena? [emoji23]

_____________________________________________________________

Updates zaidi kukujia kadiri zinavyopatikana

Mwamuzi wa Mchezo wa Leo ni Ramadhani Kayoko na wasaidizi wake ( Frank Komba [Line1] & Mohamed Mkono [Line2] bila kusahau Elly Sasii [4th Official] ) ilivyotangazwa awali

Azam Tv kupitia chaneli ya Azam sports 1 HD watakuwa mubashara (live).

Kwa wanaotaka Link ikipatikana itawekwa hapa
-----------‐-------------------------------------------------

SIO RASMI utabiri Kikosi cha Simba kinachoanza (STARTING XI)
Manula,Kapombe,Zimbwe Jr,Onyango,Inonga, Mkude,Chama,Sakho,Morrison,Kagere,Bocco

Kocha: Pablo Franco Martin/Suleman Matola


utabiri wa Kikosi cha Yanga kinachoanza (STARTING XI)
Diarra,Shaban,Kibwana,Mwamnyeto,Job,Bangala,Aucho,Moloko,Ntibazonkiza,Feitoto,Mayele

Kocha: Cèdric Kaze
(Kocha Nasridin Nabi bado anatumikia adhabu ya kadi nyekundu kwa hiyo atakuwepo jukwaani)






------------------------------------------------------------------

Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
Hii mechi ya leo bora iwe droo au yanga apoteze, ila Simba akipigwa Msimbazi hakukaliki,lile swala la bil 20 lazima litaibuka.
 
Uzuri Yanga tunaingia tukiwa hatuna presha ya aina yoyote ile! Hata itokee Mo Fc wakapata ushindi, bado Bingwa wa msimu huu atabakia kuwa Yanga.

Halafu Yanga tumeshazoea kushinda! Kwetu sisi, sare ndiyo kupoteza/ kufungwa.
Yanga wanataka ubingwa bila kufungwa mechi hata 1
 
Back
Top Bottom